Kuna uwezekano mkubwa huko mbeleni Powercef (Ceftriaxone) ikashindwa kutibu kabisa kutokana na drug resistance

Kuna mtu aliambiwa ana UTI akaenda duka la dawa wakamwambia watamchoma Ceft siku tano.
aliponiambia nikamwambia hapana nenda kanunue vidonge vya Nitrofurantoin.
Karudi dukani yule mpuuzi anamwambia eti hivyo vidonge ni vikali sana. Choma tuu sindano.

Watu siku hizi wanaangalia pesa sana.
Ethics ni sifuri.

No body care about ethics, ni professionals wachache sana the rest is about profit
 
Ukosefu wa utu ,tamaa ya pesa na kutibu kwa kubahatisha.

Jinsi inavyotumika kiholela , bacteria watatengeneza usugu hivyo huko mbeleni hii dawa haita fua dafu na mbaya zaidi hauwezi tena kurudi tena kwenye first line drugs.
Inaewezakana pia Wagonjwa wabishi. Lakini pia na tabia ya kwenda Pharmacy wakati ilihitaji kupita hospitali kwa ajili ya kusikilizwa na kufanya test. Inashangaza sana, kwamba pharmacy wakuchome sindano, maadili gani hayo!

Lakini umesema mwenyewe, resistance, ujinga/ujuaji wa mgongwa (wagonjwa wa mjini wanataka kupona haraka) ukichanganya na ukiukwaji wa ethics za daktari, ni lazima utazalisha bomu!!

Umezungumzia resistance mbeleni, lakini hata sasa kwa baadhi ya Watu ceftriaxone inagongwa mwamba, wapo kwenye ceftriaxone+salbactam!
 
Linda afya yako kwa kuishi vema, usitegemee matibabu ya binadamu..... usigeuke fursa na mtaji kwa watu.
 
Inaewezakana pia Wagonjwa wabishi. Lakini pia na tabia ya kwenda Pharmacy wakati ilihitaji kupita hospitali kwa ajili ya kusikilizwa na kufanya test. Inashangaza sana, kwamba pharmacy wakuchome sindano, maadili gani hayo!

Lakini umesema mwenyewe, resistance, ujinga/ujuaji wa mgongwa (wagonjwa wa mjini wanataka kupona haraka) ukichanganya na ukiukwaji wa ethics za daktari, ni lazima utazalisha bomu!!

Umezungumzia resistance mbeleni, lakini hata sasa kwa baadhi ya Watu ceftriaxone inagongwa mwamba, wapo kwenye ceftriaxone+salbactam!
Huu uzi umenishtua sana.
Mimi nilichomwa hiyo ceftriaxone + sulbactam! Kwahiyo na mimi nitakuwa nimeingia kwenye kundi la uresistant?! Halafu hata haikunisaidia

Btw; ndo najua leo kama hiyo ceftriaxone ndio powercef
 
Irrational use of antibiotics itatutoa damu mbeleni very soon nowdays hadi mtetezi wetu Vanco kwa baadhi ya case post op infections imekua ni kubet
 
Huu uzi umenishtua sana.
Mimi nilichomwa hiyo ceftriaxone + sulbactam! Kwahiyo na mimi nitakuwa nimeingia kwenye kundi la uresistant?! Halafu hata haikunisaidia

Btw; ndo najua leo kama hiyo ceftriaxone ndio powercef
Kwenye dawa kuna generic na brand name, kama ambavyo Panadol ilivyochukua nafasi ya paracetamol.
Usihofu sana, kuna baadhi ya maambukizi (baada ya vipimo vya maabara) inabidi upate ceftriaxone+sulbactam. Lakini kujua kama ulihitaji hivyo, hilo anajua daktari wako. Wakati mwingine first line drugs zinaweza kutibu kabisa tatizo lako, au ukachoma sindano ya 'start' ceftriaxone au ceft+salb halafu uka-switch kwenye vidonge kawaida.

Nimeshuhudia mara kadhaa daktari anayependwa sana na Wagonjwa akiwatandika hayo ma-sulbactam au strong anti-biotic nyingine ili mgonjwa apone haraka!! (huyu nafikiri ameshajua 'wateja wake wanapenda nini..hahaaa).
 
Hiyo paragraph ya mwisho hiyo......
Huenda ina majibu sahihi. Maana mtu akipewa dozi kali akapona haraka, ataenda kumwambia na mwenzie. Hapo daktari atazidi kuwadunga midawa mikali, ili kumaintain status yake.
Huzuni
 
Usugu wa vimelea vitakuja kututesa sana saiv Amoxiline kwisha habari yake. Watu dawa wanawapa mpaka wanyama ,, usugu wa dawa ni jambo linalotakiwa kuchukuliwa sirias sana ,, itafika siku magonjwa yatakosa dawa. Tukumbuke kugundua dawa sio kazi nyepesi tulinde dawa tulizonazo
 
Mkuu ndungu yangu ana Chronic Umbrical Hernia Dawa yake itakuwa nini?
 
Hii dawa ya poweref (Ceftriaxone) kuna uwezekano mkubwa huko mbeleni ikashindwa kufanya kazi.

Hii dawa ni strong antibiotic yani ni kali sana na mara nyingi hutumika dawa zingine (first line drugs) zikishindwa kuleta matokeo mazuri mfano kwenye P.I.D , Cefixime ikishindwa kuleta matokeo tunaingia kwenye second line drug ambapo ndipo Ceftriaxone hutolewa.

Sasa sikuhizi hizi Ceftriaxone inatolewa kiholela sana , yani mtu akipata shida kidogo wanamchapa na Ceftriaxone, tena utakuta muda mwingine mtu tatizo lake la kiafya sio complicated anahitaji tu dawa ambayo haina nguvu sana lakini utakuta anachapwa na Ceftriaxone.

Sasa huko mbeleni hii dawa haitakuja kutoa matokeo mazuri maana inatumika kiholela mno.

Watu waache janja janja kwa tamaa za pesa , utakuta mtu ana Ki UTI ambacho ni uncomplicated anahitaji tu nitrofurantoin ila akikutana na mtu janja janja atachapwa na sindano za Ceftriaxone ili tu huyo mtu aingize pesa.

Sindano moja inafika kuanzia elfu 5 -elfu 20 kulingana na aina ya Ceftriaxone na mtu huyu dose yake ikamilike anahitajika achome kwa siku 5 mfululizo lakini kama muongozo ungefuatwa angepewa tu vidonge vya nitrofurantoin au hata amoxyclav na asingetumia zaidi ya elfu 10 kutibu tatizo lake.

Watoa huduma za afya kuweni na huruma na afya za watu .

Tena wengine wanaitoa hii Ceftriaxone mpaka kwa vitoto vidogo kabisa kitu ambacho ni hatari sana.
Chai
 
Kwenye dawa kuna generic na brand name, kama ambavyo Panadol ilivyochukua nafasi ya paracetamol.
Usihofu sana, kuna baadhi ya maambukizi (baada ya vipimo vya maabara) inabidi upate ceftriaxone+sulbactam. Lakini kujua kama ulihitaji hivyo, hilo anajua daktari wako. Wakati mwingine first line drugs zinaweza kutibu kabisa tatizo lako, au ukachoma sindano ya 'start' ceftriaxone au ceft+salb halafu uka-switch kwenye vidonge kawaida.

Nimeshuhudia mara kadhaa daktari anayependwa sana na Wagonjwa akiwatandika hayo ma-sulbactam au strong anti-biotic nyingine ili mgonjwa apone haraka!! (huyu nafikiri ameshajua 'wateja wake wanapenda nini..hahaaa).
Inasikitisha sana kwa kweli.
 
Back
Top Bottom