Kuna uwezekano mkubwa kombe la dunia Qatar kuhairishwa

Kuna uwezekano mkubwa kombe la dunia Qatar kuhairishwa

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Mzuka Wanajamvi!

Kutokana na hali ya vita huko Ukraine hali inazidi kuwa tete. Na leo kwenye hotuba yake Putin ameendelea kusisitiza hatanii kutumia mabomu ya nyuklia.

Na uwezekano wa kizitumia ni mkubwa kwasababu anapokea mkong'oto wa haja kutoka majeshi ya Yukrein.

Hii itasababisha vita ya tatu ya dunia kwasababu Yukrein naye anatuma maombi NATO.

Kuna uwezekano kombe la dunia Qatar kuhairishwa. Na siyo kombe la dunia ratiba ya vitu vingi vitabadilika dunianina kuvurugika. Mfano Biashara na soko la hisa usafiri na kadhalika.

Inachotupasa tuombeni amani. Huu mzozo au vita ya Ukraine utaisha tu katika meza ya mazungumzo. Kwasababu tunapoelekea Yani hata EPL nayo itasimama.
 
Urusi inatakiwa itambue, Ukraine ni nchi huru na yenye maamuzi yake;kama Urusi itaondoa majeshi, na kutokuingilia Ukraine kwenye maamuzi yao, vita itaisha; na hii itafanikiwa iwapo mpatanishi atatoka G7
 
Siku yule msemaji wa serikali ya Urusi aliposema' ndugu mtangazaji Ukraine tunaoijua na mipaka yake ya awali haipo tena ' ,watu wakajua haiwezekani lakini kupitia referendum iliyofanya baadhi ya majimbo kutambuliwa Rasmi kama maeneo ya Russia ndio watu wanaanza kupata akili na kutokana na kauli ya Putin kwamba watawalinda raia wa maeneo hayo kwa nguvu zote.

Pia kingine, Katiba ya Urusi inasema 'itamlinda raia wa Urusi popote duniani hata kwa kufuta kizazi cha binadamu' hapo bado ngoma mbichi sana
 
Urusi inatakiwa itambue, Ukraine ni nchi huru na yenye maamuzi yake;kama Urusi itaondoa majeshi, na kutokuingilia Ukraine kwenye maamuzi yao, vita itaisha; na hii itafanikiwa iwapo mpatanishi atatoka G7
Iraq haikua nchi huru? Vipi kuhusu Libya? Vipi kuhusu Afghanistan? Vipi kuhusu Syria na Yemen?

Si ni haohao wanaounda G7 ndio walihusika kuvuruga hizo nchi? Leo Ukraine kuna kipi cha ajabu ambacho hawakukifanya Libya na Syria?
 
Chukulia mfano, jirani yako akuambie sitaki nisikie unapika nyama hapo kwako; kama utafanya hivyo, nitachoma nyumba yako; Je, wewe utafanyaje, hutokula nyama kwa sababu yake?
 
Chukulia mfano, jirani yako akuambie sitaki nisikie unapika nyama hapo kwako; kama utafanya hivyo, nitachoma nyumba yako; Je, wewe utafanyaje, hutokula nyama kwa sababu yake?
Mfano wako hauna uhalisia. Mfano halisi ni huu:

Kuna wahuni kila siku wanatishia kupiga mawe na kuvunja madirisha ya nyumbani kwako. Alafu jirani yako anawakaribisha, na anakubaliana nao waje kuweka nyumbani kwake mafurushi ya mawe watakayotumia kuvunja madirisha yako.

Utafanyaje? Utamuacha jirani eti kisa anao uhuru wa kuamua mambo ya nyumbani kwake?
 
Back
Top Bottom