Kuna uwezekano mkubwa kombe la dunia Qatar kuhairishwa

Kuna uwezekano mkubwa kombe la dunia Qatar kuhairishwa

Iraq haikua nchi huru? Vipi kuhusu Libya? Vipi kuhusu Afghanistan? Vipi kuhusu Syria na Yemen?

Si ni haohao wanaounda G7 ndio walihusika kuvuruga hizo nchi? Leo Ukraine kuna kipi cha ajabu ambacho hawakukifanya Libya na Syria?
Yote hayo yalikua makosa.tutakua binadamu wajinga kuhalalisha makosa ya sasa kwa makosa ya zamani.Huu ujinga ukiachwa uendelee itafika siku dunia itaangamia kwasababu za kijinga za binadamu kufumbia macho ujinga unapofanyika.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ukweli sisi raia wa hii sayari tungejifikirisha vizuri ilitakiwa wote tuandamane kulaani kuendelea kwa vita huko ukrein.

Raia wa Marekani hadi Urusi kwenyewe bado wanaona kama nchi zao zina haki ya kufanya wanacho fanya.

Huko nchi za NATO vivyo hivyo, wanaona hayawahusu wanawaachia watawala kufanya wafanyayo.

Huku Afrika raia tunaishia ushabiki mara timu Russia mara timu Marekani.

Lakini hebu tujiulize ukubwa wa gharama iwapo patatokea vita vya nuklia. Nani atasalimika?

Si afadhali tuwapigie kelele watawala waache vita hivyo?
Uku afrika sisi ni ushabiki maandazi uliojengeka kwenye ujinga.kuna ushabiki uliojengeka kwenye chuki za kidini,wivu na matakataka mengine bila kujua waanga wakubwa tutakua sisi uku.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mnaingiwa na hofu bure kupitia biased sources. Biashara inafanyika hapo vita inaisha mambo mengine yanaendelea. Recall nyakati za nyuma miaka ya vita. Hakuna relevance yeyote kwa vita vya 3 vya dunia bali ni kupeana hofu isiyo na maana.
 
Kama sijasahau nimewahi kusoma sehemu kwamba Putin alikaririwa akisema kama Russia imefungiwa kushiriki mashindano ya FIFA basi atahakikisha kombe la dunia 2022 halichezwi.
 
Huu mfano haupo sahihi.


Nikuulize wewe, USA wanaweza kukubali Russia waweke makombora yao Mexico ?
Mexico ni nchi inayojitegemea, na iko huru kwenye maamuzi, haitakiwi kuingiliwa na nchi yoyote kimaamuzi; kwa hiyo kama Mexico watakubali, hakuna shida. Mfano, we unaweza kumpangia Uganda cha kufanya?
 
Mwamba Putin umejua kutufurahisha,15% ya Ukraine umeshaibeba.Hakikisha Ukraine inabaki na Kiev tu.

Slava Ukraine Slava Ukraine 😄😄😄😄😄😄😄😄😄
 
Mexico ni nchi inayojitegemea, na iko huru kwenye maamuzi, haitakiwi kuingiliwa na nchi yoyote kimaamuzi; kwa hiyo kama Mexico watakubali, hakuna shida. Mfano, we unaweza kumpangia Uganda cha kufanya?
Kwanini Russia ilipoweka makombora yake Cuba then USA ilitaka kuingia vitamin kwasababu haitaki hayo makombora mlangoni kwake?

Cuba sio nchi huru?
 
Kwanini Russia ilipoweka makombora yake Cuba then USA ilitaka kuingia vitamin kwasababu haitaki hayo makombora mlangoni kwake?

Cuba sio nchi huru?
Kwa ujumla kuna nchi zinazotumika kwa maslai ya nchi zenye uchumi mkubwa, kwa kifupi wanakuwa wametawaliwa.
 
Back
Top Bottom