Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,051
- 12,954
Hizi nchi zetu masikini ikitokea changamoto kidogo ni shida kubwa sana.
Tanzania inategemea mapato ya utalii kwa zaidi ya 25%. Utalii mwaka huu ni kama umekufa kabisa kama sio uko chini ya 2%. Hasa kipindi hiki cha March hadi June hua kuna watalii wengi sana nchi hii, ila sababu ya corona kila mtu anajua kinachoendelea.
Maana yake ni kua mapato ya utalii tumeyakosa na hata mwaka wa 2020/2021 ni vigumu kuyapata kwa sababu nchi karibu zote Duniani zimeathirika na chumi nyingi Duniani zitaporomoka. Kama kutakua na watalii ni wachache sana.
Kwa miezi 9 ya mwaa huu wa fedha TRA wamekusanya 10.9 Trillion ila tegemea robo ya mwaka huu, yaani March-June makusanyo kua madogo sana kwa sababu hakuna biashara, wafanyabiashara wengi wanaomba kufunga na mambo yameharibika. Hivyo mwaka huu tu ni changamoto kubwa. Kitakachopatikana chote kitaishia kwenye matumizi.
Kutokana na uchumi kuvurugika serikali italazimika kukopa zaidi na hiyo mikopo haitakua ya maendeleo, itakua ya matumizi kwa sababu hata makusanyo ya matumizi itakua ni changamoto. Serikali italazimika kuachana na miradi yake mikubwa ili kugharimia matumizi ya kawaida na ya lazima.
Kws mtazamo wangu, serikali italazimika kukopa ma moja ya masharti ili ipewe mkopo ni kuachana na miradi kama SGR na Stieglers. Ikitokea hivyo ujue mradi ndio utakufa au utachukua mida mrefu kukamilika. Naona yunaelekea huko.
Binafsi naunga mkono miradi kama Stieglers na SGR ila naona kuna uwezekano mkubwa sana corona kutia mchanga kitumbua chetu na kuturudisha nyuma kama sio kutumaliza kabisa.
Itakapotokea tukaweka nchi kwenye lock down ndio itakua mwisho ya hiyo miradi na mbaya zaidi uchumi hautakuja kuka vizuri hivi karibuni. Madhara ya corona kiuchumi yanaweza kuja kukaa vizuri baada ya miaka kadhaa mbele.
Hata wahisani wetu wa maendeleo sina hakika kama watatoa hela maana wao ndio wameathirika zaidi. Njia pekee itakua ni mikopo na mikopo hiyo itakua ni eitha WB au IMF, tegemea masharti ya kuachana na miradi kama hii.
Tusubiri tuone itakuaje.