Kwanza hakuna mahala nimesema napenda miradi isiishe. Rudia kusoma.
Pili, hiyo endemic unayosema historia inasema ni ipi hiyo iliyoikumba Dunia yote? Magonjwa yametokea ila yalikua yakiathiri nchi moja au eneo flani na sio Dunia nzima. Na pia hata hivyo miaka hiyo hata kama ilitokea Dunia haikua interconnected kama sasa.
Wachumi wanasema hii ni zaidi ya 2018 financial crisis au zaidi ya great economic depression ya 1929 wewe unasema haitachukua mwaka mmoja, hizi akili watu mnazitoa wapi? Hamkwenda shule?
Tatu, hizi least developed countries kama Tanzania hakuna vyanzo vipya vya pesa zaidi ya kodi, mikopo na misaada. Kodi yenyewe inatoka kwenye mfumo wa sekta binafsi dhaifu ambayo ikipata msuko suko hakuna mbadala zaidi ya mikopo na misaada, kutembeza bakuli na kuwalamba mabeberu makalio. Sasa hakuna beberu atakaekula hela ukajenge miradi kama hiyo, hapo watapata sababu ya kukubana, pia huwezi kujenga hiyo miradi huku watu wanakufa njaa, hakuna madawa, haluna vifaa tiba wala miundombinu muhimu. Mfumo wa sekta binafsi nchi hii ulishajifia kabla hata ya corona, sasa utazikwa tu.
Kama tunaomba tuendelee kuomba hali isiwe mbaya kama inavyotabiriwa, ikiwa hivyo huku kwetu hali itakua mbaya zaidi.