Kuna uwezekano mkubwa Mwamposa akawa na pesa zaidi kuliko Diamond Platnumz

Kuna uwezekano mkubwa Mwamposa akawa na pesa zaidi kuliko Diamond Platnumz

Huyu jamaa harakati zake za kusaka tonge si mchezo, ninashawishika zaidi kuamini kwamba ana pesa zaidi kuliko Diamond Platnumz.

Kama Samia atashinda uchaguzi huu, huyu jamaa utajiri wake utazidi kupaa na si ajabu akawa miongoni mwa watu (top 10) wenye pesa zaidi hapa nchini.

Gwajima ameteleza kidogo , angekaza angekuwa kamuacha mbali Mwamposa ila harakati za kisiasa zinamyumbisha sana.
Kongole Sana kwake, namkubali Sana huyu jamaa
 
Tutachekiana mkuu. ...mwisho wa siku watoto wetu waje kwenye makabur yetu waanze kulalamika , waanze kusema mzee ulishindwa hata kututoa kafara umekufa huna kitu
Mkuu ukicheka na yoyote utachekewa kaa kimasta
 
Huyu jamaa harakati zake za kusaka tonge si mchezo, ninashawishika zaidi kuamini kwamba ana pesa zaidi kuliko Diamond Platnumz.

Kama Samia atashinda uchaguzi huu, huyu jamaa utajiri wake utazidi kupaa na si ajabu akawa miongoni mwa watu (top 10) wenye pesa zaidi hapa nchini.

Gwajima ameteleza kidogo , angekaza angekuwa kamuacha mbali Mwamposa ila harakati za kisiasa zinamyumbisha sana.
Ana pesa kuliko Kikwete
 
Kama wewe si mtu wa aibu na unaweza Fanya chochote Kwaajili ya pesa basi TZ ni sehemu inayokufaa ilimradi tu umalizane na watu wa juu.
 
Katika wote hamna tajiri Ila wana hela nyingi.

Na katika hela nyingi , diamond Ana hela nyingi .

Kwakuwa Diamond kaweka mifumo Kama Wasafi media amabayo hata ikitokea hayupo duniani watu bado wataendelea kufaidika na ubunifu wake .

Ila Mwamposa yeye biashara yake ipo kimkakati Sana na anapata hela amabayo sio halali na wala haitolei kodi.
 
Kachupa kadogo ka mafuta tena ya kupikia kwa kigezo cha mafuta ya mzeituni ni buku. Juzi mama mmoja niliyemuonea huruma kaniambia kwenye bahasha kaweka 100000 shukrani kwa Mwamposa. Eti kavuna mazao yake vizuri. Wachina wanatucheka sana.
 
Back
Top Bottom