winnerian
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 408
- 638
- Chama cha Mapinduzi (CCM) kitambue kwamba kama kimeweza kuwamudu Watanzania kwa muda wote, basi ni juu yao sasa kuhakikisha kinatawala taifa imara lenye nguvu—na siyo taifa dhaifu.
CCM iweke mazingira na sheria ambazo zitastawisha Tanzania na siyo kuididimiza. Itafika mahali hata cha kuiba kitakosekana. Kima wazuri ni wale wanaotunza mahindi ya bwana shamba wakijua kabisa kuwa bwana shamba hatakiwi apate hasara ili msimu ujao alime tena na wao wale pale pale.
Lakini kima wajinga ni wale wanaokula mahindi yote ya bwana shamba leo na kesho wanakosa mahali pa kula mahindi.
Kwa ufupi, CCM tuwekeze kwenye uthabiti wa nchi na siyo chama pekee. Tuwe wakali sana kwenye suala la maendeleo ya Tanzania—ikibidi iwe zaidi hata ya China na CCP yao.
- Chama cha Mapinduzi (CCM) kiweke mfumo imara na wenye nguvu ndani ya chama, yaani kuwa na ustahimilivu wa hali ya juu kuanzia katiba, sheria, hadi kanuni za chama. Chama kipate watu wenye uwezo mkubwa na uzalendo wa kweli kwa taifa letu—na siyo kuokota mafisi na mamba wala watu wa mchana kweupe.
- Mfumo wa chama utenganishe makundi matatu kama ifuatavyo, na yasiingiliane kamwe kimamlaka:
A. Kundi la viongozi na watawala: Hili liwe kundi la kufanya maamuzi na kusimamia uadilifu na mwelekeo mwema wa maendeleo kwa chama na taifa kwa ujumla.
B. Kundi la wasomi na watafiti: Hawa wafanye kazi ya utafiti na kutoa mapendekezo ya kitaalamu ili kusaidia kundi la juu kufanya maamuzi sahihi.
C. Kundi la wafanyabiashara (wenye mitaji): Kundi hili litoe msaada wa kiuchumi na kujenga daraja imara la maendeleo ya uchumi wa taifa.
Makundi haya yote yasiingiliane. Kuwa na mgawanyo wa madaraka (power separation), huku kundi A likibaki kuwa na mamlaka ya juu zaidi. - Chama cha Mapinduzi (CCM) kiondokane na uendeshaji wa kifalme. Kila uongozi ujitegemee na usiwe na muingiliano kati ya uongozi uliopita na uliopo sasa. Hii italeta uwajibikaji wa kweli na uongozi ulio huru.
- Chama cha Mapinduzi (CCM) kitunge sera zitakazorahisisha uongozi wa nchi na siyo kujilia nchi. Maana kule mbele kitaishia kuongoza taifa la maskini wa kutupwa, jambo ambalo litafanya isiwezekane tena kuongoza kwa maana halisi ya uongozi. Nchi ikizama kwenye umasikini na maadili mabovu, CCM haitakuwa na msingi wa utawala.