Kuna uwezekano mkubwa sana tukaendelea na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa muda wote: nini kifanyike?

winnerian

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
408
Reaction score
638
  1. Chama cha Mapinduzi (CCM) kitambue kwamba kama kimeweza kuwamudu Watanzania kwa muda wote, basi ni juu yao sasa kuhakikisha kinatawala taifa imara lenye nguvu—na siyo taifa dhaifu.

CCM iweke mazingira na sheria ambazo zitastawisha Tanzania na siyo kuididimiza. Itafika mahali hata cha kuiba kitakosekana. Kima wazuri ni wale wanaotunza mahindi ya bwana shamba wakijua kabisa kuwa bwana shamba hatakiwi apate hasara ili msimu ujao alime tena na wao wale pale pale.

Lakini kima wajinga ni wale wanaokula mahindi yote ya bwana shamba leo na kesho wanakosa mahali pa kula mahindi.

Kwa ufupi, CCM tuwekeze kwenye uthabiti wa nchi na siyo chama pekee. Tuwe wakali sana kwenye suala la maendeleo ya Tanzania—ikibidi iwe zaidi hata ya China na CCP yao.

  1. Chama cha Mapinduzi (CCM) kiweke mfumo imara na wenye nguvu ndani ya chama, yaani kuwa na ustahimilivu wa hali ya juu kuanzia katiba, sheria, hadi kanuni za chama. Chama kipate watu wenye uwezo mkubwa na uzalendo wa kweli kwa taifa letu—na siyo kuokota mafisi na mamba wala watu wa mchana kweupe.
  2. Mfumo wa chama utenganishe makundi matatu kama ifuatavyo, na yasiingiliane kamwe kimamlaka:
    A. Kundi la viongozi na watawala: Hili liwe kundi la kufanya maamuzi na kusimamia uadilifu na mwelekeo mwema wa maendeleo kwa chama na taifa kwa ujumla.
    B. Kundi la wasomi na watafiti: Hawa wafanye kazi ya utafiti na kutoa mapendekezo ya kitaalamu ili kusaidia kundi la juu kufanya maamuzi sahihi.
    C. Kundi la wafanyabiashara (wenye mitaji): Kundi hili litoe msaada wa kiuchumi na kujenga daraja imara la maendeleo ya uchumi wa taifa.
    Makundi haya yote yasiingiliane. Kuwa na mgawanyo wa madaraka (power separation), huku kundi A likibaki kuwa na mamlaka ya juu zaidi.
  3. Chama cha Mapinduzi (CCM) kiondokane na uendeshaji wa kifalme. Kila uongozi ujitegemee na usiwe na muingiliano kati ya uongozi uliopita na uliopo sasa. Hii italeta uwajibikaji wa kweli na uongozi ulio huru.
  4. Chama cha Mapinduzi (CCM) kitunge sera zitakazorahisisha uongozi wa nchi na siyo kujilia nchi. Maana kule mbele kitaishia kuongoza taifa la maskini wa kutupwa, jambo ambalo litafanya isiwezekane tena kuongoza kwa maana halisi ya uongozi. Nchi ikizama kwenye umasikini na maadili mabovu, CCM haitakuwa na msingi wa utawala.
Ni hayo tu, comrades wenzangu.
 

Kwa sasa CCM ni 'Chama Tawala Cha Maisha' nchini Tanzania. Whether you like it or not!
 
Punguza mshahara wa wabunge kwa asilimia hamsini. Hio ndio dawa ya kuondoa tafrani hapa Tanganika.
Yaani ukisikia dawa mjarab ndio io.
 
Yamefanyika hayo hayo tangu uhuru mpaka 1992, hakuna kilichofanyika! Sasa hivi kwenye ulimwengu wa kukwapua, kupora, kuua, ili mradi watu wajilimbikizie Mali! Nani atayafanya hayo???
Mcheki marehemu JPM alipambana kufanya kazi kubwa ambayo inatakiwa ifanywe na serilkali [equitability] uliona walichomfanya!
Hapa cha msingi ni kwenda na mfumo huu wa vyama vingi!, kuna siku patasimama kwa strong parties zitakazochuana vyema na kuiletea nchi yetu maendeleo!
 
CCM wanatumia mfumo kandamizi wa unyumbu wa kisiasa ambao unaruhusi wanaopewa dhamamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), a.k.a kujizima data
 
Je, unadhani kuna uwezekano hili likabadilika?
 
Ni hayo tu, comrades wenzangu.
Mimi najibu swali lako la ni nini kifanyike. Kama umejiridhisha kuwa CCM tunayo Kwa muda mrefu, basi nashauri wale wote wanaodhani Wana mawazo chanya ya kulisaidia Taifa la Tanzania ambalo serikali yake inaongozwa na CCM, ni wakati muafaka Sasa kuwa wanachama wa CCM ili wapate nafasi ya kuwasilisha maoni yao na ama ikiwezekana wapewe nafasi za uongozi ndani ya CCM ( maana watakuwa wanachama) ili wasimamie utekelezaji wa ushauri wao watakao utoa

Nashauri wakuomba uanachama haraka sana ni Ndugu Tundu Antipasu Lissu, Ndugu Heche (Makamu Mwenyekiti Chadema), Mwenyekiti wa CHAUMA, pamoja na Wenyeviti na wanachama wa vyama vingine 17 vya siasa vilivyoandikishwa hapa nchini. Pia ningeshauri Hata viongozi wa TLS wachumue kadi za kielectronic za CCM ili waweze kushiriki vikao halali vya CCM ambapo watatoa mawazo Yao na yatatekelezwa kwa sababu yatakuwa ni maamuzi ya vikao.

Huo ndiyo ushauri wangu wa nini kifanyike maana CCM is here to stay 🙂🙂

Nakaribisha mashambulizi ya Kila namna, mwenye povu arushe tu Nina koti la mvua hapa...ha ha haa!
 
Wananchi wameichoka ccm
wameona watawale kibabe kwa nguvu ya dola
Tatizo ni mifumo ya sheria, taasisi na idara za serikali zote zina wanufaisha ccm
upinzbni bado hawana nguvu, raia nao waoga

MABADILIKO NI YA LAZIMA KULETA USAWA NA HAKI KWA WOTE KTK KUTAWALA NA KUGAWANA MALI ZA NCHI
 

Wazee ndani ya ccm hawataki kuwapisha vijana

Mfano. Wasira. Lukuvi. Majariwa.
 
Je, unadhani kuna uwezekano hili likabadilika?
Je waliopo ndani hawawezi kubadilika?
 
Wanachigani walioichoka CCM? Maana ingetakiwa kama wameichoka waandaname kwenye " no reform no election"
 
Wanachigani walioichoka CCM? Maana ingetakiwa kama wameichoka waandaname kwenye " no reform no election"
sasa tupo ktk hali ya no reform. Ikifika wakati wa no election ndio utaona hayo maandamano
 
Je, unadhani kuna uwezekano hili likabadilika?

Je waliopo ndani hawawezi kubadilika?
Wangekuwa wamebadilika. Umesahau maelezo ya Hayati Mzee DC Msuya mara hii? Juu ya vijana waliokwenye vyama visivyotawala?
 
sasa tupo ktk hali ya no reform. Ikifika wakati wa no election ndio utaona hayo maandamano
Tusubiri tuone lakini kwa wote wenye kutakia mema nchi yetu basi waitakie CCM mema na kuitakiwa kiwe chama chenye unchungu na maendeleo ya Taifa
 
Nashauri yeyote ambaye anadhani na kuona ana ushauri mzuri wa kusaidia mabadiliko (mapinduzi) kwa ajili ya kuliendeleza Taifa hili ajiunge CCM ili apate platform Sahihi ya kupitisha ushauri wake na kutekeleza. Kwa sababu tumeishaambiwa CCM hipo hapa kukaa(here to stay) Kwa muda mrefu.

Kukataa kujiunga na CCM ukijua una ushauri mzuri kulisaidia Taifa tunakujumuisha kwenye kundi la wasiolitakia mema Taifa hili na upo sawa na wale puppets wanaotumiwa na mabeberu kutuvuruga kama nchi.

Maneno muhimu Aya yakikuchoma vumilia ukishindwa Rusha tu povu nimevaa koti la mvua.
 
Tatizo liko Msoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…