Ukweli unabaki palepale.
Kwamba hakuna tena hiyo CCM unayoizungumzia kwenye mada hii.
CCM ilishakuwa mateka wa Genge la Samia. Hilo jina la CCM linatumika tu kama maonyesho ya hadaa.
Yote yanayofanyika sasa hivi kwa jina la CCM yanafanywa na hilo Genge lililokwisha kichukuwa chama hicho
Niambie ni kiongozi gani sasa hivi ndani ya chama hicho mwenye uwezo wa kutoa sauti; hata huko faraghani kwenyewe kuhusu haya yanayoendelea nchini?
Wote, ndani ya CCM unayoishikilia wewe juu ya hayo uliyo eleza kwenye mada mwenye uthubutu hata wa kuzungumzia tu hayo unayowataka kama chama wayajadili, wayapime au wayatekeleze; nani?
Genge la Samia na yeye mwenyewe; kwa kutumia jina la CCM wamekwisha fikia uamzi, kwamba Oktoba ni lazima iendelee vilevile; iwe mvua au iwe jua, hakuna kitakachobadilishwa.
Hiyo ndiyo njia pekee iliyobaki kwa Samia na Genge kuendelea kuwepo madarakani. Hakuna tena njia nyingine mbadala wa hiyo.
Ndiyo sababu wamejipanga kulipa gharama yoyote ili lengo lao litimie.
Mwanzo wa mipango yao walidhani, wakitisha watu kidogo, kwa kuwateka, kuwapoteza, au kuwaua, mambo yataanza kuwaendea kirahisi ifikapo Oktoba; kwa sababu waTanzania watakuwa na hofu na woga wa kuhoji chochote. Sasa hali imekuwa ni tofauti. Watu hawaachi kuhoji, na kupiga makelele, na kutoonyesha woga.
Kwa hiyo sasa iliyobaki kwa Samia na genge lake kutimiza lengo la kubaki madarakani, italazimu kuwakabili hawa watu kwa mitutu ya bunduki kabla na wakati wa uchafuzi wa Oktoba.
Je, CCM iliyotekwa, itaendelea kuwa mateka wakati wote huu?
Kumeanza kuwepo na maswali, huko huko CCM kwenyewe, na kuanza kutambua umateka wao. Akina Gwajima, watu ambao pengine hawakuwa na kubwa la kupoteza wameanza kuhoji. Kuna hawa wengine wazito kidogo, nao lugha zao, au kutokuwa na lugha kabisa kunaanza kutafsiriwa kuwa alama ya kuzinduka.
Ngoja tuone kitakachotokea kabla ya Bunge kuvunjwa.
Lakini, kwa vyovyote na iwavyo, sioni Samia akipata nafasi ya kuendelea kuwepo madarakani baada ya Oktoba
Yeye na Genge watahadaa wenzao kwamba amalize mitano yake kwa njia yoyote ile. Sioni hili litakavyo wezekana katika mazingira yanayofuata.
CCM watakuwa na bahati sana wakibaki na wabunge wengi wa kutosha; lakini hawatakuwa chama tawala tena.
NO REFORM, NO ELECTION.