Tetesi: Kuna uwezekano mkubwa wa LOCKDOWN nchi nzima. Kama hujajiandaa fanya sasa

Tetesi: Kuna uwezekano mkubwa wa LOCKDOWN nchi nzima. Kama hujajiandaa fanya sasa

Status
Not open for further replies.

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kwa hali inavyoendelea quarantine nchi nzima inakuja.. Inawezekana viongozi wamekubali ushauri na kijifunza toka kwa walioathirika kabla

Ni wazi muingiliano wa watu ndio kichokoo kikubwa cha kueneza virus wa corona.. Kusafiri, na kuhama sehemu moja kwenda nyingine.. Mizunguko ya siku nzima tunakutana na watu anuwai.

Toka kila sehemu.. Jioni tunarudi majumbani kwetu je tunakuwa tumesalimika kiasi gani?

Kukipambazuka tunaelekea makazini kwetu inawezekana kabisa wewe uko salama na umezingatia taratibu zote za kinga lakini je vipi jirani yako? Jana alipita wapi? Alikutana na nani? Je yuko salama? Je kazingatia tahadhari zote za kinga?

Muda unakimbia kwa kasi sana... Jiandae sasa, weka akiba ya chakula ndani, maji na kila chenye umuhimu... Tunaweza tusimalize wiki kabla hatujatangaziwa habari mbaya ya TOTAL LOCK DOWN... Hujachelewa anza sasa

Jr[emoji769]
 
Mmeshaandaa Videmu Vyenu vya Kujifungia Navyo ndani basi Mnaombea Lockdown kwa nguvu zote kwa kujifanya mnatabili kwa kutisha Watu..

Wiki moja Lockdown kwa Tanzania ni mateso makubwa kwa 95% ya wananchi
 
Ukweli ni huu hatumudu!! Familia nyingi ni kaa ndani ufe na njaa au toka nje ukatafute chakula.

Ngumu sana mtu kuvumilia kufa na njaa ndio maana hata mgonjwa hulazimishwa kula kwasababu kula ni sehemu ya tiba ya ugonjwa!!
So wajitafakari wanatakiwa watibu nini kwanza kabla ya kuleta tiba ya kukalisha kaliozetu ndani.
 
'Ni wazi muingiliano wa watu ndio kichokoo kikubwa cha kueneza virus wa corona.. Kusafiri, na kuhama sehemu moja kwenda nyingine..'

'Mizunguko ya siku nzima tunakutana na watu anuwai... Toka kila sehemu.. Jioni tunarudi majumbani kwetu je tunakuwa tumesalimika kiasi gani?'

'Kukipambazuka tunaelekea makazini kwetu inawezekana kabisa wewe uko salama na umezingatia taratibu zote za kinga lakini je vipi jirani yako? Jana alipita wapi? Alikutana na nani? Je yuko salama? Je kazingatia tahadhari zote za kinga?'

Muda unakimbia kwa kasi sana... Jiandae sasa, weka akiba
 
Tutakufa na kirusi cha njaa kabla ya virus vya corona
Hivi sisi wa hapa kwangu pakavu tia mchuzi ndio tunataka kuiga njia za kutatua matatizo wanazotumia wenzetu wenye uchumi uliosimama naona kama tunatafuta majanga zaidi
 
Kama watatoa kiroba cha mchele na dumu la mafuta ya kula, kiroba cha sukari na unga kila kaya basi lockdown itakuwa inawezekana. Kinyume na hapo ni chenga za mwili tu zitaendelea.

Na hii iwe kila mwezi bila kusahau kutuombea kwa wenye nyumba msamaha wa kodi kwa muda wa miezi 6!
 
Tuige kenya wao hawatoki usiku tu na wamezuia watu kutoka na kuingia nairobi. Lockdown hapa kweli itakuwa na madhara makubwa kuliko corona yenyew
Tusiige tu bali tuangalie je hyo njia imesaidia kupunguza maambukizi? Kumbuka kabla ya hyo half lock walikuwa na wagonjwa 15+ after action ndio wameongezeka na kuwa 120+

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom