Tetesi: Kuna uwezekano mkubwa wa LOCKDOWN nchi nzima. Kama hujajiandaa fanya sasa

Tetesi: Kuna uwezekano mkubwa wa LOCKDOWN nchi nzima. Kama hujajiandaa fanya sasa

Status
Not open for further replies.
Kwa hali inavyoendelea quarantine nchi nzima inakuja.. Inawezekana viongozi wamekubali ushauri na kijifunza toka kwa walioathirika kabla

Ni wazi muingiliano wa watu ndio kichokoo kikubwa cha kueneza virus wa corona.. Kusafiri, na kuhama sehemu moja kwenda nyingine.. Mizunguko ya siku nzima tunakutana na watu anuwai...
Toka kila sehemu.. Jioni tunarudi majumbani kwetu je tunakuwa tumesalimika kiasi gani?

Kukipambazuka tunaelekea makazini kwetu inawezekana kabisa wewe uko salama na umezingatia taratibu zote za kinga lakini je vipi jirani yako? Jana alipita wapi? Alikutana na nani? Je yuko salama? Je kazingatia tahadhari zote za kinga?

Muda unakimbia kwa kasi sana... Jiandae sasa, weka hakiba ya chakula ndani, maji na kila chenye umuhimu... Tunaweza tusimalize wiki kabla hatujatangaziwa habari mbaya ya TOTAL LOCK DOWN... Hujachelewa anza sasa

Jr[emoji769]
Kwetu sidhani mkuu,tumeona majirani serikali imemsaidia corona kuua raia wake,tuendelee kujikinga kwa kadiri inavyowezekana na kujiepusha kukaa kwenye misongamano,pia kama hauna issue ni bora kutulia home kama mimi ninavyofanya leo.

macson
 
[emoji30][emoji30][emoji30][emoji30]
kaka mshana naona utakuwa busy sana mwaka huu katika ofisi yako ya wafu.nahisi unatamani hata upate uhamisho italy au US.

Jr[emoji769]
 
70% ya watanzania tunaishi maisha ya ndege yaani tukishakwisha amka asubuhi hatujui leo rizki inatoka wapi .Sasa watupige hiyo LOCK DOWN si ndo watasababisha vifo vingi vya njaa kuliko ambavyo vingesababishwa na huyo covid19
 
Tutakufa na kirusi cha njaa kabla ya virus vya corona
Hivi afrika si wa hapa kwangu pakavu tia mchuzi ndio tunataka kuiga njia za kutatua tatizo wanazotumia wenzetu wenye uchumi uliosimama naona kama tunatafuta majanga zaidi

Afrika ni kubwa kuna nchi zipo kwenye lockdown ninavyotype.
 
Total lockdown ni impossible kwa mazingira yetu na viongozi wanafahamu hilo..
Solution ni kufunga biashara zote ambazo sio vital kwa survival kama maduka ya hardware ,maduka ya vyombo ,maduka ya simu n.k then waache maduka ya vyakula na maduka ya madawa tu..
Wakifanya hivyo watapunguza idadi ya watu wanaotembea tembea hovyo.
 
Tunacheza na ugonjwa huu.... njia nzuri zaidi ya kuepuka maambukizi ni social distancing.

Piga ua kama hatutaki cases zetu zifikie za nchi zingine lazima tufanye hili...kikubwa zaidi kwenye mipaka tunajitahidi ila waendeelee kukaza.
 
.
Kwetu sidhani mkuu,tumeona majirani serikali imemsaidia corona kuua raia wake,tuendelee kujikinga kwa kadiri inavyowezekana na kujiepusha kukaa kwenye misongamano,pia kama hauna issue ni bora kutulia home kama mimi ninavyofanya leo.

macson


Jr[emoji769]
 
Serikali ikiona umuhimu wa kuboresha mwenendo wake wa awali ni sawa.

Ila tufanye taratibu ambazo shughuli za uzalishaji zitafanyika na pia ugonjwa nao utapunguzwa kuenea.

Kwani kwa inavyoonekana tunaletewa badala ya ugonjwa wenyewe kuanzia hapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom