Kuna uwezekano wa dini zinazoweza kuja kuzipiku dini za Ukristo na Uislamu?

Kuna uwezekano wa dini zinazoweza kuja kuzipiku dini za Ukristo na Uislamu?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Katika historia inaonyesha kabla ya Ukristo na Uislamu baadaye kulikwa na dini kubwa za maeneo mbalimbali lakini hazikuwa dini za kidunia kama Ukristo na Uislamu ambavyo zimekuwa dini za kidunia.

Je kuna uwezekano zikaja dini nyingine zikapiku Ukristo na Uislamu na kuwa dini za kidunia au dunia ikarudia kama enzi hizo za dini nyingi mbalimbali za kimaeneo/ kijamii/ kikanda?
 
Tunakoelekea dini zote zitakufa, ndio maana kwa sasa wajanja wachache wanajitahidi kupiga hela kabla ya huo muda kufika.
Zamani, wengi walikuwa wanapenda dini kwa sababu zilikuwa zikitoa msaada kwa jamii wa kiuchumi, matibabu n.k, ila kwa sasa dini ndio zinachukua hela kwa jamii, kwa mazingira haya, hakutakuwa na dini huko tuendako.​
 
Kuanzia mwaka 2070, waafrika wengi watakua wameachana na hizi dini kwani watagundua ni za uongo.
2100 waafrika wataungana na kuwa taifa moja na kuanzia competition na watu weupe kwenye nyanja zote.
2250 wazungu watashindwa vita hiyo na kukimbilia sayari ya Mars.
 
D
Katika historia inaonyesha kabla ya Ukristo na Uislamu baadaye kulikwa na dini kubwa za maeneo mbalimbali lakini hazikuwa dini za kidunia kama Ukristo na Uislamu ambavyo zimekuwa dini za kidunia.

Je kuna uwezekano zikaja dini nyingine zikapiku Ukristo na Uislamu na kuwa dini za kidunia au dunia ikarudia kama enzi hizo za dini nyingi mbalimbali za kimaeneo/ kijamii/ kikanda?
Ukristo siyo dini. Ni imani.

Waliitwa kwanza Wakristo na Waarabu wa Syria.
 
Kabla, watu walikuwa fetishism na animism, walitoka huko wakaingia polytheism then wakaingia monothiesm na siku hiz wanaingia atheism. Habari mbaya ni kwqmba haiwezekan dini kufa sababu steji zote hizo kuna watu wanabakiaga hapo (survivals)

So kwa sasa threat ya dini ni maendeleo ya sayansi na teknolojia. Na hii ndo inazakisha atheists kwa kasi sana
 
Screenshot_20241011-083439_Chrome.jpg
 
Kwani nini maana ya dini ?
Neno "dini" linatumika katika maana kadhaa. Ya kwanza ni uhuru, nguvu, utawala, ufalme, au utawala. Ya pili ni kinyume cha hii, yaani kuwasilisha, utii, huduma au unyenyekevu. Ya tatu ni kuhukumiwa, kuhukumu, au kutoa malipo na adhabu kwa matendo. Matumizi haya matatu yanapatikana katika Qur'an.

HQur'an 3:19
Hakika dini ambayo Mwenyezi Mungu Aliwachagulia waja Wake na Akawatumiliza kwayo Mitume Wake na ambayo Hakubali isipokuwa hiyo ni Uislamu. Nao ni kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, Peke Yake, kwa kumtii na kujisalimisha Kwake kwa udhalilifu na kuwafuata Mitume katika yale waliotumilizwa kwayo katika kila kipindi mpaka wakahitimishwa kwa kuja Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ambaye, Hakubali Mwenyezi Mungu dini kutoka kwa yoyote, baada ya kutumilizwa kwake, isipokuwa Uislamu ambao alitumilizwa nao. Na tafauti baina ya Watu wa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, iliyowafanya watengane wawe mapote na makundi, haikutokea ela baada ya kuthibiti hoja juu yao kwa kupelekwa Mitume na kuteremshwa Vitabu; hiyo ilitokana na uadui na uhasidi kwa kutafuta ulimwengu.Na yoyote mwenye kuzikanusha aya za Mwenyezi Mungu zilizoteremshwa na alama Zake zenye kujulisha uola Wake na uungu Wake, basi Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa hesabu, na Atawalipa kwa yale waliokuwa wakiyafanya.
— Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis
 
Religion must go...

On the throne of time religion must perish.

A lie must surely perish.
 

Attachments

  • facebook_video_1728635825504.mp4
    2.8 MB
Back
Top Bottom