Kuna Uwezekano wa kusoma kuanzia cheti ukafika Degree?

Kuna Uwezekano wa kusoma kuanzia cheti ukafika Degree?

WanaJF naombeni mnijulishe kama mtu anaweza kusomea cheti hadi degree baada ya kumaliza kidato cha nne, na ni kwa kozi zipi hasa.

Ikiwezekana mnipe mifano hai?

Hiyo inawezekana sana, wengi wameshamaliza degree kwa kuanzia huko.
Mwingine ana PhD anafundisha chuo kikuu alianza na certificate.
 
Mimi kuna madactari nawafahamu(Dr. /Phd) walianzia huko, mmoja alifeli kidato cha nne akaanza certificate, akaja diploma, degree, mastershadi kuwa docta wa management na human resources na sasa kishatunukiwa uproff na dr. mwingine alianzia ualim wa shule ya msingi (grade 3A) hadi sasa ni dr wa kuheshimika. mwisho nina dogo alipata div 4 ya 28 na sasa yupo mwaka wa pili kozi ya IT. So sio lazima watu wote mpite njia rasmi na si kwel kwamba watu waliofel hawana akili/vilaza ila inategemea na vitu flan flan
 
Ubaya au changAmoto kubwa ya kutumia hiyo njia ni gharama yake ni kubwa zaidi ukilinganisha na kupitia fom five na six na pia unatumiA miaka mitatu kufika chuokikuu badala ya miaka miwili kwa yule aliepitia kidato cha 5 na cha 6.
 
Ndio tena njia ya cheti inafaa zaidi kwa maisha yetu ya nchi zinazoendelea kwakuwa ukianza na cheti let say ni ya marketing then unachukua Accounts kwa ngazi ya diploma na then bachelor unabeba let say Banking unakuwa unauzoefu kwakuwa kila ngazi uichukuayo unaifanyia field na unagain mambo mengi na uzoefu tayari unao na hata kazi unaweza fanya ukiwa bado upo chuo kwa kutumia vyeti vya CHETI, DIPLOMA tofauti na mtu alotoka direct from school hana ujuz wa kazi (experience) na atasoma bila job kwa mwaka wa kwanza then ataweza anza apply kazi second year tena kazi kma kibarua tu kwakuwa hana cheti.
 
raha ya kuanzia certificate hadi degree utaijua pale utakapoanza kutafuta kazi....kila kazi ikitoka we ni unaapply tu....ikitoka ya wanataka wa diploma unaficha cheti cha degree.....ikitoka ya degree una apply na cheti chako....Hivyo kupata kazi kwako itachukua mda mfupi sana....Demerits za kwenda form five and six Kuna POSSIBILITY KUBWA SANA ya kufeli form six then utakuja uanze diploma ukishafeli........chuo ni mpela mpela tu, ukikaza unachomoa ila necta unaweza ukawakazia na wao wakakukazia jombaaaa
 
Back
Top Bottom