Tatizo watu wengi hawajui kazi ya P2. Kazi yake sio kuzuia mimba directly wala kutoa mimba. Kazi ya P2 ni kuchelewesha yai kuja kwenye njia ya uzazi ready kwa ajili ya kukutana na mbegu ya mwanaume. Na ndio maana P2 husababisha mvurugano wa mzunguko wa hedhi kwa mwanamke kwasababu inaenda kuchelewesha utokaji wa yai. Kwahiyo kama yai lilikuwa limeshatoka au tumeseme mwanamke yupo kwenye ovulation wakati mnafanya sex basi hiyo P2 haiwezi kufanya kazi hata siku moja. Na pia kuna sababu nyingine kama uzito wa mwanamke zinaweza kuchangia P2 isifanye kazi ipasavyo.
JIBU: Kwa mpangilio wa hizo tarehe za period hadi kufanya sex, kuna high chances tarehe 16/17 alikuwa tayari ameanza ovulation (egg lilikuwa released on that day) kwahiyo P2 haikuweza kufanya kazi yake inavyotakiwa.