Kuna uwezekano wa Taifa Stars kusonga mbele?

Kuna uwezekano wa Taifa Stars kusonga mbele?

Joined
Mar 2, 2012
Posts
57
Reaction score
17
Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania, Taifa Stars yalejea Nchini na ushindi mwembamba wa 2-1 ikitokea Malawi na kueleza mkakati wake wa kusonga mbele inapoelekea kucheza na Algeria kutafuta nafasiya kufuzu kucheza kombe la Dunia mwaka 2018.

Kwa mchezo waliouonyesha Taifa Stars pindi walipocheza uwanja wa Nyumbani na kisha ugenini, unadhani kuna uwezekano wa na kusonga mbele?
 
Ukisema wahabeshi unamaanisha nn mkuu???
 
hapo ndio mwisho wetu, kwani Malawi ndio ilikuwa level yetu. huko kwingine kina kirefu sana.
 
Wahabeshi tena??jamani angalia usije ukaingia kwenye kapu moja la Magufuli,membe,na yule aliyewahi kuwa naibu wizara ya elimu kutoka mbeya,ALGERIA sio wahabeshi,na hapo ndio mwisho wa safari yetu timu bora Afrika.
 
Kwa rekodi za karibuni Algeria tulikutana nao kwao matokeo ni 1-1 na huku pia sare ingawa baada ya hapo jamaa walipanda sana kwenye chat na sis kushuka ila maajabu yanaweza tokea
 
Tunawategemea Samata Na Ulimwengu Watupe Ushindi,wao Timu Nzima Inategemewa Kuwapa Ushindi,tusijipe Moyo Tusibirie Miracle Tu.
 
Kwa rekodi za karibuni Algeria tulikutana nao kwao matokeo ni 1-1 na huku pia sare ingawa baada ya hapo jamaa walipanda sana kwenye chat na sis kushuka ila maajabu yanaweza tokea

Uwezo wa kuwafunga hawa jamaa tunao, wachezaji waandaliwe kisaikolijia zaidi kuliko hata kiufundi maana kiufundi vijana wako vizuri.

TFF iajiri japo kwa muda mtaalam wa kuwajenga wachezaji kisaikolojia kwa ajili ya mechi hizi mbili za Algeria. Tukiwatoa hawa bila shaka tutapaa sana katika rankings za FIFA.

CC. Jamal Malinzi (shughukia suala la saikolojia Mkuu, tutawapiga).
 
Last edited by a moderator:
Tunawategemea Samata Na Ulimwengu Watupe Ushindi,wao Timu Nzima Inategemewa Kuwapa Ushindi,tusijipe Moyo Tusibirie Miracle Tu.

Siyo kweli kwamba sisi tunawategemea wachezaji wawili tu watupe ushindi, haya ni mawazo potofu, tubadilike. Kila mchezaji anao mchango mkubwa sana kufanikisha ushindi hivyo timu inawategemea wachezaji wote.

Hakuna cha kusubiri miujiza, tujiandae kuwabamiza kipigo cha mbwa mwizi hadi Afrika na dunia nzima ishangae, huu ndio muda muafaka wa kudhihirisha ubora wa soka letu.
 
Algeria tutawashinda. Hawatatufunga hata mechi moja. Kwa Stars ndio mwisho wao. Mkwasa ndiye mwisho wa manung'uniko yetu. Stars tunawaamini
 
Kwa kulinganisha hizi timu mbili ni kama tumetoka lakini mpira hauko hivyo.Nazikumbuka mnoo game za South Korea na Spain,South Korea na Italy- World cup2002.Na nikiwa kama mchezaji niliecheza mpira kwa mafanikio ya juu na kiwango kikubwa nawapa turufu starz ya kusonga mbele.
 
Wachezaji wa taifa stars si kanakwamba hawajui mpira..kujituma na kujitambua tu ndio kutafanya tufike mbali mwaka huu
 
hakuna kisichowezekana katika mpira kama timu ikijiandaa vizuri, serikali nayo ikawajibika huku sisi mashabiki tukiwaunga na kuwatia moyo wachezaji.

timu yetu siyo mbaya japo inatakiwa marekebisho katika maeneo kadhaa ya umuhimu. kuna umuhimu wa mtu kama jonas mkude au salum telela wakawa wanachezeshwa nafasi ya holding midfield ambayo bila kificho kwa sasa hapa nchini tanzania hawa wachezaji wawili wanastahili japo abubakary salum sure boy naona maumivu yamemmaliza ila hata yeye nae humudu vizuri mno hiyo nafasi.

hata hivyo kwakuwa tumempa mkwasa timu sasa rasmi na mkataba wa mwaka mmoja basi tusimpe presha na badala yake tumwamini na tumpe jukumu la kututengenezea kikosi cha afcon kijacho na hata cha kombe la dunia la mwaka 2022 ila kiutaalam kombe la dunia hili la urusi tutakuwa kama vile tunalazimisha kwenda peponi wakati tuna dhambi nyingi tu ila tuzitumie tu hizi mechi kuwapa experience na exposure wachezaji wetu.
 
Siyo kweli kwamba sisi tunawategemea wachezaji wawili tu watupe ushindi, haya ni mawazo potofu, tubadilike. Kila mchezaji anao mchango mkubwa sana kufanikisha ushindi hivyo timu inawategemea wachezaji wote.

Hakuna cha kusubiri miujiza, tujiandae kuwabamiza kipigo cha mbwa mwizi hadi Afrika na dunia nzima ishangae, huu ndio muda muafaka wa kudhihirisha ubora wa soka letu.

hata goliath alipigwa na daudi,anything may happen lets wait and see
 
Inawezakena kushinda hiyo mechi iwapo;Wachezaji wetu wakicheza kwa ari na bidii ,Wasiruhusu adui kumiliki mpira hata kidogo kwa kutibua mbinu au formula za timu pinzani(hii itawachanganya sana wapinzani wetu)
Muhimu timu iwe na stamina na pumzi ya kutosha kukimbiza na kukaba mwanzo mwisho.
 
Algeria tutawashinda. Hawatatufunga hata mechi moja. Kwa Stars ndio mwisho wao. Mkwasa ndiye mwisho wa manung'uniko yetu. Stars tunawaamini

jinsi nilivyowaona Aljeria kwenye kombe la dunia na jinsi nilivyowaona Stars kule Malawi, kazi tunayo.
 
Back
Top Bottom