DOKEZO Kuna uzembe mkubwa Makao Mkuu ya Utumishi Dodoma, ila hakuna wa kuwawajibisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

SayiG

New Member
Joined
Jul 29, 2026
Posts
1
Reaction score
3
Leo nimejionea kwa macho yangu pale Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Utumishi (OR-Utumishi), Dodoma, na kuthibitisha kwamba, kwa uzembe uliopo pale ofisini, hakuna mtu yeyote anayewaadhibu Maafisa Kazi na Maafisa Utumishi waliopo pale UTUMISHI-HQ. Ndiyo maana hawawajibiki ipasavyo.

Si Rais, Waziri Kikwete wala Ndg. Mkomi (Katibu Mkuu) wanaoweza kuwadhibiti watumishi waliopo pale, kwa sababu karibu maafisa wote wamepelekwa kufanya kazi pale kupitia vigogo wa nchi. Hawa viongozi wataendelea kupiga kelele mitandaoni za kuwaridhisha watumishi wao na wananchi, lakini watendaji wao ni watu wa hovyo sijapata kuona.

Nimemshuhudia dada mmoja aliyetokea Mwanza akilia kama mtoto mdogo baada ya hao Maafisa kumkatalia kuonana na Katibu Mkuu, wakisema hana appointment ya kuonana naye, wakati huo huo suala lake la uhamisho ni mara ya nne sasa anasafiri kutoka Mwanza kwenda Dodoma. Akifika Ofisi ya Rais, Utumishi, wanaishia kumpatia maneno ya kisiasa ili kumfariji ili arudi mkoani, na wanampatia namba zao za simu zisizopatikana au zikiita, anasema hazijawahi kupokewa.

This time around, dada wa watu (Mtumishi) alijipanga apeleke kilio chake kwa Katibu Mkuu, lakini wamegoma kumruhusu. Hivi, mtumishi anapataje appointment ya kuonana na Katibu Mkuu?

Mtumishi mwingine nimemkuta anafuatilia ombi lake la uhamisho ambalo, baada ya kupitishwa katika hatua zote kuanzia kwa mwajiri wake na kupokelewa Ofisi ya Rais, Utumishi, ombi lake lipo hapo OR-Utumishi mwezi wa nne sasa na hakuna chochote walichoshughulika nacho. Majibu anayopewa ni kwamba ombi lake lipo kwenye process.

Alipolazimisha kuonana na Mkurugenzi wa masuala hayo ya uhamisho, akajibiwa (na Mkurugenzi) kuwa pamoja na kwamba ombi lako lipo kwenye mchakato na pamoja na kwamba majukumu ya nafasi unayoomba yanafanana na majukumu yako ya sasa, lakini cheo ulichonacho ni kikubwa kuliko cheo cha nafasi iliyopo (iliyotangazwa kuhamia), hivyo akamshauri arudi kwenye ESS yake aka-cancel ombi lake kwa sababu hawezi kupata uhamisho. Badala yake akamwambia akatafute nafasi nyingine ya kuhamia ambayo ina majukumu sawa na anayoyafanya na cheo cha hiyo nafasi kifanane na cheo alichonacho yeye.

Kuna visa vingi sana nimeviona pale HQ vinavyohusiana na changamoto mbalimbali za watumishi, hususani kwenye eneo la UHAMISHO. Watumishi wengi niliozungumza nao wamesema ni bora utaratibu wa zamani wa kuomba uhamisho kupitia waajiri wao urudi, kwani wanasema pamoja na kwamba ulikuwa na rushwa nyingi, lakini watu walikuwa wanahamishwa.

Nilimsikia mwingine akisema watumishi waliopo Serikali za Mitaa, ambao wanahudumiwa na Katibu Mkuu wa TAMISEMI kwa niaba ya Katibu Mkuu OR-Utumishi, wana nafuu sana kuliko wale wanaohudumiwa na OR-Utumishi moja kwa moja.

Baada ya hadithi hizi kutoka kwa watumishi na urasimu niliouona pale, hata mimi binafsi nikaamua kuishia njiani na kurudi zangu Tabora.

MY TAKE:​

1. OR-UTUMISHI wamenyang'anya majukumu ambayo wameshindwa kuyatekeleza ipasavyo, hususani kwenye eneo la uhamisho wa watumishi. Hii ni aibu kubwa kwao kuwa chini ya Ofisi ya Rais. Viongozi wafuatilie haya niliyoyasema, watakutana na ukweli.

2. Rais afahamishwe kuhusu hizi changamoto, kwani mahubiri ya kila siku mitandaoni kutoka kwa Mhe. Kikwete, Waziri mwenye dhamana, Naibu Waziri wake, Katibu Mkuu na Naibu wake yamekosa tija, hayatekelezwi, ni dharau na aibu kubwa kwao. Kwa aibu hii, nashauri UTUMISHI iondolewe chini ya Ofisi ya Rais.

3. Kila Afisa pale OR-Utumishi anasingizia tatizo la mtandao kwenye hii mifumo yao ya utumishi, ikiwemo ESS. Kama ndivyo, basi OR-Utumishi haina wataalamu wa TEHAMA, wakati wataalamu wamejaa mtaani. Fukuzeni maafisa wanaoshindwa majukumu yao, ajiri wapya.

4. OR-Utumishi imekosa kitengo cha kuwatetea watumishi wenye shida. Mtumishi anatoka mikoani kwa ajili ya kuonana na mwajiri wake (Katibu Mkuu), Afisa wa Wizara anamwambia kwa sababu huna appointment huwezi kumuona, wakati Katibu Mkuu yupo ofisini.

Ombi la uhamisho wa mtumishi limewafikia OR-Utumishi na kukaa ofisini kwao zaidi ya miezi 4 bila kufanyiwa kazi, halafu Mkurugenzi anamshauri mtumishi aliyetoka mkoani kwamba nenda kafute ombi hilo kwa sababu unakosa sifa, lakini hamuoneshi kwamba akaombe nafasi ipi na inapatikana katika taasisi gani. Hii ni zaidi ya dharau kwa watumishi wenye shida, lakini hawana wa kuwatetea.

Niombe kila mmoja apaze sauti juu ya hizi changamoto ili watumishi wapone.

Naomba kuwasilisha.
 
Kwa hali hii mbona tunatesana wenyewe kwa wenyewe, Wahusika wajaribu kuwasaidia hao wahanga

Poleni sana.
 
Lengo la huo mfumo wa kieletronic wa uhamisha halikuwa kuwarahisishia watumishi kuhama kama ma boss walivyoupigia debe.

Lengo halisi lilikuwa kuwafanya watumishi wasihame kirahisi ili wengi wabaki vituoni kwao. Wakikubaliwa kuhama kirahisi Kuna vituo, hasa vya vijijini vitakosa watumishi.
 
Mtafute mh RIDHIWANI Kikwete hanaga mbamba kama unasababu za msingi. Mungu amjalie aje kuwa rais wetu
 
Back
Top Bottom