dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483
Salaam wakuu,
Kumekuwa na video mitandaoni ikionesha polisi/traffic wa Inyala, Mbeya wakimshusha kwa nguvu dereva wa lori na kumuangusha chini, na baada ya hapo imeripotiwa dereva huyo amefariki. Tunaomba mamlaka husika itolee majibu sintofahamu hii, na ni nini kinachopelekea matumizi ya nguvu kubwa namna hiyo kwa askari wa usalama barabarani?
Hiyo video imeonesha dereva akiwa amevuliwa suruali nusu hadi magotini.
Hii ni post ya dereva wa magari makubwa kuhusiana na hii:
"Habarini za mida wapambanaji wenzangu nimesikia mahala kua kuna dereva kapigwa na askari wa usalama barabarani huko Mbeya na amefariki alipokua sero. Je, imekaaje hii viongozi wetu? Kama ni kweli mbona tunafanywa kama nguruwe tukiwa barabarani? Mimi huea nadhani nikikutana na askari wa usalama barabarani najua nimekutana na nipo salama lakin sasa kwa staili hii tunapelekwa wapi? Makosa watubambikie na hauna pakwenda kulalamika hasa ukishapigwa cheti, kutupiga watupige ndio; na kifo?
Polisi kama kweli mmelifanya hili, hampo sahihi ndugu zetu. Kumbukeni mapolisi wengine mmesomeshwa na baba ambaye ni dereva. Pia je, wakati unasoma usikie baba yako amepigwa na police, ungejisikiaje?
Tubadilikeni maaskari; hicho ni cheo tu. Sisi na ninyi wote ni sawa. Tofauti yetu isikufanye kumuona dereva ni adui yako. Mmefundishwa kutenda haki, tendeni haki ndugu zangu. Haya, Mwenyezi Mungu awabariki. Labda mlichokitaka ndio hicho.
Pumzika kwa amani mpambanaji mwenzetu, mbele yako nyuma yetu"
Tunaomba kujua kama kuna ukweli wowote juu ya video hii.
UPDTAES: 30 JANUARI 2021
Polisi Mbeya wadai dereva wa lori alikuwa na homa ya mapafu
Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema dereva wa lori, Abrahaman Hussein (61) aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kumkamata alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu.
Hayo yameelezwa leo Jumamosi Januari 30, 2021 na kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Jerome Ngowi akibainisha kuwa Hussein akiwa njiani alijisikia vibaya na madereva wenzake walimpeleka hospitali ya Chimala na baada ya vipimo alikutwa na ugonjwa huo.
Amesema kwa mujibu wa maelezo ya Peter Kigombola ambaye ni daktari aliyempokea, baada ya kugundua hali hiyo aliwaeleza anapaswa kutengwa na kulazwa.
Amesema kauli ya daktari huyo ilipingwa na madereva waliompeleka Hussein hospitali na walimchukua wakidai atakwenda kutibiwa katika hospitali iliyopo mamlaka ya mji wa Tunduma Mkoa wa Songwe.
Amebainisha kuwa baada ya kutoka hospitali hiyo, Hussein aliendelea kuendesha gari huku akiyumba barabarani na aliyagonga magari mengine na wananchi walitoa taarifa kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani kituo cha Inyara wilaya ya Mbeya.
Ngowi amesema baada ya kulizuia gari hilo walimwamuru Hussein kuteremka lakini alikaidi, askari wakalazimika kutumia nguvu kumshusha na kumpeleka kituo cha polisi.
“Kadri muda ulivyokwenda hali yake ilizidi kudhoofu.
na hivyo askari waliokuwa zamu wakalazimika kumkimbiza kwenye kituo cha afya cha Igawilo kwa matibabu lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia,” amesema.
Wakati polisi wakieleza hayo, mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa malori Tanzania, Abubakar Msangi ameomba kamati ya uchunguzi iliyoundwa na mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kukamilisha uchunguzi wake na kutoa taarifa sahihi za chanzo cha kifo cha Hussein.