Kuna Video iliyokuwa ikionesha Polisi/traffic wa Inyala, Mbeya wakimshusha kwa nguvu dereva wa lori. Polisi wadai amekufa kwa homa ya mapafu

Kuna Video iliyokuwa ikionesha Polisi/traffic wa Inyala, Mbeya wakimshusha kwa nguvu dereva wa lori. Polisi wadai amekufa kwa homa ya mapafu

Ila madereva wa malori huwa ni wakorof na wana lugha za matusi Sana,mi naona sawa tu, sheria isipofuatwa mtu lazima awajibishwe,
 
Story ya kusikitisha sana. Mamlaka husika ziingilie kati kutatua matatizo haya kabla hayajawa utaratibu wa kila siku.
 
Daah, naomba nijibu kitaalam zaidi. Katika saikolojia ya binadamu kuna kitu kinaitwa ‘Compensation behavior’, hii huonyeshwa hata na mtoto wa shule ambae anashindwa kung’ara katika masomo na badala yake anaamua kung’ara kwa njia zingine, mfano kupiga kelele darasani, kuwa mkorofi darasani, kujifanya comedian nk.

Tukirudi kwa hao form 4 failure, nadhani sasa inaeleweka why wanafanya hivyo..
Nimekuelewa vizuri sana
 
Niliwahi kumtafuta mtetezi wa Madereva lakini sikuwahi kumpata. Tajiri anaijali mali yake dereva kwake ni mbwa tu, trafiki anaijali buku buku wanayowekewa kwenye kadi ya gari.
 
Kwani ni.lazima kushuka kwenye gari?? Kama umetii na umesima...wakataka leseni ukawapa? Kwa nn wakushushe kwa nguvu kwenye gari mpaka kupelekea kifo?
Haki itendeke
 
IGP Simon Sirro najua kwa sasa utakuwa jijini Dar tena kwenye sherehe ya kuwatunuku baadhi ya vijana wako kuhitimu mafunzo.

Tafadhali issues kama hizi zinadhalilisha jeshi lako na kukuweka kwenye tanuru, hebu toa mfano kwa hawa vijana wako kwa kitendo hiki.



NB:
Vaa barakoa, nawa mikono kwa sabuni na maji tiririka pia uwe mbali na mikusanyiko.
 
Baadhi ya Askari polisi Ni tatizo Sana..wanajionaga Kama miunga watu wakati matatizo yamewajaa Hadi kichwani.
 
Nimejikuta machozi yamenilenga lenga tu. Kwakweli ndugu wa marehemu Mungu awape uvumilivu mkubwa sana sana. Poleni madereva wote najua vile mnajiskia lkn kila mtu kwa imani yake amuombee marehemu pumziko la milele. Lkn sote tupaze sauti kukemea huu Udhalimu wa Kikoloni.
 
Huyu TBI imemsombaa pale alipodondoshwa toka kwenye garii...!! Yani Polisi hawa wanavuta mtu kama mbwa kwelii as if ni gunia la mahindi.. inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom