Yenga08
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 458
- 894
Habari zenu wanajamvi,
Poleni na majukumu na ninaimani Muumba wetu amejaalia tumeamka salama, kwa wale wenye kujisikia kuumwa poleni sana.
Kuna vitu vingi sana vinafikirisha katika Taifa letu. Kwanza kabisa kwa nin mtawala huwa hakili makosa yake inapotokea kakosea, na inapotokea mtu kuikosoa serikali anaonekana mpotoshaji na atashambuliwa kutoka kila kona hususani wale wanaopata ugali kupitia mamlaka.
Ikitokea tu ukaanza hata semina na uelimishaji juu ya haki za msingi za raia, Maliasili za serikali na namna zinavyotakiwa kuendeshwa, Mambo ya muungano nayasiyo ya muungano, ukomo wa mtawala juu ya mamlaka yake kwa raia, utaonekana MCHOCHEZI, huwa ni uoga au ndio ile ukitaka kumtawala raia mnyime vitu vitatu ELIMU, UHURU NA FEDHA yaani aendelee kuwa masikini.
Swali la kujiuliza, hivi hata kule kwa wenzetu Nchi zilizoendelea huwa kuna haya mambo kweli, kwanini mambo haya yawepo nchi za watu weusi tu yaani Africa.
Inaweza kuwa sisi weusi niwabinafsi sana, wanafiki sana, tunaendekeza njaa sana, tunafikilia leo tu na hatuna malengo ya mda mrefu kama miaka 20 mpaka hata miaka 70 au katiba zetu ndio tatizo.
Maana kama kiongozi unatakiwa uwe na dira maalum, watu wako unataka wafike wapi baada ya miaka kadhaa, na dira hiyo inatakiwa hata akija mwingine akanyage mle mle alipokanyaga mtanguliz wake na kama nimabadiliko ni kidogo sana. Lakin Afrika akianza huyu then akaja mwingine anakuja na mtizamo wake mpya kabisa na anakwambia hiki na hiki siyo priority yangu.
Siyo dhambi kuchungulia kwa jirani kuona anafanyaje mpaka anapata mafanikio, kama kuna watu wanamkosoa hata Mungu sembuse wewe uliyetoka mavumbini na utarudi mavumbini. Nchi yetu sote hii siyo ya kikundi flani tu chenye mamlaka.