Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana kwa ushauri mkuu.Hii story imenilumbusha miaka hiyo pale tawi la Mazimbu (SUA).
Kuna mtaa nje ya chuo pale unaitwa DARK CITY, Pana migahawa mingi ya vyakula na vyumba vya kupangisha wanafunzi wa chuo.
Sasa tulikuwa tunatoka ndani ya chuo (hostel) tunakuja kula na kurudi chuoni mimi na rafiki yangu.
Siku moja tumeingia mgahawani aisee tumekutana na mtoto mhudumu mzuurii, mweupe wastan, ana unywele wa chotara, kila mwanaume anatoa macho, kumuuliza anasema ndio ana siku nne pale toka atoke kwao kijijini huko mgeta (code).
Tukahudumiwa tukala tukamuaga tukaondoka, ile tumerud kesho kutwa yake binti hayupo, kuuliza tunaambiwa kachumbiwa na mwanafunzi mwenzetu chap. (niliumia mana nilipanga kuonja haha).
Jamaa tunamjua, kumbe kweli kamchukua kamfungia room. Kwake huko nje ya chuo alipopanga na muda mfupi kalipia mahali kaweka mtu ndani mazima mke wa mtu.
Show inaanza mwaka uliofuata wahuni wanavizia jamaa yupo darasani wanamkamua yule dada geto kwa mshikaji.
Mshikaji akaona amwemdeleze sijui kapeleka chuo cha ufundi wa nn vile sikumbuki.
Alitandkiwa mwanamke huko, akapigwa matukio ila jamaa alikuwa mpole anavumilia.
Miaka 8 baadae alishindwa akatema bungo mdomoni wakaachana.
Akaanza upya. Jamaa alikuwa anatembea njiani anaongea peke yake, full mtifuano katika ndoa yake.
Moral of the story = usikurupuke kuoa mwanamke sababu ya
1. Kuwahi wenzio wasimchukue
2. Urembo na uzuri wa usoni
3. Kabla hujasoma kwa kina na kujua tabia yake
4. Kutaka sifa ya kusifiwa mtaani, ukoo, kazini au barabaran umeoa pisi
[emoji848][emoji848]Na honestly wanaume wengi wa miaka hii no 4 ndo inayowaponza mkuu. Yani ilitakiwa iwe point ya kwanza. Mara nyingi humu ukisikiliza vigezo wanavyosifia wanaume weng ni shepu na sura...wenyewe mnasema tabia mtarekebishana lakin ndo inakua inawacost wengi. Soma.kimasihara nyingi kule...weng ni demu pisi, demu mkali, etc Na naamini si kimasihara zote hupita hv, sometimes nyingne huresult katika ndoa...lakin za taabu.
Noted, mkuu.KAMWE usithubutu kumuoa mwanamke kwasababu ya kumuonea huruma
[emoji23][emoji23][emoji23]Yule mke mtarajiwa asiemjua Lowasa ajiandae anaenda kupigwa chini kama masikhara.
[emoji848][emoji848]Mwanamke ni kiumbe mwenye rangi zote, kitu kizito chakuja mkuu jiandae
[emoji28][emoji28]Na yule mke mtarajiwa amfanyaje?
Nimekusoma mkuu.Weka ndani kaka , kufanya kazi bar ni kazi kama kazi zingine, kazi ya bar haina tofauti na kazi zingine kama MAHOTEL kazi za bank n.k.
Kivipi?Utajuta .
Afadhali umenisaidia.Hata hivyo hukuisoma hii story ukaimaliza.
Bar maid waweza sema kuwa nayo ni kazi mtu kaacha, are'u serious?
Umetisha sana mkuu, asante.Sio wote wanaouza bar ni Malaya na sio Malaya wote ni Wauza Bar. Muuza Bar na Muhudumu wa Kempsky awana tofauti.(wote wana kutana na kuonekana na watu wengi wakiwa kazini) umalaya ni hulka ya mtu na sio mazingira au pale ulipomkuta. Nna ndugu na jamaa walio oa Wauza bar na ndoa zipo huu mwaka wa 35. Nna jamaa alio mdada anaejuza Leo hii wapo katika ndoa huu mwaka wa 22. Wapo walioa Mabinti waliosoma shule za Watawa na kulelewa na wazazi wawili walio kwenye ndoa ! Wamewaletea Waume zao HIV kwa umalaya wao uliojificha kwenye historia zao nzuri na upole wao machoni petu[emoji24]. Verify and decide.... uhenda Mungu amekukutanisha na your life partner
[emoji28][emoji28]Kijana anaenda kuingia choo cha kike....Nipo palee
Sawa kabisa mkuu.An
Angalia moyo wakoo mkuu siyo kila muhudum malaya mda mwingine changamoto za maisha kama unauwezo wa kumsaidia kupata angalau kibarua msaidie usiangalie malipo yakee
Softcopy, soma uzi kwa utulivu.Alikuonyesha vyeti alitembea navyo??
Kumnunulia tu bia ukalala nae khaaa!!
[emoji28][emoji28]Hao wanawake wa singida na wakimbulu achana nao hawajawahi kupendeka hao, waongo waongo sana na Malaya kiasili. We piga mrudishe bar usije ukasema hatujakuambia.
HahaaKama yupo sahihi sana, wale wa kwa mwamposa ni mafedhuli kupitiliza.
Kwa hiyo wifi yangu unamuacha kisa umekutana na chuma kipya kikali?[emoji23][emoji23][emoji23]
Duh! mkuu hujasahau tu.
Unamuamini, siku ya kwanza tu kamkabidhi binti kwako kama bidhaa na binti kakubali. Jiulize kabla yako ashakabidhiwa kwa wangapi. Binti anayejielewa hawezi kubali akabidhiwe tu kama mzigo. Tuliza akili acha pupa siku zote huwa anayekuliza ni yule unayemwamini usiyemwamini hawezi kukuliza maana humpi nafasi ya kufanya hivyoHuyo ndg wa huyo binti ni mtu ambaye namuamini sana. Hawezi kunishuhudia uongo. Hana sababu ya kufanya hivyo. Hata Binti mwenyewe, Kwa sisi wenye macho ya rohoni anaonekana ni mkweli kabisa.
Utakuja kujutia usipo tii sauti inayokupa amani juu ya hili! Binafsi nahisi MUNGU amejibu maombi yenu ninyi wawili!Jana nilipita Baa Moja hivi usiku mkali kula, nikakuta ndio Bar inakaribia kufungwa. Ghafla nikasikia malumbano kati ya Meneja wa Baa na kabinti kamoja hivi (waitress). Kumcheki yule waitress sikuamini. Mrefu, ana rangi ya udhurungi, shape ya kwenda, pua ya kisomali halafu nywele mpaka mgongoni! Baada ya malumbano yule binti mhudumu akawa analia.
Malezi niliyopewa na wazazi wangu ni kusababisha tabasamu kwa wengine, ingawa sababu ya ziada ni uzuri wake pia, nikamuita yule waitress, nikamuuliza kulikoni mbona malumbano? Akaniambia, "kaka angu, tangu nianze kazi hapa nina siku ya 9, kila mhudumu wa kike ananichukia wanadhani nitawachukulia mabwana zao, kumbe mimi natafuta maisha".
Nikapatwa na simanzi sana. Nikamwambia basi usilie, agiza kinywaji. Akasema na kazi anaacha. Eeh! Nikashtuka, akamuuliza kaunta anamdai sh ngapi ya vinjwaji, akamlipa hela yote, akaniambia kaka angu kama unataka kuninunulia bia twende ukaninunulie kwengine ila silali na wewe, nikamwambia poa. Kumbe ananipeleka sehemu ambayo atakutana na mwenyeji wake.
Tukahama joint, tukafika kwenye night club Moja hivi, akawa anakunywa bia kwa hasira kama mtu mwenye msongo hadi nikawa namzuia, wakati tuko pale akaja dada mmoja ambaye nilimuacha primary madarasa mawili, anamuita yule waitress dada, nikamuuliza vipi mnafahamiana? Akasema huyu ni mtoto wa marehemu mama mkubwa na mimi ndio nimempokea hapa mjini anaishi kwangu, ana matatizo makubwa, na yeye ndio kanitumia msg yuko hapa ndio nimekuja, yule waitress akafurahi kuona nafahamiana na ndugu yake.
Tamaa zikanijaa, nikamuomba sana niondoke naye kwasababu mimi sio stranger kwake tena kwasababu nafahamiana na ndugu yake, akaanza kumuuliza ndugu yake mara mbilimbili kwamba unamuamini huyu kaka? Ndugu yake akamjibu ndio, namfahamu sana tangu tukiwa Primary. Ikabidi ndugu yake aniapize kwamba sitafanya ufirauni [emoji2]
Tukaondoka, nikam-drop mdg mtu kwake, nikasepa na manzi. Tumefika kwangu aisee story aliyonipa inahuzunisha sana. Aliolewa miaka 2 iliyopita na mwanaume ambaye alikuwa na familia mkoani. Yeye akiwa amaemaliza Shahada yake ya kwanza ya BAF (Bachelor of Accounts and Finance) na kazi nzuri, mwanaume akamshauri aache kazi, kwa mapenzi binti akaacha kazi. Mwaka mmoja baadaye mwanaume akaanza kumnyanyasa, na ndio akagundua kwamba mwamba alikuwa ana mke na watoto 4 mkoa X!!! Kumbe binti ni yatima na alizaliwa kwao peke yake. Anachoshukuru ni hakuzaa na yule mwanaume kwasababu mwanaume hakutaka kuzaa nae kwa wakati ule.
Nikamuuliza kwanini auze bar na taaluma yake? Akasema ilibidi akimbie ule mkoa alipoolewa aje mkoa huu kuficha aibu na kuwasahaulisha watu, na akaona hawezi kukaa tu kwa ndugu yake bila kujishughulisha na chochote wakati anatafuta ajira. Kikubwa zaidi kwenye ile bar aliyoacha kazi hakuna mtu aliyekuwa anajua binti ni msomi, alijishusha afanane nao, nikamuuliza kazi umeacha kweli? akanijibu nimeacha kaka.
Baada ya zile story usiku wa jana nikamwambia haya lala mama. Asubuhi wakati naamka nakuta kavaa pensi na t-shirt yangu vyombo vyote kaosha, nguo chafu kafua, kuna sufuria nilitakaga kuzitupa ila kaziosha zimekuwa nyeupe kama theluji. Nikamuomba anioshe vyeti soft copy, aisee ni kichwa hasa, O na A level ni vijiti tu, Sekondari zote kasoma za kike. Chuo GPA KUBWA!
Mchana nikampa maelekezo asipike nitamuagizia Chakula ikabidi sasa nimtafute yule ndugu yake akaanza ku-verify zile taarifa alizonieleza Binti. Wakuu Mimi sijaoa, il Kuna Binti ambaye nilikuwa namfikiria fikiria kumuoa ila hili ni jaribu kwakweli. Yani huu ni wakati mgumu sana napitia, sielewi kwakweli. Sijamfanya kitu tangu Jana. Sasa hivi ndio nimeingia kwangu na msosi wake namuangalia tu hapa namna alivyotulia kwenye kochi anatazama tamthilia.