Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Jana nilipita Baa Moja hivi usiku mkali kula, nikakuta ndio Bar inakaribia kufungwa. Ghafla nikasikia malumbano kati ya Meneja wa Baa na kabinti kamoja hivi (waitress). Kumcheki yule waitress sikuamini. Mrefu, ana rangi ya udhurungi, shape ya kwenda, pua ya kisomali halafu nywele mpaka mgongoni! Baada ya malumbano yule binti mhudumu akawa analia.

Malezi niliyopewa na wazazi wangu ni kusababisha tabasamu kwa wengine, ingawa sababu ya ziada ni uzuri wake pia, nikamuita yule waitress, nikamuuliza kulikoni mbona malumbano? Akaniambia, "kaka angu, tangu nianze kazi hapa nina siku ya 9, kila mhudumu wa kike ananichukia wanadhani nitawachukulia mabwana zao, kumbe mimi natafuta maisha".

Nikapatwa na simanzi sana. Nikamwambia basi usilie, agiza kinywaji. Akasema na kazi anaacha. Eeh! Nikashtuka, akamuuliza kaunta anamdai sh ngapi ya vinjwaji, akamlipa hela yote, akaniambia kaka angu kama unataka kuninunulia bia twende ukaninunulie kwengine ila silali na wewe, nikamwambia poa. Kumbe ananipeleka sehemu ambayo atakutana na mwenyeji wake.

Tukahama joint, tukafika kwenye night club Moja hivi, akawa anakunywa bia kwa hasira kama mtu mwenye msongo hadi nikawa namzuia, wakati tuko pale akaja dada mmoja ambaye nilimuacha primary madarasa mawili, anamuita yule waitress dada, nikamuuliza vipi mnafahamiana? Akasema huyu ni mtoto wa marehemu mama mkubwa na mimi ndio nimempokea hapa mjini anaishi kwangu, ana matatizo makubwa, na yeye ndio kanitumia msg yuko hapa ndio nimekuja, yule waitress akafurahi kuona nafahamiana na ndugu yake.

Tamaa zikanijaa, nikamuomba sana niondoke naye kwasababu mimi sio stranger kwake tena kwasababu nafahamiana na ndugu yake, akaanza kumuuliza ndugu yake mara mbilimbili kwamba unamuamini huyu kaka? Ndugu yake akamjibu ndio, namfahamu sana tangu tukiwa Primary. Ikabidi ndugu yake aniapize kwamba sitafanya ufirauni [emoji2]

Tukaondoka, nikam-drop mdg mtu kwake, nikasepa na manzi. Tumefika kwangu aisee story aliyonipa inahuzunisha sana. Aliolewa miaka 2 iliyopita na mwanaume ambaye alikuwa na familia mkoani. Yeye akiwa amaemaliza Shahada yake ya kwanza ya BAF (Bachelor of Accounts and Finance) na kazi nzuri, mwanaume akamshauri aache kazi, kwa mapenzi binti akaacha kazi. Mwaka mmoja baadaye mwanaume akaanza kumnyanyasa, na ndio akagundua kwamba mwamba alikuwa ana mke na watoto 4 mkoa X!!! Kumbe binti ni yatima na alizaliwa kwao peke yake. Anachoshukuru ni hakuzaa na yule mwanaume kwasababu mwanaume hakutaka kuzaa nae kwa wakati ule.

Nikamuuliza kwanini auze bar na taaluma yake? Akasema ilibidi akimbie ule mkoa alipoolewa aje mkoa huu kuficha aibu na kuwasahaulisha watu, na akaona hawezi kukaa tu kwa ndugu yake bila kujishughulisha na chochote wakati anatafuta ajira. Kikubwa zaidi kwenye ile bar aliyoacha kazi hakuna mtu aliyekuwa anajua binti ni msomi, alijishusha afanane nao, nikamuuliza kazi umeacha kweli? akanijibu nimeacha kaka.

Baada ya zile story usiku wa jana nikamwambia haya lala mama. Asubuhi wakati naamka nakuta kavaa pensi na t-shirt yangu vyombo vyote kaosha, nguo chafu kafua, kuna sufuria nilitakaga kuzitupa ila kaziosha zimekuwa nyeupe kama theluji. Nikamuomba anioshe vyeti soft copy, aisee ni kichwa hasa, O na A level ni vijiti tu, Sekondari zote kasoma za kike. Chuo GPA KUBWA!

Mchana nikampa maelekezo asipike nitamuagizia Chakula ikabidi sasa nimtafute yule ndugu yake akaanza ku-verify zile taarifa alizonieleza Binti. Wakuu Mimi sijaoa, il Kuna Binti ambaye nilikuwa namfikiria fikiria kumuoa ila hili ni jaribu kwakweli. Yani huu ni wakati mgumu sana napitia, sielewi kwakweli. Sijamfanya kitu tangu Jana. Sasa hivi ndio nimeingia kwangu na msosi wake namuangalia tu hapa namna alivyotulia kwenye kochi anatazama tamthilia.
Ningekuwa mimi ndo wewe kwenye hiyo position na status uliyonayo huyo mwanamke nisigeacha. Hiyo combinations tu ya kuwa ana elimu na alifaulu vizuri darasan halafu kaja ghetto kwako kakufulia nguo na kutosha vyombo vyako kwa ustadi wa hali ya juu, ni adimu kuipata kwa wanawake wengi sana..
She seems to be loyal too kwa mwanaume aliye naye.
Trust me utachukua Miaka mingi na unaweza usimpate kama. Huyo
 
Wewe ni mgeni na wahudumu wa bar.... Utakuja kupigwa na kitu kizito!!! Yaani we umeopoa siku ya kwanza tu unajiona mjanja? Jiulize kabla yako wameopoa wangapi ndugu, na wote mmepewa story hio hio, hata kama maisha magumu kiasi Gani mwanamke anayejua thamani yake hawezi kufanya kazi bar, period!!!
Kwahiyo mkuu hutaki watu tuhudumiwe bar na wanawake.?
 
Ningekuwa mimi ndo wewe kwenye hiyo position na status uliyonayo huyo mwanamke nisigeacha. Hiyo combinations tu ya kuwa ana elimu na alifaulu vizuri darasan halafu kaja ghetto kwako kakufulia nguo na kutosha vyombo vyako kwa ustadi wa hali ya juu, ni adimu kuipata kwa wanawake wengi sana..
She seems to be loyal too kwa mwanaume aliye naye.
Trust me utachukua Mika mingi na unaweza usimpate kama. Huyo
Endeleeni kujichanganya sisi tunaenda kuchekea mbali [emoji81][emoji81][emoji81]
 
Upo sahihi ila angalau upate muda kidogo kumjua mtu. Ukikurupuka majuto huwa makali zaidi.
Bro sijajua umri wako ila nina miaka 19 ya ndoa!!
Story yangu kwenye kuchagua mke pengine ni complex kuliko hii aliyoleta mdau hapa, nilisikiliza tu moyo wangu kwa wakati huo,
Nimekuwa na mahusiano kadhaa kabla na baada ya kuoa ila to honest sojapata anayefanana na mke wangu hata kwa nusu. Na kama ningemkosa kipindi kile basi naamini hadi leo ningekuwa natafuta mke.
 
Wewe ni mgeni na wahudumu wa bar.... Utakuja kupigwa na kitu kizito!!! Yaani we umeopoa siku ya kwanza tu unajiona mjanja? Jiulize kabla yako wameopoa wangapi ndugu, na wote mmepewa story hio hio, hata kama maisha magumu kiasi Gani mwanamke anayejua thamani yake hawezi kufanya kazi bar, period!!!
Mkuu,
Mimi naogopaga Sanaa 😊 wanawake wa bar na sehemu za starehe nawaonaga Kama ma VEMPIRE
 
Sio wote wanaouza bar ni Malaya na sio Malaya wote ni Wauza Bar. Muuza Bar na Muhudumu wa Kempsky awana tofauti.(wote wana kutana na kuonekana na watu wengi wakiwa kazini) umalaya ni hulka ya mtu na sio mazingira au pale ulipomkuta. Nna ndugu na jamaa walio oa Wauza bar na ndoa zipo huu mwaka wa 35. Nna jamaa alio mdada anaejuza Leo hii wapo katika ndoa huu mwaka wa 22. Wapo walioa Mabinti waliosoma shule za Watawa na kulelewa na wazazi wawili walio kwenye ndoa ! Wamewaletea Waume zao HIV kwa umalaya wao uliojificha kwenye historia zao nzuri na upole wao machoni petu😭. Verify and decide.... uhenda Mungu amekukutanisha na your life partner
Mkuu huu ni utetezi kama utetezi mwingine wowote!

Kijana 'fresh' hajaoa, aanze ndoa yake ya kwanza kwa kuoa nungayembe?

Tuchukulie hili swala ni la kwako, mdogo'ako wa tumbo anataka kuoa, waweza mshauri aanze maisha yake ya kwanza ya ndoa na mwanamke aliyeachika?

Emb tuweni serious kwa ushauri bas!
 
Bro sijajua umri wako ila nina miaka 19 ya ndoa!!
Story yangu kwenye kuchagua mke pengine ni complex kuliko hii aliyoleta mdau hapa, nikisikiliza tu moyo wangu kwa wakati huo,
Nimekuwa na mahusiano kadhaa kabla na baada ya kuoa ila to honest sojapata anayefanana na mke wangu hata kwa nusu. Na kama ningemkosa kipindi kile basi naamini hadi leo ningekuwa natafuta mke.

Mimi sio bro ni mwanadada. Nina umri wa kutosha sakafu ya tatu sasa.

Wewe kama ulisikiliza moyo wako na hata hukutaka kujua unaenda kuoa mtu wa aina gani mambo yakatick basi ni jambo la kushukuru Mungu lkn vipi kama mambo yangeenda tofauti? Usingeandika hiyo comment yako . Maana yangu ni kwamba angalau kabla ya kuingia kwenye mahusiano hasa ya ndoa ni better kuchukua time kujuana angalau kidogo. Neno langu sio sheria ila tusikurupuke. ahsante!
 
Back
Top Bottom