Kuna wahubiri siku hizi wanauza maji, chumvi ama mafuta je walipe kodi?

gcmmedia

Member
Joined
Jul 19, 2024
Posts
34
Reaction score
75
Kuna wahubiri siku hizi wanauza maji, chumvi ama mafuta ili kutatua shida za watu (sina uhakika kama vinatatua).

Bei zao ni kubwa sana na wanaingiza pesa ya kutosha. Swali, Je, kuna haja walipe kodi ya mapato kwa mauzo hayo?
 
Ukiweza kuteka akili za watu kupitia Dini unafanikiwa, wazo zuri kuwauzia watu udongo, Maji, Mafuta, Chumvi, Sukari, kupitia Dini.
Utajiri unaupata.
 
Nukuu...JMK ....twajuwa dini ni biashara, fuateni sheria za nchi.....
Baada ya kusikia mapasta fake wakituhumiwa kuuza ngada, madini, pembe za ndovu nk nk!
 
Kijiko cha udongo buku.. Na kuna mtu ananunua hadi vijiko 20.. Nilishuhudia pale Kawe kwa Mwamposa mende la cbm 16 linamwaga kifusi cha udongo.. Sijui siku ile mwamposa aliingiza milion mia ngapi
hapo alipiga pesa za kutosha unauziwa udongo wakati nyumbani kwako kuna udongo? kwa nini asiwaambie kila mmoja aje na udongo wake auombee
 
Ukiweza kuteka akili za watu kupitia Dini unafanikiwa, wazo zuri kuwauzia watu udongo, Maji, Mafuta, Chumvi, Sukari, kupitia Dini.
Utajiri unaupata.
Umesahau na keki za upako
 
Wakilipa kodi kura za kina Tlaatlaah na Lucas Mwashambwa zitatoka wapi?
wajinga ndio waliwao,

yaani uache maji halisi nyumbani kwako ambayo ndio umekunywa, ndiyo umeyaogea, umepikia chakula, umeyaoshea vyombo, umeyafulia nguo zako, halafu eti ujitie kimbelembele eti yale maji unayoyafuata huko kwenye kichupa sijui kwa akina nani ili upate muujiza...

hiyo ni completely useless and nonsense, ni kujidharau kwa kiwango kibaya mno katika upeo wa mwanadamu. Hiyo inamaanisha maji uliyoyatumia nyumbani tangu unazaliwa ni mapepo.

kutoza kodi kwenye eneo hilo ni kuchochea jambo hilo la wizi wa mchana kweupe.
Umoja wa makanisa ya kilokole waketi chini mara moja na kukemeana kuhusu ulaghai huo wa aibu sana 🐒
 
Kuna nabii anauza maandazi ya upako, kuna nabii anauza kikombe cha uji cha upako yani dar utapeli mtupu
 
hapo alipiga pesa za kutosha unauziwa udongo wakati nyumbani kwako kuna udongo? kwa nini asiwaambie kila mmoja aje na udongo wake auombee
mimi nimeshawahi kwenda kwa Mwamposa sio mara moja wala mara mbili, udongo pale hauuzwi, kinauzwa mafuta na maji tu. na huwa anasema ukikutana na mtu akakuuzia udongo toa taarifa, pale yanuzwa mafuta na maji na ni shiling elfu moja tu kwa pc. myonge mnyongeni haki yake mpatie. ndio ni mfanya biashara ila hauzi udongo ni bure.
 
Udongo unauzwa ktk mikutano yake. labda tuseme kuna mataPeli wameingilia biashara ya tapeli mwenzao
 
wajinga ndio waliwao,

yaani uache maji halisi nyumbani kwako ambayo ndio umekunywa, ndiyo umeyaogea, umepikia chakula, umeyaoshea vyombo, umeyafulia nguo zako, halafu eti ujitie kimbelembele eti yale maji unayoyafuata huko kwenye kichupa sijui kwa akina nani ili upate muujiza...

hiyo ni completely useless and nonsense, ni kujidharau kwa kiwango kibaya mno katika upeo wa mwanadamu. Hiyo inamaanisha maji uliyoyatumia nyumbani tangu unazaliwa ni mapepo.

kutoza kodi kwenye eneo hilo ni kuchochea jambo hilo la wizi wa mchana kweupe.
Umoja wa makanisa ya kilokole waketi chini mara moja na kukemeana kuhusu ulaghai huo wa aibu sana 🐒

Mwendelezo huo huo hadi kufikia kwenye kuaminishwa hapa duniani kuna wajomba zake Mungu kuliko wengine.

Yakute Goba huko uyaambie nini kuhusu Isiraeli?
 
Back
Top Bottom