kamtesh
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 1,395
- 513
Kujenga reli, kufufua reli ya Kaskazini, kujenga barabara na mengine yote. Huu ni wajibu wa serekali inayokuwepo madarakani.
Kipi kigeni kufufua Reli ya Dar mpaka Arusha? Ilikuwepo na waliiuwa wenyewe kifisadi. Ubungo exchange, sijui bwawa la la Nyerere, sijui nini? Huo ni wajibu wa serekali na sio fadhila kwa wananchi kwenye maeneo hiyo miradi inakopita.
Tangu Uhuru, kama nikuchelewesha au kusitotekeleza wajibu ni sahihi kuulizwa na kuwawajibisha CCM. Watanzania wenzangu, nchi hii haijawahi kuongozwa na chama tofauti na CCM. Kwa hiyo, wasije mbele ya watanzania kutwambia mmejenga hiki na kile. Tuambie hali ngumu vipi, nyongeza mlizominya vipi, Rushwa, watu kuumizwa na wasiojulikana, kukataza siasa, manunuzi ya vitu bila idhini ya bunge.
Na uchafu mwingine mwingine mwingine mpaka Leo. Swala la Richmond, EPA, IPTL, ESCROW mpaka leo hatujui Richmond alikua nani? Na hiyo kesi imeishia wapi, Escrow imeishia wapi? Hela zilikua za nani? Na waliopata ule mgao wako wapi? EPA ni kizungu mkuti mpaka leo hakieleweki. Mgodi wa Mwadui, Mgodi wa Mchuchuma makaa ya mawe hizi kesi zimeishia wapi?
Mimi hawa hawa CCM kila unapofika muda wa uchaguzi wanawalaghai watanzania na mambo raisi sana ambavyo ni wajibu wa serekali.
Siwezi nikasema nakupigia kura kwa kujenga barabara, ni wajibu wako ndio maana uliomba ridhaa ya kuongoza nchi.
NIWAJIBU WA CHAMA CHOCHOTE KUENDELEZA MAENDELEO YA NCHI, SIO KWA CCM TU. KANU KENYA ILIFANYA MAENDELEO YAKE JAPO KWA KIDUCHU ILA ALIPOKUJA MPINZANI, KENYA IMEENDELEA ZAIDI KULIKO WAKATI WA MOI NA KANU YAKE.
Wapambe na wanaojali matumbo yao na vyeo vyao serekali na ndani ya CCM watapinga sana mabadiliko, sio kwasababu ni mabaya lahasha, ni kwa kulinda matumbo yao. Na ni wachache na kwavile wana dola, watazunguka sana nchi nzima kuwaaminisha watanzania wapumbavu kuwa CCM ni bora kuliko upinzani. Baada ya uchaguzi kupita, ndio wa kwanza kulalamika dhidi ya hali ya maisha ilivyo ngumu.
UNAFIKI NA WANAFIKI NI WENGI MNO. EE MUNGU TUSAIDIE