Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 6,441
- 8,408
Andiko hili ni kwa hisani ya ndugu Vareliano Ulrick Mtundu
"..........mfalme akamwambia Yeremia, nataka kukuuliza neno, nawe USINIFICHE neno lolote. Basi Yeremia akamwambia Sedekia, kama nikikufunulia neno hilo, je! Hutaniua wewe? Tena mimi nikikupa shauri wewe hutanisikiliza." (Yeremia 38:14-15)
Kuna NYAKATI utahitaji KUSIKIA ukweli hata kama UNAUMA.
Mtu mmoja mwenye hekima aliwahi kusema kwamba,"Ukweli ni sura ya kwanza kabisa katika kitabu cha hekima." Na mwingine alisema,"AFADHALI kuumizwa na UKWELI kuliko kufarijiwa na UONGO."
Na
Ulrick Mtundu

Yeremia alipowaambia UKWELI walimchukia, wakampiga, wakamtupa kwenye SHIMO la matope. Wakasema anadhoofisha mikono ya watu wa vita. Lakini baada ya kuona ya kwamba yale aliyoyasema yanatokea kweli mfalme akaona ni bora tu asikie UKWELI kutoka kwa nabii.
Hata kama ni ukweli mchungu wacha nisikie tu. Ukweli ni kwamba UKWELI utabaki kuwa UKWELI hata kama hakuna mtu anayetaka kusikia. Ukweli HAUPIGIWI kura kwamba wengi wape.
Ukweli ni kama mwangwi. Ukiukataa huku unakuitikia kwa nyuma. Hata kama utamwua mkweli, ukweli hauwezi kufa. Hata kama utamtupa mkweli kwenye shimo ukweli utasemwa na mtu mwingine.
Wakati mwingine penda kusikia ukweli unaokuhusu maisha yako hata kama ni mchungu itakusaidia.Hata kama ni ukweli mchungu wacha nisikie tu. Ukweli ni kwamba UKWELI utabaki kuwa UKWELI hata kama hakuna mtu anayetaka kusikia. Ukweli HAUPIGIWI kura kwamba wengi wape.