The Eric
JF-Expert Member
- Feb 23, 2019
- 6,446
- 10,976
Wakuu habari za wakati na poleni kwa majukumu kwa ujumla.
Nina stori naleta kwenu na hichi ni Kisa cha kweli kuwahi kunitokea mimi katika maisha yangu, basi niaze nakusema maisha yana mengi sana wakuu.
Miaka ile ya 2000's nikiwa bado shule nilifika mahali nikawa nimekwama mahitaji ya kujikimu kama daftari, kalamu, kujinunulia msosi kutokana na niliishi na babu tu maana wazazi walishatangulia mbele ya haki na babu hakuwa na uelewa wakunikazania nikaona bora nijichanganye kitaa na kushindwa kuendelea na shule hivyo kuna hali ilinipelekea nikawa na makuzi ya kitaa kama mtoto wa mtaani (hawa wanao itwa chokoraa) miaka hii nilikuwa Arusha japo mimi ni mzaliwa wa mkoa wa Kilimanjaro na shule nilianzia moshi.
Kwanza kabla sijaenda Arusha kuna mwalimu wangu wa shule alinipa mchongo wa kazi huko kenya hapo la saba nilishamaliza ndio niko form one sasa, Mwl. fulani alitokea kunikubali akaona dogo anajipambania afu anafight japo shule kiukweli ilikuwa haipandi kiivo kutokana na mawazo mengi, kula yangu tu ni mpaka nioshe magari siku nyingine lazima niwe mtoro siku 3 au week nifanye vikazi vya saidia fundi na vikazi vya hapa na pale ili niishi.
Ticha alinipa mchongo pale shule ilipofungwa kipindi cha mwezi wa sita ilikuwa na akanielekeza namna nitavyo pokelewa huko Kenya na mwenyeji wangu.
Kuvuka KENYA nilivushwa pori na Rasi mmoja niliyemfahamu kwa sasa ni marehemu aliitwa Rasta P. Apumzike kwa amani Rasi ni broh alikuwa piece kitaani pale, alikuwa kaenda hewani na mbavu anazo alikuwa na piki piki baja XR lile la machalii wa chuga, maana alikuwaga ni apolo yaani wale wachimba ulanga kule mererani wanaotafuta madini ya Tanzanite. so aliwahi kaa mererani sana miaka kadhaa way back to 2000's nakuotea Tanzanite kiaina.
To make story short Tulifanikiwa kuvuka pori na kufika kenya pale mitaa ya chumvini pale yaani ukivuka tu boda ya Tanzania nikakabidhiwa kwa jamaa mmoja pale ni mtanzania ila yupo Kenya.
Kisha Rasi akarudi zake Tanzania.
baada ya maongezi kadhaa tulifikia nyumbani kwa huyo jamaa alikuwa naye ni mchagga tu kama sisi maana rasi naye alikuwa mchagga so tulibonga kinyumbani fresh na jamaa alitoa maelekezo ya kazi pale.
Nitakuja kuendelea kuwajuza zaidi wakuu hii bado stori mbichi kabisa ni kisehemu cha kwanza.
Sehemu ya kwanza.....01. itaendelea