Kuna Watu hawafai jamani: Waliokaa chini wakatengeneza hizi Series nitawaheshimu siku zote

Uliishawahi kuiona movie inaitwa " the story of the perfume of murderer"
 
Mimi kuna series mbili tu za kikoroea nilizowahi kuziangalia mpaka episode ya mwisho.Hizi series ukishamaliza kuangalia episode ya kwanza lazima uwe na arosto utamani kuangalia episode inayofuata ujue kuna nini!!! Ni series nzuri sana mpaka nilikuwa na arosto ya kuangalia episode zote mpaka mwisho.


Kuna hii inaitwa "Queen of ambition"
ndani yake yumo mwanadada Joo Da Hae alikuja kuwa first lady baada ya kutokea kwenye umaskini wa kutupwa.Yumo pia Ha Ryu.
Unapokulia katika umaskini uliokithiri, uzoefu unaweza kukuza azimio thabiti la kufanikiwa kwa gharama yoyote. Joo Da Hae ameazimia kuacha maisha yake ya umaskini nyuma na hataacha chochote hadi apate utajiri na mtindo wa maisha anaotamani. Ha Ryu, ambaye alimpenda Da Hae na angemfanyia chochote, anatumiwa na kusalitiwa naye katika harakati zake za uchoyo. Baadaye anakuwa mwendesha mashtaka wa umma ambaye lazima amwangushe. Lakini Da Hae asiye na moyo, ambaye anaibuka kuwa Mama wa Kwanza(first lady), ana watu wengine wengi ambao watajitolea kwa matakwa yake, ikiwa ni pamoja na Baek Do Hoon aliyepigwa. Je, Da Hae mkatili anaweza kusimamishwa kabla hajaenda mbali sana?

Nyingine inaitwa "King Gwanggaeto,the Great Conquerer" ndani yake yumo Damdeok, jamaa alikuwa na mbinu nyingi sana za kivita, alipigana vita nyingi na kila vita aliyopigana,alishinda.
 
Àisee hii gwangaetto sio poa kabisa. The ghost general of the North
 
Ukimaliza njoo nikuhadithie kuhusu Song of Ice and fire. Ndo utajua kama kuna magenius duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…