utasumbuaje watu wakati una mshahara na una bajeji umeshaipanga mpaka pombe?
Mimi sinywi lakini kipindi nakunywa nikipokea mshahara baada ya kununua mahitaji ya msingi nilikuwa natenga mpaka hela ya bia japo bajeti yake huwa inakuwa na maajabu sana.
Unapanga kwamba hii laki 3 natenga nitakuwa nakunywa taratibu mwezi mzima bila kutoa ofa za bila mpango.
Matokeo yake asubuhi unaamka na 70,000 na ndio inabidi unywe mwezi mzima.
Utajibanabana lakini siku ya pili unajisemea maisha ndio haya haya, unaikamua na 70 yote.