Kuna watu wakarimu dunia hii

Kuna watu wakarimu dunia hii

Nisipo kukaribisha, sitaweza kula kwa amani, roho itanisuta.

Changamoto ni pale unapomkaribisha mdada vitu kama hivyo anakutafsiri vingine au anakuja kukuanzishia uzi hapa kwamba jamaa alimdondokea.

Bora wewe umeona upande wa ukarim.
 
Wiki iliyopita nilisafiri kwenda Tanga, nilipanda basi la Raha Leo. Pembeni yangu alikaa mwanaume amenizidi miaka kama 10 hivi. Nilikuja kugundua baadae ni m-Pakistan na Kiswahil aliongea kidogo sana.
Jirani yangu huyu alikaa siti ya dirishani. Alikuwa amejiandaa kweli kwa safari. Alikuwa na mfuko wa makula kula. Kwenye mfuko alikuwa na meat chops, biscuits, chocolate, juice.

Tulipifika Chalinze nilimuomba aninunulie korosho kwani yeye alikuwa amekaa dirishani, ndipo nilipogundua uwezo wake wa lugha ya Kiswahili.

Alipoanza kutoa vyakula, alinikaribisha meat chops, nilijibu asante, kabla ya kutoka nyumbani nilipiga breakfast ya nguvu na nilijua lunch ya ugali na mchunga inanisubiri kwangu mimi korosho zilitosha.

Baba huyu roho yake ilisononeka sana kwa kukataa kwangu kula chakula. Alinipa chocolate, ilibidi niichukue kumridhisha.

Aliniacha hoi, alipofungua box la juice na kuniambia nianze kunywa mimi kwani anajua akianza yeye mimi sitakunywa. Nilimuomba kuwa mimi ni mzima, nilikuwa na chupa ya maji nikamionyesha huku nikimfahamisha kuwa ninapunguza matumizi ya sukari, kwangu mimi maji ndiyo mpango mzima.

Huu ni Mfano wa gentleman ambao wamebaki wachache sana.
Nahic kama hii habari iko nusu hiv[emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Wengine wanaweza kukuwekea madawa, unakula kitu chake alafu unalala haujitambui hapo atakuibia alafu anashukia njiani, au anajifanya kuomba msaada ashuke njiani mwenzake kazidiwa ampeleke hosptl kumbe ndo umetekwa hivyo. sio vyema sana kumpokea pokea chakula kwa usiyemjua unapokua safarini.
 
Wengine wanaweza kukuwekea madawa, unakula kitu chake alafu unalala haujitambui hapo atakuibia alafu anashukia njiani, au anajifanya kuomba msaada ashuke njiani mwenzake kazidiwa ampeleke hosptl kumbe ndo umetekwa hivyo. sio vyema sana kumpokea pokea chakula kwa usiyemjua unapokua safarini.
🙏🏾
 
Back
Top Bottom