Kuna watu wakatili aisee; nilishuhudia mgeni rasmi akitoa zawadi ya mfuko wa pipi tu

Kuna watu wakatili aisee; nilishuhudia mgeni rasmi akitoa zawadi ya mfuko wa pipi tu

Ni mwaka jana tu katika mahafali ya darasa la saba sehemu fulani niliyoalikwa na mkuu wa shule huyo ambaye ni rafiki yangu mzuri. Tumetulia mara mgeni rasmi kafika na suti yake kuuubwa. Yamefanyika yaliyofanyika hadi muda wa kukaribishwa yeye ukafika. Akaongea vizuri kwa kutoa rai murua kabisa huku hoja zilizoelekezwa kwake kwenye risala akizipotezea kimtindo (niligundua hilo).

Mara ikafika sehemu ya kutoa zawadi yake aliyokuja nayo; akamwita kiongozi wa wanafunzi wa darasa la saba na, kwa mshangao mkubwa, akamkabidhi mfuko wa pipi. Kwenye vyoooote muhimu (madaftari, peni n.k) mheshimiwa huyu ye akaona mfuko wa pipi ndo zawadi bora kwenye tukio hili....dah!!!

Aisee kuna watu wakatili sana, sikia tu.
Hahaha jamaa anajiaminii darasa la saba si mtu wa kumpa pipi
 
Safi Sana

Vi graduation vya darsa la Saba havina ishu kbsa
 
Maneno murua aliotoa ni tosha kabisa kuwapa vijana motisha ya awamu inayofata katika elimu.
Mgeni rasmi sio lazima na hapaswi kuja na zawadi yeyote. Zawadi ni kazi ya waandalizi.
 
Back
Top Bottom