Kuna watu wamerogwa vibaya sana na hawajijui kuwa wamerogwa.

Kuna watu wamerogwa vibaya sana na hawajijui kuwa wamerogwa.

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!
Mtu akirogwa anajijua kabisa lakini akirogwa vibaya sana hawezi kujijua. Anabaki tu kama kipepeo hajui afanye nini kutwa kutwa.
Hawezi kuwa na mipango thabiti, leo atapanga hili, kesho atapanga lile , keshokutwa atapanga jingine.
Mtu huyu hawezi kufanikiwa kwenye jambo lolote.
Kuna watu wengi ukiwaona tu unasema huyu karogwa vibaya.
Mfano:
1. Binti mmoja anafanya kazi kwenye mgahawa wa mtu malipo ni sh. 5000 kwa siku huku akipata mlo mmoja tu wa asubuhi bure, yaani chai tu mchana anashinda njaa. Yakibaki makombo ndio haki yake pamoja na wafanyakazi wenzake.
Nilimwambia kwakuwa una experience ya miaka zaidi ya 3 kwenye shughuli hii unaonaje Mimi nitoe mtaji tufanye mgahawa mzuri halafu faida Mimi taichukua 50% na wewe 50% kila siku.
Mgahawa mzuri faida kwa siku sio chini ya sh.50000 . Binti mpaka leo hanipi jibu. Anatumikishwa tu.
Huyu karogwa vibaya.
2.Kuna mdogo wangu mmoja wa faza mmoja nilimwambia nipe laki 3 au 2 tu Mimi nikuongezee kiasi kitakachobaki upate kiwanja hapa Dar , nikamwambia kwakuwa wewe ni boda nitumie sh. Elfu 5 kwa siku 40 jumla itakuwa laki 2 Mimi nitalipia kiwanja hata cha milioni 1 au mbili. Huu mwezi wa 8 kimya. Hanikumbushii wala kuonyesha Nia ya uhitaji na amepanga chumba kimoja na watoto anao 3.
3. Kuna kijiana anafanya internship ya ufundi magari zaidi ya miaka 6 sasa , nikamwambia nifungue biashara ya garage kwakuwa Mimi sina utaalamu wa mambo ya ufundi. Simamia utapata pesa kuliko kujitolea muda mwingi bila malipo maalumu. Kijana ananikwepa .
Kuna watu hawasaidiki, wamerogwa vibaya sana.
Wanahitaji maombi makubwa.
 
Uoga tu mazee waliologwa huwa wapo wapo tu , watu ni waoga kuanzisha maisha mapya wengine uakuta ndo mpaka wafukuzwe iyo kazi yani shida ni kwamba wanakuwa na majibu negative ya kitu na wanayaamin wape mindset
 
Back
Top Bottom