Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari za Sabato!
Kuna watu wanaamini kuwa watu wote wa CCM ni Najisi, wezi, majambazi, mafisadi yaani kitendo cha kuwa CCM wanaamini wewe ni muovu. Jambo ambalo sio kweli
Wakati huohuo wanaamini kuwa chama cha upinzani kama CHADEMA ndio kuwa Mtakatifu au mzalendo wa taifa. Jambo ambalo sio kweli.
Majizi, waovu, na madikteta wapo vyama vyote. Ubaya hauna chama kama vile ubaya hauna kwao.
Watu wema wanaweza kuwa chama chochote tuu. Wapo CHADEMA wema, na wapo CCM wema.
Wapo CHADEMA wabaya na wapo CCM wabaya.
Wapo wanaccm wanaamini kuwa mpinzani au kuwa CHADEMA ni kuwa muasi, mhaini, pingapinga na Muda wowote unaweza kuangusha serikali. Jambo ambalo sio sahihi.
Kumbe unaweza kuwa CCM na ukawa Muasi, mhaini, na pingapinga na Muda wowote unaweza kuiangusha serikali.
Hoja ni nini?
Kila chama kinaowajibu wa kutambua watu wema waliopo ndani ya chama hiko ili waongoze kwa sababu wema wakiongoza taifa limepata kuanzia CCM wenyewe na upinzani.
Halikadhalika na upinzani, wawape watu wema uongozi ili hata CCM nayo inufaike na watu hao.
Mwema ni mwema hata awe CHADEMA au CCM. Awe muafrika au Mzungu.
Na mbaya ni mbaya hata awe CHADEMA au CCM. Awe muafrika au mzungu.
Nawatakia IBADA Njema ya Sabato.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa, Manzese Kanisani, Dar es salaam