Kuna watu wanabeza Rais kusikiliza maneno ya mitandaoni, kwani watu wa mitandaoni sio Watanzania au hawapaswi kusikilizwa?

Upo sahii Sana mkuu,ni WATU wa maajabu wanaofikili mtanaoni wapo WATU wajinga na wasiojielewa ,bila fikra kwamba why mtu anaweza kua on line 24 hrs, je kifurushi anatoa wapi ,familia yake inakula wapi au yeye mwenyewe, majukwaa ya mtandaoni yana WATU makini,kuanzia kifikra,elemu na uwezo wa kupambanua Mambo hata kuliko wabunge,na mawaziri pia sema tu wapo hawajulikani au Wengine wanajulikana and by the way hawana haja na vyeo ,ila nasema ndo wazalendo wa kweli kuliko wale wanaojipendekeza
Ukiona mtu anawachukia jua ni jambazi lililokubuhu halitaki lijulikane ili kuendelea na unyanganyi kwa kutumia neno maskin,THNKS JF MEMBER
 
Mama ajisikie amani so far anatenda haki , binafsi Kama mwanachama wa chadema ambae sikuwahi jiunga na chama chochote Cha Siasa na niliojiunga na chadema as new member Kipindi Cha mwendazake ,naapa kwamba
NITAMTETEA MAMA AKIFANYA VIZURI, NITAMPINGA PALE SIONI TIJA, NITASEMA HAFAI PALE NAONA ANAENDA KINYUME,
MUNGU MSAIDIE MAMA, SAIDIA TANZANIA, SAIDIA NA KUIBARIKI CHADEMA,CHADEMA MUNGU INAKUITAJI SANA KAMA AMBAVYO UMEKUA NAYO MWANZO MPAKA MWISHO - IMEKUA
 
I concur with you 100%.Sina cha kuongeza,you have said it all..
 
Kwanza inamrahisishia kazi Rais.

Na wala siyo kwamba Rais mwenyewe atashinda mitandaoni akitafuta majungu na upotoshaji na kuchuja mazuri na yaliyo ya ukweli.

Rais akitaka kuitumia kwa manufaa memngi mitandao ni kuwa na vijana walioiva vizuri katika utumiaji wa mitandao, wenye uelewa mpana.

Hawa wana uwezo wa kuchambua upuuzi na mambo ya msingi ambayo watayawasilisha kwake na washauri wake wa karibu.

Kama jambo ni zito, linaloonekana tokea kwenye mitandao, kwani ni lazima Rais alirukie mara moja bila ya kulitafutia ukweli na kuupima kabla ya kulitolea uamizi?

Sasa hapo tatizo litatoka wapi, kiasi cha kwamba aogope kutumia mitandao?

Wasiojua kuitumia mitandao, na wenye akili iliyofungwa pekee ndio wasiopenda mitandao.
 
Ni wapuuzi tu hao wako zama za ujima

Nchi nyingi zimechafuka na kukosa amani kwa hamasa ya mitandaoni afu pimbi mmja anasemaje?

Tena Rais awatafute kwa kutumia vyombo vya usalama awafunze adabu
 
Kwa hiyo maoni ya watu sahihi yanapatikana wapi? Halafu unataka afanye maamuzi yapi ili asionekana anafanya maamuzi bila mhemuko?
 
Mkuu achana nao hao ni lile genge la legacy, acha wafu wazikane. OVER!!
 
Hao wanaosema mama asiingie mitandaoni ndiyo hao hao wanaotumia mitandao hiyo kumpiga mikwara, naiita mikwara mbuzi!

Watu wa ajabu sana hawa...

Yaani wao waitumie, yeye asiitumie, ili iweje, ili iweje...
 
Kiongozi anayethubutu kupita humu mitandaoni akaona anavyosifiwa na kukosolewa,anavyotukanwa,anavyokashifiwa,anavyoshauriwa,huyo sio dhaifu bali ni imara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…