4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 8,406
- 9,619
Upo sahii Sana mkuu,ni WATU wa maajabu wanaofikili mtanaoni wapo WATU wajinga na wasiojielewa ,bila fikra kwamba why mtu anaweza kua on line 24 hrs, je kifurushi anatoa wapi ,familia yake inakula wapi au yeye mwenyewe, majukwaa ya mtandaoni yana WATU makini,kuanzia kifikra,elemu na uwezo wa kupambanua Mambo hata kuliko wabunge,na mawaziri pia sema tu wapo hawajulikani au Wengine wanajulikana and by the way hawana haja na vyeo ,ila nasema ndo wazalendo wa kweli kuliko wale wanaojipendekezaKuna watu wana hoja mfu sana. Wanabeza Rais kusikiliza maneno ya mtandaoni. Kwani watu walioko mitandaoni sio watanzania au hawapaswi kusikilizwa? Watu wa mitandaoni ndio hawa hawa watu wa mitaani. Au wanadhani watu wa mitandaoni wanatoka sayari nyigine?
Mitandao ni platform sahihi kabisa ya watu wa kawaida kutolea maoni yao, na Rais kama kiongozi wao yupo sahihi kabisa kuyafanyia kazi maoni ya kwenye mitandao maana yametolewa na raia wake ambao hawana uwezo wa kumfuata ikulu na kuongea naye ana kwa ana.
Raia wa kawaida hawana uwezo wa kuonana na Rais kwa urahisi hivyo mitandao ni sehemu pekee ya kuwasilisha malalamiko yao. Na nadhani Rais wetu analitambua hilo ndio maana amekuwa akisisika akiongelea anachokisoma mitandaoni.
Hao wote wanaobeza Rais kusikiliza maneno ya mtandaoni nadhani wana matatizo yao binafsi au kuna maslahi yao yanaguswa. Wanataka Rais asisikilize maneno ya mitandaoni halafu asikilize maneno ya wapi ilihali hata wabunge wetu hawatusemei huko bungeni kazi kujipendekeza na kusifiasifia tu kusikokuwa na faida yoyote kwa raia wa kawaida.
Mama Samia njia uliyoichukua ya kusikiliza maneno ya mitandaoni ni sahihi kuliko maelezo yenyewe maana hawa watu wa mitandaoni ndio raia wanaokutegemea uwatumikie kupitia dhamana uliyo nayo na mitandao ndio njia yao pekee ya kukufikishia ujumbe wao maana hawana uwezo wa kukufuata ikulu.
Kazi iendelee.
Ukiona mtu anawachukia jua ni jambazi lililokubuhu halitaki lijulikane ili kuendelea na unyanganyi kwa kutumia neno maskin,THNKS JF MEMBER