Kuna watu wanafanikiwa zaidi baada ya kuacha kuwaambia watu mipango yao ni coincidence au kuna ukweli?

Kuna watu wanafanikiwa zaidi baada ya kuacha kuwaambia watu mipango yao ni coincidence au kuna ukweli?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Nimekua nikifikiria jambo hili kwa muda.

Kuna watu ambao zamani walikuwa wanawaambia watu kila kitu wanachopanga kufanya kama biashara, ujenzi, kazi wanayoomba, miradi wanayoandaa na hata mipango ya maisha. Lakini baada ya muda wanaamua kukaa kimya, wanaacha kuelezea kila hatua ya wanayopitia na wanaanza kufanya mambo yao kimya kimya.

Cha kushangaza, baadhi yao wanaonekana kuanza kupata progress kubwa zaidi.

Sasa swali ni: Je, ni coincidence tu, au kuna nguvu fulani kwenye kutotangazia kila mtu mipango yako?

Wengine wanaamini kwamba unaposema mipango yako unaweza kupata opinions nyingi (hasi), pressure, discouragement, watu ambao bila kukusudia wanakyfanya uanze kuwa na doubts. Mbali zaidi, kwa watu wenye imani wanaamini inaweza kuleta husda na kusababisha mipango yako kutokamilika.

Na kwa upande mwengine, kuna point kwamba; wapo watu ambao wamefanikiwa kwasababu walipewa ushauri na mawazo tofauti tofauti kwa waliotangulia kufanikiwa, connections support na opportunities kwa kupitia kushirikisha watu kuhusu mipango yao au wanachofanya kwa wakati huo.

Kwahiyo, je, ni bora kufanya mambo yako kimya mpaka yaonekane, au ni muhimu kuwaambia watu ili upate support na opportunities?

Je, wewe umewahi ku-experience upande gani?
 
Usiwaambie watu mipango yako, hata ndugu zako wa karibu.

Tunaishi kwenye ulimwengu uliojaa wivu, husda, chuki na tamaa.

Kuwaambia hawa mipango yako wataanza kukufikiria kwa vinyongo hata kama usoni watakuchekea, vinyongo ambavyo vinaweza kugeuka vikwazo kwako kwenye kutikiza malengo yako.
 
Imani Imani Imani

Mimi nimeamua kupinga hicho kitu nimejikita kwenye Imani yangu kama Mungu amepanga kitokee basi kinatokea

Imani yangu inafanya kazi Sinaga mambo ya kufikiria negative mda wote
Imani and positivity.
 
Back
Top Bottom