Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Natumaini mu wazima. Binafsi namshukuru Mungu sijambo.
Japo Kuna baadhi ya watu wachache wanaweza kukuharibia siku kwa matendo au hata maneno yao.
Wanakera sana. Utakuta mtu anakulazimisha kukusalimia kwa kukushika mkono wakati amekotoka magali pa 'faragha' ama alikuwa akishika sehemu fulani fulani hivi za mwili wake na hajanawa popote!
Mwingine anakukuta mahali umekaa kwa kutulia anakupulizia hewa ya mdomoni mwake! Sipendi!
Au analazimisha kukukumbatia, ukikataa anakuvuta kwa nguvu.
Kwenye upande wa maneno kuna wale wanaopenda kukuuliza mipango yako kila mara au kama hujaoa/kuolewa basi kila siku lazima wakuzungumzie wewe! Wanatumia muda mwingi kutathimini maisha yako badala ya kutathmini ya kwao! Wananiudhi!
Kumbuka: hao ni watu wazima na familia zao!