Kuna watu wanakula utadhani wanahamisha upande wa pili.

Habari.
Juzi nilikuwa kwenye harusi ya ndugu. Wakati wa kupata chakula kuna jamaa alikuwa anakula hatarii alikula sahani saba hadi kamati ya chakula wakakataa kumpa chakula kingine alikuwa bado anadai. Nini kinasababisha mtu kula sana wataalam??
Behemoth spirit
 
Ukute hizo sahani saba alikuwa ana onja tu, kula alikuwa bado hajaanza. 🤣🤣
 
sahani 7 itategemea zina ujazo gani sio mnapimia watu ujazo wa kikombe kimoja cha chai na wakisema hawajashiba mnawaona walafi.! na hii inachangiwa na tabia ya wenye sherehe kuwachangisha watu pesa ndefu utasikia single 50,000 alafu akifika kwenye hiyo sherehe mnataka alambelambe tu sio kushiba wakati 50 yake inamuuma lazima afukie kisawa sawa
Mkuu hata sahani za visosi vya chai, 7 huwezi vimaliza kwa mlo wa kawaida.

Wali wenyewe siyo mkavu ni pamoja na kujaziwa zaga zingine zikiwemo vitoweo na matunda.

Hilo ni tatizo, kuna mdau comment #6 kadadavua vizuri sana.
 
Habari.
Juzi nilikuwa kwenye harusi ya ndugu. Wakati wa kupata chakula kuna jamaa alikuwa anakula hatarii alikula sahani saba hadi kamati ya chakula wakakataa kumpa chakula kingine alikuwa bado anadai. Nini kinasababisha mtu kula sana wataalam??
Tulikuwa naye 'power Mwamgiga', anakula ndoo ya wali ya lt10, galoni la maziwa, mkungu wa ndizi na creti la soda ndiyo anashiba.

Soda anafungulia ukucha.

Akitaka kubeba maji, ni pipa mbili zinajazwa halafu mzega wa kubebea ni mwamba wa nguzo za simu za Ttcl, mwanaume anaondoka nazo.

Gari mbili anazizuia kwa mkono mkavu.

Chai yake ni chai ya maziwa birika zima na mkate unakatwa kati kati kwa mkono unafinywa na kusokomezwa mdomoni, hataki silesi!

Mngekutana na mtu wa hivyo, mgelimwandika sana kwa kulalamika na kujaza server.
 
Habari.
Juzi nilikuwa kwenye harusi ya ndugu. Wakati wa kupata chakula kuna jamaa alikuwa anakula hatarii alikula sahani saba hadi kamati ya chakula wakakataa kumpa chakula kingine alikuwa bado anadai. Nini kinasababisha mtu kula sana wataalam??
Nafikiri anafidia mchango wake wa harusi...
 
Kula ni haki yake kwa sababu hakukuwa na bango au kipeperushi ambacho kina sema mwisho kula ni sahani moja
 
Katika harakati za kutafuta maisha nilikuwa mwenye najipikia
unga wa dona nusu kilo na nyongeza mboga mbaazi nusu ya robo bila kusahau kuna visamaki flani vinaitwa nguruka vya kurumangia pembeni
hiyo ngoma Moro.
Kazi ngumuuu
asee nilikata body na hapo kumbuka unakula asbh na usiku tu.
 
Tulikuwa naye 'power Mwamgiga', anakula ndoo ya wali ya lt10, galoni la maziwa, mkungu wa ndizi na creti la soda ndiyo anashiba.

Soda anafungulia ukucha.

Akitaka kubeba maji, ni pipa mbili zinajazwa halafu mzega wa kubebea ni mwamba wa nguzo za simu za Ttcl, mwanaume anaondoka nazo.

Gari mbili anazizuia kwa mkono mkavu.

Chai yake ni chai ya maziwa birika zima na mkate unakatwa kati kati kwa mkono unafinywa na kusokomezwa mdomoni, hataki silesi!

Mgekutana na mtu wa hivyo, mgelimwandika kwa kulalamika na kujaza server.
Hapa umetupiga
 
Katika harakati za kutafuta maisha nilikuwa mwenye najipikia
unga wa dona nusu kilo na nyongeza mboga mbaazi nusu ya robo bila kusahau kuna visamaki flani vinaitwa nguruka vya kurumangia pembeni
hiyo ngoma Moro.
Kazi ngumuuu
asee nilikata body na hapo kumbuka unakula asbh na usiku tu.
Siku hizi umepunguza?
 
Habari.
Juzi nilikuwa kwenye harusi ya ndugu. Wakati wa kupata chakula kuna jamaa alikuwa anakula hatarii alikula sahani saba hadi kamati ya chakula wakakataa kumpa chakula kingine alikuwa bado anadai. Nini kinasababisha mtu kula sana wataalam??
Acha uongo, nilikula sahani nne...ya tano nilikula nusu tu...na ile ya sita nilienda kula kwenye gari wakati wa kuondoka ya saba nilienda kulia nyumbani

Umekuja kunisema huku ili iweje?
 
Ulimaliza chakula waliokuja mwishoni walikosa
 
Back
Top Bottom