Kodi ya watu wa Soka pia ni kubwa wanakatwa 35 mpaka 45% ya kipato chao wasichokitumia. Na kila hela wanayolipwa haimaaanishi ni Thamani yao wanalipa mishahara, wanatumia na wao kama binadamu wengine, wanalipa kodi ya Nyumba etc. There is a reason hakuna Mwanasoka Bilionea so far.
Kuhusu MO mkuu Hebu twende Taratibu.
-MO ni exporter mkubwa wa mitiki, quality ndogo ya mitiki cubic meter ni $900 quality kubwa mpaka $1500 kontena la futi 20 ni Cubic meter 33, so tunaongelea milioni 60 mpaka 120 hivi kwa Container. Jamaa ana Yard nzima, kuna kipindi kila wiki zinaingia gari kama 10 toka mashambani huko Tanga ama Morogoro, so easily tunaongelea Mamia ya macontainer na Revenue makumi ya Bilioni.
-kwenye Katani jamaa ana Heka 40,000 na production yale ni Tani 10,000 kwa mwaka, bei ya Tani sasa hivi ni $850 mpaka $900 hivyo tunaongelea Dola milioni 8 ama 9 hivi ambayo ni zaidi ya bilioni 20.
-Njoo Pamba hapa napo tunaongelea Tani 30,000 mpaka 45,000 ambayo roughly ni hizo Bilioni 30 mpaka 45 haijakuja processed hapo, kiwanda cha nguo cha MO kina capacity ya kutengeneza Mita milioni 100 kwa mwaka, mita moja ya Fabric inategemea ya nini at minimum sokoni ni 1000 ila inaenda mpaka 8000 hivyo tunaongelea market ya mamia ya Bilioni.
Nikupe tu comparison moja hapa, Tanzania Nzima ina heka milioni 86, Metl mashamba wanayohudumia kwenye Pamba tu heka milioni 5.
-kwenye Mawese/crude oil jamaa anaingiza Tani 120,000 kwa mwaka bei ya Tani ni Around $600 hivyo anaspend around $72m kwenye hili, hii ni raw Material tu ya kiwanda ni around bilioni 200 bado haijatoka Final product ambayo ina Thamani zaidi.
Hivi Vyote mkuu, nimebase Kwenye kitu kimoja tu Agriculture, na sijamaliza mazao yote, kuna Korosho hapo, mbaazi, dengu na mengine mengi hata Sina ya Angalia ila tayari tunavuka Bilioni 500 tayari. Bado kuna viwanda na biashara etc. Na hio ni Tanzania tu jamaa yupo Nchi 12.
Naona uvivu kuweka source ya kila kitu, ukihitaji source ya data yoyote unayoitilia mashaka niambie nitakuekea.