Kuna watu wanamshindanisha Diamond Platnumz na Cristiano Ronaldo

Source ya huo utajiri ni majini au unatoka METL? Sijui kwanini mmekaria nadharia Bakhressa ni tajiri kuliko kila mfanyabiashara huku Tz.. Akina Marehemu Subhash Patel alikuwa tajiri kuliko hata hao akina Mo na Bakhressa.

After all Bakhressa unayemsifia kuna shares kama zote za Mzee Mwinyi huko ndani..
 
Mo anapenda kujibrand kama billionea ili apate mikopo kirahisi benki za nje kunamtu aliuliza kuhusu magu atakua amepata jibu lake hapo.
Mo hawezi sema METL imetoka kwenye turnover ya $30m mpaka $1.5b alafu eti mahesabu ya METL kodi iwe pungufu ya hao waarabu walioshikilia hela za Mwinyi..

Nenda Department ya Large Taxes pale TRA HQ ukaupate ukweli wa nani ni tajiri kati ya METL na SSB..
 
Acha kutuone wapuuzi kama vile siye hatuwajui wwafanyabiashara mji huu.

Skia wewe huyo subash patel alikua ni mdogo wa jeetu pate, enzi za mwinyi na mkapa jeetu patel alikua na hela kuliko kina bakhresa kabla bakhresa hajapanda mpaka kuwafunika.
Baada ya skendo la kupiga pesa za EPA za bot, jeetu ilibidi a step aside amkabidhi biashara zake subash ambaye alikua anamiliki Sea Cliff hotel. Kwaiyo hayo ma kiboko paint/pipe et all, sayona, kunduchi beach, ni pesa zimekuwa channeled through Azania group. Magari ya Eicher haya, ma apartments pale posta CBD yote ile pesa ya jeetu patel kapiga enzi za mwinyi na mkapa.
Ila kwa sasa hao wametulizwa na mtu pekee anaye make big moves ni bakhresa. Hata gsm spidi imepungua baada ya msoga kutoka mjengoni.
 
Unapopimwa Utajiri yote hayo huzingatiwa.

MO amechukua Mkopo billioni 300 toka bank ya South Africa, nani atakupa Mkopo wote Huo bila kuwa na Asset ama pato la ku backup ombi lako la mkopo?

JAMAA ana contribute 2.5% ya GDP ya Tanzania, hilo pekee linahitimisha hii debate, ameajiri watu takriban 24,000 assume wanapata average mshahara laki 4 hio zaidi ya billioni 100 mshahara tu kwa mwaka. Kila data unayoiangalia inakuja mule mule kwamba yeye ni Bilionea.

Na mkuu mimi ni mkaazi wa Tanga kabla ya MO kuchukua mashamba Tanga nakumbuka viongozi wa serikali walikuwa wakipita Nyumba hadi Nyumba unapewa shamba Bure la mkonge, hakuna mtu aliyekuwa interested, mo akakomba Ardhi yote a kaanza kulima yeye, sasa hivi kelele ni nyingi sababu katani imepanda bei soko la Dunia, ila ikishuka Tena yanatekelezwa tena Mashamba yote..

Na mkuu Tajiri ni Tajiri Nchi za ulaya Matajiri wanapewa mpaka Ruzuku as long as anachofanya kina Faida kwa Taifa, hata Leo serikali ya Tanzania isipowapa mashamba na Viwanda vya zamani Basi nchi nyengine zitawapa.

Leo hii serikali isingetoa viwanda vya zamani tusingekuwa tunatengeneza Mashuka, Kanga, vitenge, jeans na mambo mbalimbali wenyewe. Sababu ya juhudi zilizofanyika kwenye Pamba Tunaona Viwanda vingi vimefufuka, even Levi's kampuni kubwa Kabisa Duniani ya Jean's ina Kiwanda Tanzania, Nchi zinazotuzunguka Nyingi tuna Supply bidhaa za Pamba kwao.
 
mnalinganisha Diamond na Ronaldo???really??
Diamond alinganishwe na Zari , Ronaldo mbona maji marefu sana hayo😀😀😀😀😀😀
 
Hata tapeli anaweza kuwa billionaire kama mali na fedha zake zanafika hesabu hizo, ni kweli MO ni mtoto wa Azim Dweji lakini Azim alishajitoa kitambo katika biashara na kuzikabidhi kwa mwanae. Unajua hata before MO came into the picture Azim was among the top three richest business moguls in TZ? I remember back then tajiri namba moja alikuwa ni Rostam Aziz wakifuata Bakhresa na Azim na kwa mbali namba nne akiwa Mengi na namba tano Ali Mufuruki baada ya kuhamishia biashara zake zote kutoka Kenya kuja Tanzania. Ila top three hawakuwa wameachana mbali kwa thamani za utajiri wao.
 
Siyo Mwinyi peke yake, kumbuka akiwa kapuku hata Salim Ahmed Salim aliwekeza sana. Bakhresa hayuko peke yake lakini hilo si tatizo kwani wafanyabiashara wengi hutumia mfumo huo, there are always powerful personalities behind the scene ambao wao kazi walishamaliza kwa kuwekeza hivyo wakula faida tu.
 
Sasa kwa huo mtazamo wako tajiri mwenye mali ni Azim ay mo
 
Mkuu mimi wala sipingani na wewe walichokosna na mwendazake ni anapewa assets yeye hakuziendeleza walipo taka kunyanganya wakakuta hati zake zote zipo ulaya na sio hapo South na mbaya hakuna muendelezo na mkwanja mrefu kachukua mimi huko kwenye nani number moja sipo mie sipo maana hiyo proprietorship firms mwisho familia yake ndio inafaidika ila ukweli metl imewekeza sehemu kubwa huo ushindani wa nani tajir kumzidi mwenzie mie sijui
 
Sasa kwa huo mtazamo wako tajiri mwenye mali ni Azim ay mo
Kwa hilo wanaojua ni wao, wenyewe wanadai baba kila kitu kakabidhi kwa mwanae. Sisi ni outsiders hivyo wanaweza kutueleza chochote kadri wanavyojisikia.
 
Azim dewji si baba yake MO sidhani hata kama ni ndugu. Baba yake MO anaitwa Gulam.
 
Na bado ananunua cement na kusupply
 
Azim dewji si baba yake MO sidhani hata kama ni ndugu. Baba yake MO anaitwa Gulam.
Hahahahah oyaa acheni kutoa info za uzushi, kwani wakati Mo ametekwa nyie mlikua nchi gani wakati Azim dewji anaitisha press na kutangaza kiasi cha billioni moja kwa atakayetoa info za kupatikana kwa "mtoto wetu", .tena Azim ndiyo alikua msemaji kama mkuu wa ukoo na gulam babaake mo alikua pembeni mnasema hawana undugu .
Kaeni mkijua kwamba hela za billionea mo asilimia kubwa ni za Tajiri namba moja enzi za mwinyi wakati akiwa mfadhili wa simba mzee Azim, mo pale hana hata $100m ndo mana 20b za simba kidogo zimtoe roho.
 
Point of correction, MO ni mtoto wa Gulamabbas Dewji. View attachment 1881424
Hahahahah oyaa acheni kutoa info za uzushi, kwani wakati Mo ametekwa nyie mlikua nchi gani wakati Azim dewji anaitisha press na kutangaza kiasi cha billioni moja kwa atakayetoa info za kupatikana kwa "mtoto wetu", .tena Azim ndiyo alikua msemaji kama mkuu wa ukoo na gulam babaake mo alikua pembeni mnasema hawana undugu .
Kaeni mkijua kwamba hela za billionea mo asilimia kubwa ni za Tajiri namba moja enzi za mwinyi wakati akiwa mfadhili wa simba mzee Azim, mo pale hana hata $100m ndo mana 20b za simba kidogo zimtoe roho
 
Kuna uzi hapa pitia wanazungumziwa

Azim, Kasim na Dewji wengine ni jina tu kama una Sema Lyimo ama Tarimo.

Haimaaanishi watu wote wenye ubini wa kimaro ni ndugu.
 
Check correctly, si mimi niliyesema hawana undugu ila hapa nime-Google kumjua biological father wake. That's all.
Suala la kuwa nchi gani si issue kwani kila information unaweza kuipata popote ulipo.
View attachment 1881621
 
Mtabishana mtachoka mwisho wa siku tajiri ndo anayejua utajiri wake Kama wa kwakwe au wa ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…