Kuna Watumishi wasiyo na sifa wanakaimu nafasi ya Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri kwa muda mrefu wakati wenye sifa wapo

Kikwava

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2015
Posts
1,741
Reaction score
1,068
Hili siyo jungu ni uhalisia kabisa, huko kwenye Halmashauri zetu ili uwe mkuu wa idara shart moja wapo inatakiwa uwe na Master degree,

Sasa imetokea kuna halmashauri watu wasio na sifa wanakaimu kwa muda mrefu wakati wenye sifa za kushika hizo nafasi wapo labda wangeweza kupatikana kupitia ajira portal au taratibu zingine za uteuzi.

Tunaiomba serikali yetu kuliona hili swala kimapana zaidi ili kuongeza uwajibikaji kwa hawa Watumishi wetu.

Mungu ibariki Tanzania Mungu mubariki Rais wetu 🇹🇿
 
Sasa imetokea Kuna halmashauri watu wasio na sifa wanakaimu kwa muda mrefu wakati wenye sifa za kushika hizo nafasi wapo labda wangeweza kupatikana kupitia ajira portal au taratibu zingine za uteuzi.

Tunaiomba serikali yetu kuliona hili swala kimapana zaidi ili kuongeza uwajibikaji kwa hawa Watumishi wetu.

Mungu ibariki Tanzania Mungu mubariki Rais wetu 🇹🇿
Kwako wewe sifa ni zipi? Au uchu na tamaa ya madaraka ndio vinakusumbua
 
Kuna udhaifu kwakuwa nafasi hizo hazitangazwi watu wenye sifa waombe na kisha washindane.

Hata kama zitatangazwa kwa watumishi wa umma peke yake.

Matokeo yake vitengo wanapewa wale wanaoweza kula vizuri na mkurugenzi na wakubwa wengine. Kama hawana sifa basi watakaimu hapo miaka nenda rudi.
 
Hizi nafasi Bora ziwe zinatangazwa kwenye ajira portal, hakuna halmashauri ingekuwa na mtu anayekaimu,
Ili uwe mkuu wa idara uwe senior kwenye utumishi wa umma na uwe na Masters hawa watu wapo
 
Hili siyo jungu ni uhalisia kabisa, huko kwenye Halmashauri zetu ili uwe mkuu wa idara shart moja wapo inatakiwa uwe na Master degree,

Sasa imetokea kuna halmashauri watu wasio na sifa wanakaimu kwa muda mrefu wakati wenye sifa za kushika hizo nafasi wapo labda wangeweza kupatikana kupitia ajira portal au taratibu zingine za uteuzi.

Tunaiomba serikali yetu kuliona hili swala kimapana zaidi ili kuongeza uwajibikaji kwa hawa Watumishi wetu.

Mungu ibariki Tanzania Mungu mubariki Rais wetu 🇹🇿
Ww unataka uwe mkuu wa idara? Kuwa na Master degree is just one of the requirements. Vigezo vipo ni vingi na pengine ndo havijakidhi viwango
vinavyotakiwa.
Eti mtu ametoka chuo na masters anataka kuwa mkuu wa Idara. Hapana. Lazima uangaliwe na ufanyiwe vetting.
 
Kwahyo mkuu Bora idara Iendelee kukaimiwa na mtu asiye na sifa huku mwenye sifa anasubiri kufanyiwa vetting 🤣🤣
Nashauri hizi kazi zitangazwe na watu waombe hayo Mambo ya vetting sometimes yapo very biased
 
LSSE ni noma....... Kuna mtaalamu yupo kakonko SEMA kama unahitaji msaada wake. Ukiitafuna dawa ukaenda tamisemi unaibuka na barua siku hiyo .
 
Hahaaaa umenichekesha Sana,
Anyway Mimi nimetoa maoni yangu kwahiyo isitafusiliwe vibaya
 
Kwahyo mkuu Bora idara Iendelee kukaimiwa na mtu asiye na sifa huku mwenye sifa anasubiri kufanyiwa vetting 🤣🤣
Nashauri hizi kazi zitangazwe na watu waombe hayo Mambo ya vetting sometimes yapo very biased
Ndiyo. Kinacho jaliwa hapo ni service delivery efficiency. Kama huduma za Idara zinaendelea kutolewa kwa ufanisi wa kiwango cha juu, huyo kaimu anatosha au vinginevyo wakiona inafaa wam-confirm au wamthibitishe awe mkuu wa Idara kamili.
Kutangaza kazi au nafasi wazi za Idara ni sawa lakini Mkurugenzi /TAMISEMI anayo kauli kubwa kutoa mapendekezo na maoni yake.
Kumbuka na zingatia kwamba hakuna chuo kinachosomesha Wakuu wa Idara.
Mkuu wa idara ni kiongozi tu au ni sawa tu na Monitor darasani.
Kuwa na Masters au Phd ni added advantage. Mkuu wa Idara, pamoja na Taaluma yake anapewa majukumu ya ziada tu e.g. kusimamia utendaji wa kila siku wa Watumishi/Watendaji walio ndani ya Idara husika na ndiye msemaji mkuu katika Idara hiyo. Anawajibika moja kwa moja kwa Mkurugenzi.
Sasa wapo wakuu wa Idara pamoja na Masters zao hawajui kujenga hoja mbele ya Vikao, hawajui kuandika na kutoa Taarifa sahihi ya kina, sio wabunifu ila kazi yao ni kukimbizana na madokezo/vocha kwa Mkurugenzi na hata wapo wengine ni wababaishaji tuu wanabeba mabegi yenye laptop tu lakini hakuna cha maana. Hao wanakuwa ni kero na wanaifedhehesha sana Idara/Halmashauri na Taasisi kwa ujumla.
 
Hizi nafasi Bora ziwe zinatangazwa kwenye ajira portal, hakuna halmashauri ingekuwa na mtu anayekaimu,
Ili uwe mkuu wa idara uwe senior kwenye utumishi wa umma na uwe na Masters hawa watu wapo
Sijaelewa vizuri unatangazaje nafasi ambayo ni nafasi ya Kuteuliwa? Hakuna mahali (labda nisahihishwe) mtu anaajiriwa kama Mkuu wa Idara kwani hakuna Chuo kinachosomesha na kutoa cheti cha "Mkuu wa Idara" kama Taaluma/Profession.
Watu seniors kwenye Utumishi wapo ni wengi sana, wenye masters nao si haba ni wengi pia. Lakini nafasi ya Mkuu wa Idara ni nafasi ya Kuteuliwa tu sio lazima ukiwa senior na una master basi automatically ww utakuwa Mkuu wa Idara. Yan bora useme kwamba ww unafaa kuangaliwa katika Kuteuliwa kuwa mkuu wa Idara. Na usipoteuliwa basi ridhika kwani mpo wengi na nafasi ya mkuu wa Idara huwa ni moja tuu. Usilazimishe au Usidai kana kwamba ni haki yako au kuna mtu amekukalia vibaya. Piga kazi kwa weledi na Uaminifu iko siku watakuona au watakukumbuka ktk Ufalme na kula mema ya nchi.
 
Kuna udhaifu kwakuwa nafasi hizo hazitangazwi watu wenye sifa waombe na kisha washindane.

Hata kama zitatangazwa kwa watumishi wa umma peke yake.

Matokeo yake vitengo wanapewa wale wanaoweza kula vizuri na mkurugenzi na wakubwa wengine. Kama hawana sifa basi watakaimu hapo miaka nenda rudi.
Mkuu; Katika hali ya kawaida katika Halmashauri zetu Nafasi ya Mkuu wa Idara hujazwa na mteule wa TAMISEMI. (I stand to be corrected). Mkurugenzi anayo mamlaka ya kuteua Kaimu Mkuu wa Idara. Kama TAMISAMI wakiona inafaa wanamthibitisha huyo kaimu kwa kumpa barua ya Uteuzi.
Sasa naomba nikuulize swali kidogo: Ungelikuwa ww ndiye Mkurugenzi ungemteua kaimu atakayekuwa ni kero kwako? Ungemteua yule anayepandisha mabega"Kujitutumua" eti kaenda shule lakini kiutendaji ni sifuri? Hapana. Si utamteua yule aliye mchapakazi mwaminifu na mtiifu kwako sio??
Habari za kula vizuri na Mkurugenzi ni za kupakazia hazina uthibitisho.
 
Sijaelewa vizuri unatangazaje nafasi ambayo ni nafasi ya Kuteuliwa? Hakuna mahali (labda nisahihishwe) mtu anaajiriwa kama Mkuu wa Idara kwani hakuna Chuo kinachosomesha na kutoa cheti cha "Mkuu wa Idara" kama Taaluma/Profession.
Watu seniors kwenye Utumishi wapo ni wengi sana, wenye masters nao si haba ni wengi pia. Lakini nafasi ya Mkuu wa Idara ni nafasi ya Kuteuliwa tu sio lazima ukiwa senior na una master basi automatically ww utakuwa Mkuu wa Idara. Yan bora useme kwamba ww unafaa kuangaliwa katika Kuteuliwa kuwa mkuu wa Idara. Na usipoteuliwa basi ridhika kwani mpo wengi na nafasi ya mkuu wa Idara huwa ni moja tuu. Usilazimishe au Usidai kana kwamba ni haki yako au kuna mtu amekukalia vibaya. Piga kazi kwa weledi na Uaminifu iko siku watakuona au watakukumbuka ktk Ufalme na kula mema ya nchi.
Kama hoja hujaielewa tulia, acha mengine yakupite
 
Ndiyo. Kinacho jaliwa hapo ni service delivery efficiency. Kama huduma za Idara zinaendelea kutolewa kwa ufanisi wa kiwango cha juu, huyo kaimu anatosha au vinginevyo wakiona inafaa wam-confirm au wamthibitishe awe mkuu wa Idara kamili.
Kutangaza kazi au nafasi wazi za Idara ni sawa lakini Mkurugenzi /TAMISEMI anayo kauli kubwa kutoa mapendekezo na maoni yake.
Kumbuka na zingatia kwamba hakuna chuo kinachosomesha Wakuu wa Idara.
Mkuu wa idara ni kiongozi tu au ni sawa tu na Monitor darasani.
Kuwa na Masters au Phd ni added advantage. Mkuu wa Idara, pamoja na Taaluma yake anapewa majukumu ya ziada tu e.g. kusimamia utendaji wa kila siku wa Watumishi/Watendaji walio ndani ya Idara husika na ndiye msemaji mkuu katika Idara hiyo. Anawajibika moja kwa moja kwa Mkurugenzi.
Sasa wapo wakuu wa Idara pamoja na Masters zao hawajui kujenga hoja mbele ya Vikao, hawajui kuandika na kutoa Taarifa sahihi ya kina, sio wabunifu ila kazi yao ni kukimbizana na madokezo/vocha kwa Mkurugenzi na hata wapo wengine ni wababaishaji tuu wanabeba mabegi yenye laptop tu lakini hakuna cha maana. Hao wanakuwa ni kero na wanaifedhehesha sana Idara/Halmashauri na Taasisi kwa ujumla.
Ila we jamaa Bwana🤣
 
Back
Top Bottom