Kikwava
JF-Expert Member
- Sep 6, 2015
- 1,741
- 1,068
- Thread starter
- #21
Sasa mtu hana sifa watamthibitishaje? Jaman hebu tujenge hoja zenye akili basi, tukizingatia Sheria za nchi yetuNdiyo. Kinacho jaliwa hapo ni service delivery efficiency. Kama huduma za Idara zinaendelea kutolewa kwa ufanisi wa kiwango cha juu, huyo kaimu anatosha au vinginevyo wakiona inafaa wam-confirm au wamthibitishe awe mkuu wa Idara kamili.
Kutangaza kazi au nafasi wazi za Idara ni sawa lakini Mkurugenzi /TAMISEMI anayo kauli kubwa kutoa mapendekezo na maoni yake.
Kumbuka na zingatia kwamba hakuna chuo kinachosomesha Wakuu wa Idara.
Mkuu wa idara ni kiongozi tu au ni sawa tu na Monitor darasani.
Kuwa na Masters au Phd ni added advantage. Mkuu wa Idara, pamoja na Taaluma yake anapewa majukumu ya ziada tu e.g. kusimamia utendaji wa kila siku wa Watumishi/Watendaji walio ndani ya Idara husika na ndiye msemaji mkuu katika Idara hiyo. Anawajibika moja kwa moja kwa Mkurugenzi.
Sasa wapo wakuu wa Idara pamoja na Masters zao hawajui kujenga hoja mbele ya Vikao, hawajui kuandika na kutoa Taarifa sahihi ya kina, sio wabunifu ila kazi yao ni kukimbizana na madokezo/vocha kwa Mkurugenzi na hata wapo wengine ni wababaishaji tuu wanabeba mabegi yenye laptop tu lakini hakuna cha maana. Hao wanakuwa ni kero na wanaifedhehesha sana Idara/Halmashauri na Taasisi kwa ujumla.