Kuna Watumishi wasiyo na sifa wanakaimu nafasi ya Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri kwa muda mrefu wakati wenye sifa wapo

Sasa mtu hana sifa watamthibitishaje? Jaman hebu tujenge hoja zenye akili basi, tukizingatia Sheria za nchi yetu
 
Acha kuwasagia kunguni wenzio.
Yeah. Kuna kitu Maslahi amekiona na amekuwa na matamanio nacho kwa siku nyingi. Hao ndo wakipewa Ukuu wa Idara ni hatari na nusu. Atapitia sketi zote Idarani kwake, kila vocha aipitishayo lazima iwe na 10%, atakumbatia mafungu yote ya miradi ya maendeleo, Hatotulia Ofisini kila siku yupo safarini(Semina, warsha, makongamano etc anageuka kuwa Vasco da Gama), anawafokea hovyo subordinates wake n.k.n.k.
 
Nawomba wadau msome uzi muuelewe vizuri ndo mchangie, si lazima uchangie Kama hujaelewa
 
Kuna wajanja huutumia kama mwanya was kupiga madeal na wahusika waliowekwa!!

Nilikuta certificate mmoja ni mwalim mkuu sehem,kumbe anagawana pasu kwa pasu Ile posho na DEO pale halmashauri ,yule DEO alipohamishwa tu Wakateuliwa makundi ya wakuu was shule wapya ili kuwaindoa wale vivuli!!
 
Una hoja ila Qualification ya wasailiwa pamoja na kuwa na Master pia awe na uzoefu kwenye idara hiyo sio chini ya Senior level au 10 years.
Usipofanya hivyo vijana wa Dotcom Hawa miaka 26/27 Wana masters ila hawana uzoefu. Watapasua usaili halafu akifika kule site anakutana na wazoefu miaka 15+ kazini wanaanza kumfundisha kazi. Heshima itapungua
 
Sasa mtu hana sifa watamthibitishaje? Jaman hebu tujenge hoja zenye akili basi, tukizingatia Sheria za nchi yetu
Ndo mana anaishia kwenye Kukaimu tu. Hiyo Nafasi itajazwa na TAMISEMI. TAMISEMI wanaweza kumhamishia mteule wao hapo au kumpromote mwenye sifa aliyeko hapo Halmashauri lakini atabadilishwa kituo cha kazi.
 
Hahaaaa ni noma
 
Exactly
 
Hadi Kaimu unamsagia kunguni kitu anachofaidi 40k ya Vikao
Sidhani kuwa ni hivyo bali naamini mdau anahoja asikilizwe. Kama hali iko hivyo kweli manake waliochini ya huyo kaimu akiwepo yy mwenyewe wanaona mambo hayaendi na huyo kaimu ana inferiority complex kiasi cha kuwaburuza wale anaowaongoza. Pengine dhana ya ushirikishwaji imemshinda huyo kaimu ila Mkurugenzi ameamua kumpotezea na kuacha mvurugano uendelee ndani ya Idara. Hiyo ni kero.
 
Tatizo lako hujaelewa hoja, pole sana
 
Kwanini hamuwezi mkausoma uzi na mkauelewa au jinzi umri unapozidi kwenda na akili zinayumba?
 
Upatikanaji wa hizo nafasi, mchoro wake ni 20 millions. Kupitia wizara ya Mkaza Mwana.
 
Yawezekana hao wasio na sifa wanasoma ili kufikia hizo masters hapo sawa lakini kama hawasomi na wameweka ndeke hapo kwa muda mrefu njoo inbox taja jina la huyo mtu mm namuanika hapa kama unaogopa kuanika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…