Ep 10
Turudi kidogo kwa mama, mjomba anafuatilia mpaka kijijini anajua kuwa sisi ni Watoto wake. Mjomba anaitisha kikao cha famila tukiwepo na sisi anamsema sana mama. Ila anamsamehe kwa sababu anampenda sana. Pili mjomba hakuwa na mtoto hata wa kusingiziwa. Anataka mama atuchukue tukae nae na sisi atatumbulisha kwenye familia yake kama Watoto wake. Mama anakubali ila mimi na Joy tunakataa kwenda kuishi kwa mama.
Mama anamwibia mjomba hela na kutorokea South Africa. Mjomba anaumwa sana pressure mara sukari ni mtu wa kuugua sana. Siku moja moja najiiba nikiwa chuo naenda kumsalimia mjomba kumbe na Joy huwa anaenda.
Mjomba anafariki dunia. Mali zake anatuandika mimi na Joy kama warithi lakini ndugu zake wanataka kututoa roho. Na sisi tunakataa kurithishwa mali za mjomba ila msiba tulishiriki lakini mama yetu hakuwepo.
Upande wa baba, bamkubwa mjeda anaamua kumpa mdogo wake mtaji (baba. Mungu anamnyoshea njia baba anainuka kidogo kidogo kiuchumi anafungua biashara ndogo ndogo amejenga amehamia kwake. Ana biashara ya kuuza nguo na mikoba Morogoro mjini. Amenunua bodaboda 4 na bajaji 2 amewapa vijana wanafanyia kazi. Na anaishi na mzee mwenzake. Yaani mama yetu mwingne wa kufikia mwanzo alitudanganya ni shangazi yetu lakini baadae tunajua kuwa ni mama yetu mpya hivyo tunamwita Aunt tunashindwa kubadilisha jina la aunt kuja kuwa mama hivyo tunaendelea kumwita aunt tu. (Aunt popote ulipo Mungu akupe Maisha marefu na yenye furaha nimekukumbuka sana)
Mamayetu wa kufikia nae ameachika kwa mume wake wa pili tunasikia yupo Arusha anafanya kazi za bar Watoto wake wanaishi na ndugu zake Morogoro yaani mdogo wetu mmoja na mtoto mwingine aliyemzaa kwa mume wake wa pili (Tutamuona tena msijali)
Mimi na Joy bado tunaendelea kuishi kwa ndugu zetu yaani mimi kwa babamdogo na Joy kwa Mjomba huku tukiendelea na masomo yetu.
Chuo kinakaribia kufungwa nawasiliana na Kaka Dav anaambia una mpango gani na rikizo namwambia sina mpango wowote zaidi ya kuwa tu nyumbani. Kaka Dav huwa namwambia baadhi ya changamoto zangu nazozipitia. Yeye alishamaliza chuo siku nyingi anafanya kazi kwenye enjioo ya wazungu. Ananiambia Lisa unajua maana ya likizo wewe maana yake ni kupumzika, unatakiwa upumzishe akili na mwili ukiendelea kukaaa hapo kwa babamdogo hutoona kabisa maana ya likizo. Namuuliza sasa nifanye nini akanambia unatakiwa uage hapo nyumbani useme kuwa unaenda field.
Kaka Dav mbona sio muda wa field kwa ratiba za chuo chetu? (chuo nachosoma hawana mambo ya field. Kaka Dav anafunga safari anakuja Dar anakutana uongozi wa chuo na kujitambulisha kuwa ni kaka yangu anaomba waniandikie barua ya field. Kweli wamekubali wananipa barua, Kaka Dav anasema nitaenda kufanya field kazini kwake. Swali linakuja nitatokaje pale nyumbani je wakisema field watanitafutia wao itakuwaje? Nampigia Aunt namweleza kila kitu anakutana na Kaka Dav wanaweka mipango sawa.
Aunt anamwambia baba kuwa amenitafutia sehemu ya mimi kufanya field baba anampigia baba mdogo na kumweleza kuwa aunt amenitafutia sehemu ya kwenda kufanya field hivyo likizo ikifika tu natakiwa kwenda Morogoro kwa ajili ya field.
Siku ya safari imefika ya kutoka Dar kwenda Moro kipindi hicho hata shule za kawaida zimeshafungwa nimeamka mapema nimefua nguo zangu na za wadogo zangu nimepanga kuondoka na Abood ya saa nane mchana. Mdogo wangu ameondoka ametumwa sijui wapi anampa maagizo mama yake amsaidie kumyoshea nguo zake jioni walikuwa na mtoko wa familia. Nguo alizo mwambia mama yake blauzi imefuliwa hipo kwenye nje Kamba imeanikwa.
Nimeshapaki mizigo yangu kwenye begi langu limejaa top kufunga kwenyewe mtihani. Nimeshaoga nipo chumbani kwangu navaa naona mtu anaingia bila hodi ni mamamdogo Lisa fungua begi lako haraka. Sijui sasa kinachoendelea mimi naendelea kumshangaa amefungua begi langu na kuanza kutupatupa vitu vyangu kuna blauzi ya mwanangu siioni hiko wapi aliniambia hipo kwenye Kamba nimyoshee naitafuta siioni hiko wapi?
Mimi nimebaki namshangaa anavyotupatupa vitu vyangu. Ameangalia kila sehemu hakuna anaondoka ananipa kazi tena ya kupanga upya vitu vyangu huku machozi yakinitoka nalia kwa hasira. Mdogo wangu anarudi kumbe ameivaa hiyo blauzi mama yake anamwambia kuwa alikuwa anaitafuta hajaiona, mtoto anamjibu mama yake kuwa ile nguo aliyokuwa amevaa aliona inampa joto hivyo akaamua kuivua na kuvaa hiyo blauzi wakati wa mtoko atavaa nguo nyingine.
Nimeshikwa na hasira natamani sijui niwafanyaje namfuata mama mdogo na kumuuliza ina maana ulihisi mimi naweza kuiba nguo ya mwanao inisaidie nini maneno yaninitoka kwa hasira.
Kosa! Nilipigwa babamdogo na mama mdogo walinipiga kama kibaka nilipigwa sana. Nikabeba mizigo yangu mpaka ubungo stend ya mkoa nimeingia kwenye abood naenda zangu Morogoro nikiwa mnyonge sana.
Nimefika Msanvu Aunt kaja kunipokea kanipeleka mpaka kwenye nyumba kuna wapangaji. Ananipeleka kwenye chumba kimoja. Akanambia Lisa mwanangu usiwe na wasiwasi mimi ndo nimemshauri baba yako akupangie chumba ukae hapa kipindi chako cha likizo unatakiwa kuwa huru mwanangu najua yote uliyoyapitia na unayoyapitia anaongea hivyo huku amenikumbatia. Kwa mara ya kwanza nakumbatiwa kwa upendo sana. Kweli kumbato ni tiba nikahisi kupona majeraha. (nakiri sijawahi kupata upendo kama wa huyu mama) hakika aunt nitakukumbuka daima.
Kwenye hicho chumba wameweka godoro, tv, redio, jiko la gasi na vitu vingine muhimu. Auntie ananipa maji naoga, anipa hela ya kujikimu. Anasema nijiandae tutatoka alafu kesho ndo atanipeleka nyumbani kwa baba tunatoka out anapiga simu Kaka Dav anakuja eneo la tukio amebadilika amependeza kweli pesa ni sabuni ya roho namuona kaka Dav naanza kulia upya wote wananikumbatia kwa pamoja yaani lisa najiona nipo dunia hipi sijui iliyojaa amani. (jamani hawa jamaa waliniharibu nikiwaga na mastress yangu nikikumbatiwa tu huwa najihisi tofauti kabisa nieleweke Lisa napenda kukumbatiwa ndo udhaifu wangu mkubwa)
Kesho yake auntie kanijia kunipeleka kwa baba kwakweli ushukuriwe Mungu baba yangu naye ana mji wake angalau hakai tena kwa watu. Baba yupo na nuru kumbe baba yangu ni kijana sio mzee kama alivyokuwa ametoka Tanga. Baba na aunt wananifurahia baba ananichinjia kuku ameweka kibanda cha kuku uwani yaani furaha tele kukutana na watu hawa. Nimekaa pale siku tatu huku moyo wangu una amani ile kesho niende kazini kwa kina kaka Dav kuanza field.
ALAMSIKI