Kuna wengine hatujui tulipokosea

Sasa Kwa Nini hukukagua jikoni ili ujue kama kweli yeye ndiyo alipika?
 
Ep 20

Baada ya kurudi Dar. Sikutaka kuwasiliana kabisa na Dav. Lakini mama yake tunawasiliana. Yaani nimeanza kuchoka vitimbwi vya Dav tumekaa miezi sita nikamsamehe tena. Baada ya kumsamehe alitoa mahali na kunivisha pete ya uchumba.

Taratibu za ndoa zimeanza taratibu kipindi hiki Dav anaonekana kutulia kidogo. Lakini ukiwa naye simu yake hana uhuru nayo mara azime mara aweke flight mode. Kuna wakati unampigia simu Dav anapokea mwanamke yaani sio Dav yule wa mwanzo huyu ni Dav mpya kabisa.

Ujenzi umeisha Dav inabidi ahamie kwake mama Dav akanipigia simu kuwa siku ya kuhama inabidi niwepo ili tusaidiane kupanga vitu. Sababu kama kujuana mnajuana kwahiyo jitahidi siku ya kuhamia uwepo sababu kutakuwepo na ibada na tafrija fupi. Kweli siku ya kuhamia nilikuwepo. Tumehamisha vitu na na wamefanya ibada pale ndugu zake Dav walikuwepo mimi alikuja tu rafiki yangu Jack.

Baada ya kuhamia familia zote mbili inabidi zikutane sasa ili mipango ya harusi ianze. Tofauti na kufanya kazi za kuajiliwa kwa watu na mimi nilikuwa na kibanda changu cha chips Mwenge hivyo lazima na mimi niweke utaratibu wa kuangalia biashara zangu zinavyoenda.

Nimerudi Dar naendelea na kazi zangu kama kawaida tukapata kazi ya tenda Morogoro kwahiyo inabidi nisafiri kwenda Morogoro kikazi. Lakini sikumwambia Dav kama naenda Morogoro. Nimefika zangu Morogoro tulifikia hotelini na boss wangu na wafanyakazi wenzangu. Tumekaa siku mbili baada ya kumaliza shughuli zetu tunatakiwa kurudi dar. Mimi nilikataa kurudi nao nikawaambia watangulie mimi naenda nyumbani kwanza kusalimia.

Lengo si kwenda kwa baba tangu aondoke auntie nyumbani siendi mara kwa mara nia yangu ilikuwa kwenda kwa Dav kumfanyia surprise sababu ilikuwa jumapili nilikuwa na uhakika kuwa Dav atakuwepo nyumbani. Na kabla sijaenda nilimpigia kuumuliza yupo wapi akanambia yupo nyumbani na mimi sikutaka kumwambia kuwa nipo Morogoro. Basi nikachukua zangu bodaboda kutoka Morogor mjini mpaka nimefika getini nimemlipa boda. Geti limeegeshwa kidogo mimi Lisa huyo ndani.

Mlango wa kuingilia ndani ulikuwa umefungwa nikanyonga zangu kitasa nikaingia zangu ndani. Nailaani sana siku hii sikuamini nilichokiona. Nilimkuta Dav amekaa kwenye sofa kifua wazi, amevaa pensi tu miguuni kwake amejaa yule dada aliyempikiaga chakula kipindi anaishi kwenye nyumba ya kupanga na dada yule alikuwa kajaaliwa jamani amejifunga kanga moja amemlalia Dav.

Sikujua kilichotokea baadae nilikuja kujikuta hospitali mama Dav yupo pembeni yake. Nililia sana siku hiyo nahisi hata msiba sijawahi kulia hivyo. Mama alinizuia nisiongee chochote mpaka nitakapokuwa sawa. Nikaendelea vizuri nikaruhusiwa kutoka hospitali nikapelekwa kwa mama yake Dav na sikutaka kuongea chochote niligeuka bubu si kwamba siwezi kuonge ila sihitaji kuongea chochote wala kuongea na yeyote yaani kwa ufupi nikawa kama zezeta. Baba alikuja kunichukua kwa mama Dav na kunipeleka nyumbani kwake. Pale pia sina amani make mimi na mama yetu wa kufikia hatupo sawa. Nikamwomba baba ruhusa nirudi Dar nikajitahidi asione kama nipo mnyonge. Baba akaniruhusu na kunipa dogo anaisindikize. Kumbuka dogo Dav kapita lakini nitamwambiaje baba uchafu huu. Nikakubali nilivyofika Dar tu baada ya siku mbili nikamwambia dogo arudi moro nisijekumzuru na nikamwambia uking’ang’ania kukaa hapa eti unanipa huduma nitamwambia baba kuwa na wewe umetembea na Dav na Ushahidi ninao. Dogo kusikia hivyo alikubali kuondoka.

Nikaanza kunywa tena viloba nikaacha kwenda kazini yaani nipo nipo tu. Tunaweza kuwa nimekaa na watu tunaongea kawaida ghafla naanza kupiga kelele yaani kwa ufupi nilikuwa chizi fresh kuna muda nakuwa sawa kuna muda zinahama. Jack rafiki yangu alikuja akanichukua na kunipeleka kwake akawa ananipa ushauri. Akanianzishia uji wa lishe yaani na afya yangu ilidorora sana. Nilivyokaa kwa jack nikaona afya yangu inaimarika nikarudi kule nilipokuwa nimepanga nikachukua vitu vyangu na kuhamia sehemu nyingine na kazi nikaacha lengo nikutoka katika sehemu ambayo Dav anaweza kunipata. Nikabadilisha line ya simu na nikamtoa Dav kabisa kwenye Maisha yangu. Familia yangu akiwemo mama yake Dav walijitahidi sana kunisihi lakini nilikataa nikaamua kuishi ulimwengu wangu. Kama sikujiua kipindi hicho hata itokee nini siwezi kuchukua Maisha yangu.

Nikirudi nitaandika nitajitahidi kusumarize ili tumalizane na hili nishachoka. Muwe na siku njema.
 
Episode nimeisoma kwa hisia sana, pole sana
 
Siku ukila matunda nisiyokwambia ule utakufa.

Dadakidoti dav kalishwa vzuri ndy mana long distance sio nzuri .Lazima nikae na wewe karibu ili mambo yawe sawa.
 
asante. hayo ni matokeo unapompenda mtu asiyetambua thamani yako.
Maskin pole sana Mungu atakupa mume mwema ataekufuta machozi yako🥺☹️😪 Dah! hivi inawezekana ikawa karma baba alivomtenda Auntie ndo na nyie binti zake hamjapata wanaume wema?? Mlilie sana Mungu na uwaombee msamaha wazazi naamini utapata mume mwema Lisa usikate tamaa, umepitia mitihani mingi
 
Kiroho ni kuwa baada ya kutolewa mahali wewe ni mke halali kabisa wa Dav na kimila pia ukikutana na Hali kama hizo inabidi upambane kama mama mjengo na sio kukimbia.

Na kama humtaki tena inabidi urudishe mahali ili upate mwenza mwengine wa kufangamana na roho yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…