Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umechelewa sie wenzio tumeweka makao kabisa!Naweka kambi hapa
Sasa Kwa Nini hukukagua jikoni ili ujue kama kweli yeye ndiyo alipika?Ep 19
Pigo la tatu.
Tabia ya mtu ni Ngozi kuibadilisha ni vigumu Dav haimbiliki wala hasikii. Kama ilivyo kawaida tukimisiana mmoja lazima amfuate mwenzake. Baba D amenitumia nauli niende Moro kama ilivyo kawaida yangu naondoka ijumaa jioni kutoka ubungo.
Siku hiyo gari niliyopanda ilipata shida kidogo njiani hivyo ilitupelekea mimi na abria wenzangu kufika stand ya msamvu usiku mkubwa sana. Wakati tupo njiani tunawasiliana na baba D nikimwambia tumefika hapa tumefika hapa. Hivyo nilivyofika tu Msamvu nilimkuta baba D ananisubiri amakeja kunipokea.
Tupo njiani sioni baba D aniulize nakula nini sababu ndo ilikuwa kawaida yake baba D kuniuliza unakula nini ili anunue chakula. Tulipofika nyumbani baada ya kumaliza kuoga baba D ananikaribisha chakula. Nilimuuliza baba D umepata wapi chakula? Akaanza kusema mama D hivi huamini kama mimi najua kupika? Wewe tangu lini ukapika leo ukapika ninavyokujua ulivyo mvivu wewe. Nimekupikia bwana ebu njoo ule uache maswali yako. Haya baba D ngoja leo nionje mapishi yako. Wali umepikwa umepikika sijui uliwekwa nazi mboga nazo zimeungwa na nazi. Nikala mimi mtoto wa watu huku nikijiuliza ameanza lini kupika huyu chai yenyewe kuchemsha kwake ni mtihani. Iweje leo amepika tena mpaka nazi. Nitapata jibu tu. Nimekula tumelala zetu.
Asubuhi nimeamka kama mnavyojua wadada tunajifanyaga wife material tukifikaga kwa maboyfriend zetu. Nilikusanya nguo chafu nimefua lakini ikifika muda wa kusuuza baba D ananiwahi anasuuza na kuanika yeye tulikuwa tunafulia ndani, tumeosha vyombo tumemaliza nimedeki ndani nataka nitoke nje kudeki barazani akaniwa mama D acha tu nitamalizia mimi nikamwachia huku nikimshangaa ana nini huyu. Ameniacha napika chai akaenda kununua vitafunwa.
Tumepanga jioni twende kumsalimia mama yake (nieleweke Dav ni mtoto wa mama) tumekunywa chai. Muda wa kupika umefika namfuata baba D na kumuuliza tunapika nini? Akanijibu mama D wewe kampuzike tu mtu umefika usiku mkubwa kufua na usafi utakuwa umechoka sana. Kwa hiyo kuhusu chakula nitashughulikia nikasema sawa. Kusema ukweli nilikuwa nimechoka sana baba D yupo bize na laptop yake. Nikaamua kwenda zangu chumbani kupumzika nilipitiwa na usingizi. Nakuja kustuka baba D ananiamsha nikale. Nimeamka baba D kanibeba mpaka sebuleni nakuta chakula kimeshatengwa.
Baba D naomba unieleze ukweli hiki chakula kimetoka wapi toka usiku bado najiuliza umewezaje kupika chakula kama kile? Nakujua wewe ni mvivu chai tu inakushinda inakuwaje chakula tena mpaka nazi?
Mama D acha wivu ebu tule bwana. Si unajua tutaenda bibi D tena ngoja nimpigie simu hapa.
Usinizuge kwahiyo bibi D ndo amepika hiki chakula? Ananizuga zuga pale mwisho natulia tunakula lakini kichwani nikijisemea lazima nijue kinapotokea hiki chakula.
Tumepumzika jua limepungua tumejiaandaa hao kwa bibi D. Tumefika kwa bibi D ametupokea vizuri lakini mazungumzo ya bibi D anasisitiza ndoa hataki tuendelee kuishi Maisha haya tunayoyaishi mmoja Dar mwingine Morogoro sio mazuri kabisa. Tunamwaahidi bibi D kuwa tutalifanyia kazi hivi karibuni. Tumeongea sana na bibi D jioni imeingia bib D anatufukuza akimsisitiza Baba D anirudishe nyumbani mapema. Hajui kama tumelala wote na sasa naenda tena kwa baba D.
Tukaondoka zetu tumefika nyumbani usiku saa mbili nataka kupika tena ananizuia kuwa nisipike. Na kila kitu kipo ndani nikajifanya mjinga ili nijue chakula kinapotokea.
Huku nikijichekesha chekesha kinafiki nikambwambia sawa nipo chumbani nimepunzika kidogo. Poa nitakuamsha uje kula.
Nipo chumbani kama dakika 20 hivi Dav akaja kuanza kuniita mama D, Mimi kimya mama D…. Lisa Lisa. Mimi nikajifanya nimelala usingizi mzito. Dav akatoka chumbani nikamsikia anaongea na simu akisema Baby waweza kuniletea hicho chakula. Mke mwenzio amelala fanya haraka asije akakusikia sababu naona ameanza kuwa na mashaka.
Nikasema shenzi huyu kumbe hanunui chakula kinapikwa tena na mtu amemuita baby. Nikakaa chonjo ili nimuone huyo mpishi.
Baada ya kimya kidogo nikasikia Watoto wanaita anko Dav tumeleta chakula. Aisee mapenzi yanauma. Nilitoka chumbani sikujua nilipitaje sebuleni nikajikuta nipo nje Dav anapokea kile chakula. Nikamshika mtoto alikuwa kama miaka sita hivi nikamuuliza ehe mtoto nani amekupa chakula hiki akasema mama ndo amesema tumletee anko Dav. Nikakishika kile chakula nikarudishia mtoto nikimwambia kamwambie mama kuwa mke wa anko dav ameshapika.
Dav alichukua kile chakula na kunipiga makofi mawili matakatifu na ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kunipiga lakini sikukubali nikamwambia Dav kwa usalama wetu naomba hiki chakula kirudi kilipotoka au mimi niondoke ubaki na chakula chako. Niliingia ndani nikachukua mizigo yangu tayari kwa safari. Dav akanizuia. Nilinyamaza na kuanza kulia Dav alivyotulia nikachukua simu nikampigia mama Dav na kumweleza kila kitu huku nalia kwa kwikwi. Dav akiwa bafuni. Mama Dav alichukua bodaboda na kuja pale Dav hakuamini kama ningeweza kufanya hivyo. Basi mama alilalamika sana vijana wa siku hizi tusivyokuwa na maadili mimi moyoni nasema Dav kamwaga mboga na mimi nimemwaga ugali kama tunaachana sawa tu,
Basi mama akaniuliza nataka nini nikasema nataka aliyepika chakula aitwe na akanywe aache kabisa kumpikia Dav chakula. Mama akakubaliana na mim akamwamuru Dav kumpigia simu huyo mpishi. Kweli yule dada alikuja lakini wakajitetea kuwa Dav huwa anampa hela anampikia. Wamepanga nyumba moja lakini aprtiment tofauti.
Mama akalalamika sana mimi ndio maana natamani muoane hata leo yaani ningekuwa mwislam leo ningewapiga ndoa ya mkeka. Fanyeni haraka muoane mimi sipendi Maisha yenu ya kihuni haya. Mgekuwa mnaishi pamoja haya yote yasingetokea. Mama akaacha hali hiko poa akaondoka hakuna aliyeongea na mwenzake mpaka asubuhi niliondoka pasipo kumuaga Dav.
Nilimtumia ujumbe Dav imekwisha sasa endelea kubaki na huyo anayejua kupika mimi sijui kupika. Dav hakunijibu. Nilirudi zangu Dar na kufikia kwa shoga yangu Jack ila nikiri Mungu amenipa huyu mtu. Jack nakupenda sana kipenzi unajua kubebamatatizo yangu. Nikilia nalia nae asant Jack.
natamani kumaliza jamani.
ulikuwa ni usiku mkubwa pia nilikuwa nimechoka na safari kwa wakati huo haikuwa rahisi kukaguaSasa Kwa Nini hukukagua jikoni ili ujue kama kweli yeye ndiyo alipika?
sikia mwa mtu usiombe ikakukutaTamu sana
kutuka abiria mwenzangu - kaka- mupenzi- baba d otea akitoka baba d atakuwa nani?Awiiiiwwwww dav keshakua Baba D
kutuka abiria mwenzangu - kaka- mupenzi- baba d otea akitoka baba d atakuwa nani?
Atakuwa baba watoto wako,hamna namna,utamsamehe na kuyajenga upyakutuka abiria mwenzangu - kaka- mupenzi- baba d otea akitoka baba d atakuwa nani?
Episode nimeisoma kwa hisia sana, pole sanaEp 20
Baada ya kurudi Dar. Sikutaka kuwasiliana kabisa na Dav. Lakini mama yake tunawasiliana. Yaani nimeanza kuchoka vitimbwi vya Dav tumekaa miezi sita nikamsamehe tena. Baada ya kumsamehe alitoa mahali na kunivisha pete ya uchumba.
Taratibu za ndoa zimeanza taratibu kipindi hiki Dav anaonekana kutulia kidogo. Lakini ukiwa naye simu yake hana uhuru nayo mara azime mara aweke flight mode. Kuna wakati unampigia simu Dav anapokea mwanamke yaani sio Dav yule wa mwanzo huyu ni Dav mpya kabisa.
Ujenzi umeisha Dav inabidi ahamie kwake mama Dav akanipigia simu kuwa siku ya kuhama inabidi niwepo ili tusaidiane kupanga vitu. Sababu kama kujuana mnajuana kwahiyo jitahidi siku ya kuhamia uwepo sababu kutakuwepo na ibada na tafrija fupi. Kweli siku ya kuhamia nilikuwepo. Tumehamisha vitu na na wamefanya ibada pale ndugu zake Dav walikuwepo mimi alikuja tu rafiki yangu Jack.
Baada ya kuhamia familia zote mbili inabidi zikutane sasa ili mipango ya harusi ianze. Tofauti na kufanya kazi za kuajiliwa kwa watu na mimi nilikuwa na kibanda changu cha chips Mwenge hivyo lazima na mimi niweke utaratibu wa kuangalia biashara zangu zinavyoenda.
Nimerudi Dar naendelea na kazi zangu kama kawaida tukapata kazi ya tenda Morogoro kwahiyo inabidi nisafiri kwenda Morogoro kikazi. Lakini sikumwambia Dav kama naenda Morogoro. Nimefika zangu Morogoro tulifikia hotelini na boss wangu na wafanyakazi wenzangu. Tumekaa siku mbili baada ya kumaliza shughuli zetu tunatakiwa kurudi dar. Mimi nilikataa kurudi nao nikawaambia watangulie mimi naenda nyumbani kwanza kusalimia.
Lengo si kwenda kwa baba tangu aondoke auntie nyumbani siendi mara kwa mara nia yangu ilikuwa kwenda kwa Dav kumfanyia surprise sababu ilikuwa jumapili nilikuwa na uhakika kuwa Dav atakuwepo nyumbani. Na kabla sijaenda nilimpigia kuumuliza yupo wapi akanambia yupo nyumbani na mimi sikutaka kumwambia kuwa nipo Morogoro. Basi nikachukua zangu bodaboda kutoka Morogor mjini mpaka nimefika getini nimemlipa boda. Geti limeegeshwa kidogo mimi Lisa huyo ndani.
Mlango wa kuingilia ndani ulikuwa umefungwa nikanyonga zangu kitasa nikaingia zangu ndani. Nailaani sana siku hii sikuamini nilichokiona. Nilimkuta Dav amekaa kwenye sofa kifua wazi, amevaa pensi tu miguuni kwake amejaa yule dada aliyempikiaga chakula kipindi anaishi kwenye nyumba ya kupanga na dada yule alikuwa kajaaliwa jamani amejifunga kanga moja amemlalia Dav.
Sikujua kilichotokea baadae nilikuja kujikuta hospitali mama Dav yupo pembeni yake. Nililia sana siku hiyo nahisi hata msiba sijawahi kulia hivyo. Mama alinizuia nisiongee chochote mpaka nitakapokuwa sawa. Nikaendelea vizuri nikaruhusiwa kutoka hospitali nikapelekwa kwa mama yake Dav na sikutaka kuongea chochote niligeuka bubu si kwamba siwezi kuonge ila sihitaji kuongea chochote wala kuongea na yeyote yaani kwa ufupi nikawa kama zezeta. Baba alikuja kunichukua kwa mama Dav na kunipeleka nyumbani kwake. Pale pia sina amani make mimi na mama yetu wa kufikia hatupo sawa. Nikamwomba baba ruhusa nirudi Dar nikajitahidi asione kama nipo mnyonge. Baba akaniruhusu na kunipa dogo anaisindikize. Kumbuka dogo Dav kapita lakini nitamwambiaje baba uchafu huu. Nikakubali nilivyofika Dar tu baada ya siku mbili nikamwambia dogo arudi moro nisijekumzuru na nikamwambia uking’ang’ania kukaa hapa eti unanipa huduma nitamwambia baba kuwa na wewe umetembea na Dav na Ushahidi ninao. Dogo kusikia hivyo alikubali kuondoka.
Nikaanza kunywa tena viloba nikaacha kwenda kazini yaani nipo nipo tu. Tunaweza kuwa nimekaa na watu tunaongea kawaida ghafla naanza kupiga kelele yaani kwa ufupi nilikuwa chizi fresh kuna muda nakuwa sawa kuna muda zinahama. Jack rafiki yangu alikuja akanichukua na kunipeleka kwake akawa ananipa ushauri. Akanianzishia uji wa lishe yaani na afya yangu ilidorora sana. Nilivyokaa kwa jack nikaona afya yangu inaimarika nikarudi kule nilipokuwa nimepanga nikachukua vitu vyangu na kuhamia sehemu nyingine na kazi nikaacha lengo nikutoka katika sehemu ambayo Dav anaweza kunipata. Nikabadilisha line ya simu na nikamtoa Dav kabisa kwenye Maisha yangu. Familia yangu akiwemo mama yake Dav walijitahidi sana kunisihi lakini nilikataa nikaamua kuishi ulimwengu wangu. Kama sikujiua kipindi hicho hata itokee nini siwezi kuchukua Maisha yangu.
Nikirudi nitaandika nitajitahidi kusumarize ili tumalizane na hili nishachoka. Muwe na siku njema.
asante. hayo ni matokeo unapompenda mtu asiyetambua thamani yako.Episode nimeisoma kwa hisia sana, pole sana
Kweli aisee, nikiwa mkubwa sitaki niwe kama dev😂asante. hayo ni matokeo unapompenda mtu asiyetambua thamani yako.
Nambie yupo zenji sehemu gani nikusaidie kumtafutanimemmisi auntie wangu ila ninaamini hipo siku nitakutana nae. mtu mmoja aseme neno moja kwa ajli ya auntie
Maskin pole sana Mungu atakupa mume mwema ataekufuta machozi yako🥺☹️😪 Dah! hivi inawezekana ikawa karma baba alivomtenda Auntie ndo na nyie binti zake hamjapata wanaume wema?? Mlilie sana Mungu na uwaombee msamaha wazazi naamini utapata mume mwema Lisa usikate tamaa, umepitia mitihani mingiasante. hayo ni matokeo unapompenda mtu asiyetambua thamani yako.