We manka ungeweza ? Kupikiwa chakula ukitoka nje hutakiwi uonekane....... Yeeewoomiii 😂Hapo ulikosea nawe ungeacha Move uendelee 😅😅😅mtu anakupikia msosi mzuri hivo hadi nazi 😅😅😅
Nimeumia kwa nini hukuzaa na Dav 😊kwa lile Penzi shata shataEp 21
Siku zilienda Dav hakuamini kama ningesema basi. Nilirudisha pete kwa mhuisika Dav hakuamini kama ningemwacha nilimwambia kuwa siku ukiona umebadilika na unaweza kuniheshimu japo kidogo na kutulia utanitafuta ila sio kwa sasa Dav nahitaji kupumzisha akili yangu sasa. Nikikaa sawa nitakwambia ila sidhani kama naweza kukusamehe. Hivi hatujaoana Dav huko hivi ukiniweka ndani ukajua tayari nipo chini ya himaya yako itakuwaje. Kinachoniuma mwanamke yuleyule toka umepanga mpaka umejenga kwako bado tunakosana kwa sababu yake. Kitanda kilekile ninachokilalaiaga mimi bora mgeenda sehemu nyingine si hapa. Au ningewakuta sehemu nyingine sio hapa kwako ningekusamehe kabisa. Au angekuwa mwanamke mwingine siku ile si ulikana ukasema ulikuwa unampa hela ili akupikie na hapa alikuja kukupikia tena sababu unampa hela? Dav alilia sana, alinipigia magoti lakini sikujali kilio chake wala magoti yake niliondoka zangu nikawaacha kwenye kikao na nikaazimia kumuondoa Dav kabisa Dav kweye Maisha yangu na nilifanikiwa kumuondoa mazima.
Mahusiano yangu na Dav yalidumu kwa miaka mitatu na miezi minne na kipindi chote hicho japo ilikuwa long distance relationship sikuwahi kumsaliti wala kuwaza kufanya hivyo mpaka tunaachana. Nikawa bize na Maisha yangu japo ilikuwa ngumu lakini mwisho wa siku niliamua kukubali matokeo.
Maisha yana pilika pilika nyingi sana. Kwenye heka heka za hapa na pale nikakutana na kijana mwingine mtanashati ni daktari katika hospitali kubwa hapa dar alinisumbua kwa kipindi cha mwaka na zaidi. Nilishamtoa Dav kwenye akili yangu nikaamua kuwa naye ila kumbe yule jamaa alikuwa ameoa na ana Watoto watatu familia yake inaishi mkoani lindi.
Nilivyogundua tu sikutaka kuangalia nyuma wala sina cha kupoteza kwake nikakimbia futi mia. Hakuna mtu namwogopa kama mume wa mtu. Maisha yalisonga nilikaa single miaka miwili yaani mtu akiniambia habari za mapenzi simwelewi kabisa hata kidogo. Nikaamua kujikita kwenye kazi zangu.
Nikaja nikakutana na huyu mpendwa namaanisha mlokele ni mtu maarufu kidogo nikaanza nae mahusiano nikiamini huyu ni mtumishi wa Mungu hawezi kunitenda. Msinilaaumu jamani Lisa nakula nashiba kuna siku tulijikuta tumevunja amri ya sita hata sielewi ilikuwaje. Mungu naye hakuwa mbali jamani mimba hiyo. Nikalea mimba yangu mpendwa yule naye kumbe ni silent killer ana matukio yake pia. nikaamua sasa kuwa bize na mimba yangu.
Namshukuru sana Mungu alinijalia handsome boy mwanangu ana miaka miwili sasa ananipa kila sababu ya kupambana. Sasa hivi nina amani na katoto kangu nikiwa single mother.
Kuhusu nyumba ya antie aliyokuwa anajenga niliimalizia na document zake ninazo mimi siku yoyote akitokea nipo tayari kumpa pasipo kudai chochote kile.
Dav alikuja kuoa mwanamke mwingine lakini walishindwana. Walikatana mpaka mapanga wakapelekana mpaka mahakamani. Dav siku hizi ni chapombe ana midevu kama osama yaani usmat ule hana tena nilikutana mwaka juzi nilivyooenda kumsalimia baba tulikutana mjini bahati mbaya nikiwa na kichanga aliumia sana. Kuna siku huwa anamfuata baba yangu na kuanza kumsumbua baba kuwa mimi nimke wake anamtaka mke wake nilimwambia baba ampeleke polisi. Ila baba hataki anampenda Dav ila mimi nilishakula viapo na viapo siwezi kurudi tena kwa Dav. Simchukii nilishamsamehe kabisa ila pia simpendi namchukulia kama mtu wa kawaida tu.
Mama naye yupo south Africa kuna kipindi aliumwa sana alipata ajali akateguka mguu akawa anahitaji msaada wetu ndugu zake wakatwambia kuwa twende kumuuguza tukagoma sio mimi sio Joy alikubali kwenda south Africa kumuuguza ilibidi aende mdogo wake. Alivyopona tu alikuja Tanzania akatuomba msamaha, tulimsamehe hivyo alirudi south kuendelea na Maisha yake ila tuko poa kabisa. Joy naye anaendelea vizuri mwezi wa 7 tunatarijia kula ubwabwa mdogo wangu antarajia kufunga ndoa. Hatuna ukaribu wa kivile ila tunawasiliana japo kidogo kidogo.
Baba naye ndoa yake inapumulia gas walitengana chumba na mama yetu wa kambo na mdogo wetu ni mdangaji maarufu Morogoro mjini. Yaani ni ameshindikana. Kwa baba mimi na Joy tuliacha kwenda kabisa nina miaka mitatu toka nilivyoenda mwaka 2021 sijawahi kukanyaga tena. Nikimmisi baba yangu huwa najitahidi kwenda na mabus ya kufika mapema moro na mtoto wangu tunafikia ofisini kwa baba jioni tunaru zetu Dar naondoka juu kwa juu.
Katika hekaheka zote hizo nimefanikiwa kujenga kakibanda kangu kadogo kazuri japo si kivile lakini kanaridhisha kapo Mbezi Msumi. Nitaarajia kuhamia kabla ya pasaka mwaka huu. Nina amani furaha na afya njema mimi na mtoto wangu tuko poa kabisa.
Sijutii kuwa single mother sababu mtoto wangu ananipa kila namna ya kupambana na ndiye mtu pekee niliye naye katika Maisha yangu japokuwa ni mdogo lakini ananipa furaha. Nina amani na sasa hivi naufanyia kazi msemo wa Joy naishi ulimwengu wangu kabisa. Mwanangu ndiye dunia yangu.
Asanteni kwa kuwa na mimi, niliyemkosea au kumkwaza kwa namna moja ama nyingine naomba anisamehe. Na samahani kwa kuwachosha ila nina Imani kuna mtu japo mmoja amejifunza kitu kutokana na historia ya Maisha yangu.
NAWAPENDA!
Mwishooooo.
Tena wakati mwingine wangenishirikisha ningewaandalia ratiba kabisa mimi nilale tu 😅😅😅😅😅nawapongeza sana kwa jitihada zao za mapishi kabambe.We manka ungeweza ? Kupikiwa chakula ukitoka nje hutakiwi uonekane....... Yeeewoomiii 😂
Daaah mapenzi ya hovyo hasa yakikukaa kichwani unaweza ua mtu 😂😂Tena wakati mwingine wangenishirikisha ningewaandalia ratiba kabisa mimi nilale tu 😅😅😅😅😅nawapongeza sana kwa jitihada zao za mapishi kabambe.
kipenzi sioni cha kunipeleka kanda ya ziwa tena. mwaka juzi mwezi wa kumi nilimzika babu yangu mzaa mama, mwaka jana nimemzika mwezi wa tatu nikamzika babu mzaa mama na mwaka jana pia mwezi wa nne nikamzika tena bibi mzaa mama. kwahiyo hao waliokuwa kama wazazi kwangu wameondoka tena kwa kufuatana ulikuwa mwaka mgumu sana kwangu.Dadakidoti
Mda sasa hujaenda kanda ya ziwa kwa akina baby ujue
Poleni sanaaEp 17
Mapicha picha yameanza nyumbani. Ukienda kama baba hayupo kulala njaa ni kawaida tena mama yetu wa kamboa haoni aibu kukwambia kuwa kuwa leo hatujapika mwanangu huku hakijichekesha hivyo sisi na wadogo zako tumeshakula vitumbua, au maandazi hivyo wewe nawe fanya mpango wako wa kula sisi tumeshashiba. Yaani nyumbani pamebadilika sio mimi sio Joy anayeenda pale asikumbuke uwepo wa Auntie.
Kuna siku nimeenda mororogoro tulikuwa na safari yetu mimi Dav tulikuwa tunaenda Arusha Vacation nikaamua kupitia nyumbani kuwa salimia siku moja kabla ya safari. Chumba changu kimejaa vitu vya auntie, kuanzia nguo zake na makabati yake huwezi kulala mule kwa ufupi kimegeuka stoo ya vitu vya auntie.
Joy mazoea hataki kabisa chumba chake kimefungwa na funguo anazo mwenyewe. Chumba cha wageni kuna ndugu yetu mtoto wa shangazi amefikia pale kutoka kanda ya ziwa kufanya shughuli zake na kuondoka.
Nikaamua kulala chumbani kwa wadogo zangu. Morogoro hali ya hewa ni baridi kidogo tofauti na hali ya hewa ya Dar. Nikachukua gauni langu nimelala nimelivaa. Alfajiri kama saa kumi nastuka usingizini nakuta wenzangu wamelala chini. Nashangaa nimelowa mwili mzima. Mdogo wangu akaniuliza dada umelowa? Nikamwitikia ndio akaguna kwanza pia akasema pole sana dada angu nitafanyaje sasa.
Sikumtilia maanani sana nikahisi labda mdogo wake atakuwa anakojoa kitandani japo ni bint mkubwa tu darasa la sita. nikaamka nikajiandaa na kubeba mizigo yangu na kwenda zangu kwa Dav kwa ajili ya safari. Nguo zangu zilizolowa nikaziweka kwenye mfuko. Nimefika kwa Dav tunaenda kwa mama kwanza kumsalimia safari yetu ni kesho yake. Jioni tumerudi kutoka kwa mama yake Dav ndo nakumbuka nguo nilizoziweka kwenye mfuko. Nikazifuata kwa lengo la kuzifua nikihisi ni mikojo tu lakini ajabu ngu hazinuki hata mkojo na yule bint ana miaka kama 14 mpaka 15 hivi na mkojo wa mtu mzima unavyonuka. Ndio nikagundua kuwa watakuwa walinimwagia maji.
Siku zimeenda namuona mdogo wetu ambaye ni mtoto wa baba na mdogo wake ambaye ni mtoto wa mama yake aliyemza huko kwingine Watoto wameanza dharau siwaelewi. Pale lazima niende kwa sababu ni kwa baba yetu. Joy akienda lazima atatoka kule wamegombana hatuna ukaribu sana na Joy lakini changamoto tunazokutana nazo kwa baba tunaambiana.
Joy ni mkorofi sana hivyo ukitokea umemchokoza unakuwa umewasha moto. Kuna kipindi cha likizo Joy alienda kukaa kule kwa ajili ya likizo yake. Yaani kulikuwa pa moto sana. Ilifika hatua Joy akawa anapika chakula chake na wao wanapika chukula chao. Yaani ni fujo tu. Kuna siku baba alinipigia simu kuhusu Joy anavyokuwa hana adabu na ametaka kuwakalisha kikao Joy kakataa kasema mpaka mama yake au antie mmojawapo awe kwenye hicho kikao ndio atakubali kukaa kikao. Na anajua kuwa haiwezekani ili mradi tu fujo.
Mama mdogo (mama wa kambo) ananigombanisha na baba yangu
Siku zimeenda sana nimemkumbuka baba yangu naamua kumpigia simu. Nilipiga sana simu inaita tu haipokelewei, nikawa na wasiwasi juu yake. Nilikaa muda kidogo nikaamua kupiga tena.
Simu ilipokelewa na mama yetu wa kufikia. Hakunisalimia anaongea kwa jeuri unapiga simu sana wewe na ukiona simu yako haipokelewei jua mwenye simu hayupo. Hiyo kauli ilinikera nilikuwa sijawahi kumjibu ila siku hiyo nilimjibu na mimi nilikuwa sikupigii wewe nilikuwa nampigia baba yangu. Akanambia huyo ni mume wangu
Namimi ni baba yetu tena mama yetu ulimkuta na alikuwa amefunga ndoa na baba yangu tena ya kanisani si kama yakwako ya bomani na umetukuta hivyo tuheshimu ili na sisi tukuheshimu. Pia usisahau mama yetu alichumbiwa na kutolewa mahali.
Sikutaka kusikia neno lingine kutoka kwake.
Kumbe nilipokata simu akaanza kujiliza na kuanza kusema kuwa nimemtukana nasikia baba alivyorudi alimwambia kuwa nimemtukana na kumuita baa med kuwa yeye na baba wote ni wahuni tu kwani walikutana bar na maneno mengine mengi. Hayo aliniadithia Joy sababu kipindi hicho alikuwa Morogoro akiwachachafya na fujo zake.
Nimekaa kama wiki moja tena nikampigia baba yangu simu lakini akawa hapokei namtumia ujumbe hajibu. Nikaamua kuwapigia ndugu zake na kuuliza kama kuna tatizo wakanambia kuwa baba aliwapigia na kuwaeleza kuwa nilimtukana hivyo hanitambui tena kama mtoto wake.
Nilivyoambiwa vile nikamtumia baba ujumbe na kumwambia. Asante baba unawaambia watu kuwa nimekutakana wewe na mke wako na kuwa hunitambu kama mtoto wako nashukuru ila ungejiuliza swali moja huyo mkeo angekuwa mama yetu na kweli nimekutukana angekwambia navyojua angekuwa amekutukana mwanae kama mnavyodai asingekwambia angemkalisha chini mwanae na kumkanya ila kwakuwa mimi sio wa kwake lazima atafanya anavyoona ni sawa kwake. Nakushukuru sana baba ila mimi nishazoea kuishi bila wazazi tangu nipo mdogo hivyo sioni ajabu kwangu.
Baba hakunijibu. Tulikaa karibia miezi sita pasipo kuwasiliana na baba nikaamua kuishi ulimwengu wangu kama alivyosema Joy. Nikienda Morogoro naishia kwa Dav labda na kwa mama yake Dav na kurudi zangu Dar. Baba alikuja kunitafuta kunipa taarifa kuwa yeye na mke wake wamepata mtoto mwingine wa kike. Ndio ukawa mwanzo mpya wa mimi kuwasiliana na baba. Ila sasa mimi ndio mtoto kipenzi cha baba hakifanyiki chochote bila kunishirikisha. Haijalishi nimepitia nini bado nampenda sana baba yangu.
Nawatakia weekend njema. Niko na mafua yananitesa kweli naona yananiletea homa. Nikipata nafuu nitarudi kuendelea. Asanteni!
Mbona hukumrudia Omar...?!sio pastor naomba nieleweke. nimesema mtumishi wa Mungu. kuna aina nyingi ya watumishi. labda ni mwimbaji, au mwinjilist au shemasi au vinginevyo. Achana nae huyo. sio kwamba nimeandika kila kitu mpenzi. nimeelezea tu kwa ufupi.
Aisee, pole sanaaEp 20
Baada ya kurudi Dar. Sikutaka kuwasiliana kabisa na Dav. Lakini mama yake tunawasiliana. Yaani nimeanza kuchoka vitimbwi vya Dav tumekaa miezi sita nikamsamehe tena. Baada ya kumsamehe alitoa mahali na kunivisha pete ya uchumba.
Taratibu za ndoa zimeanza taratibu kipindi hiki Dav anaonekana kutulia kidogo. Lakini ukiwa naye simu yake hana uhuru nayo mara azime mara aweke flight mode. Kuna wakati unampigia simu Dav anapokea mwanamke yaani sio Dav yule wa mwanzo huyu ni Dav mpya kabisa.
Ujenzi umeisha Dav inabidi ahamie kwake mama Dav akanipigia simu kuwa siku ya kuhama inabidi niwepo ili tusaidiane kupanga vitu. Sababu kama kujuana mnajuana kwahiyo jitahidi siku ya kuhamia uwepo sababu kutakuwepo na ibada na tafrija fupi. Kweli siku ya kuhamia nilikuwepo. Tumehamisha vitu na na wamefanya ibada pale ndugu zake Dav walikuwepo mimi alikuja tu rafiki yangu Jack.
Baada ya kuhamia familia zote mbili inabidi zikutane sasa ili mipango ya harusi ianze. Tofauti na kufanya kazi za kuajiliwa kwa watu na mimi nilikuwa na kibanda changu cha chips Mwenge hivyo lazima na mimi niweke utaratibu wa kuangalia biashara zangu zinavyoenda.
Nimerudi Dar naendelea na kazi zangu kama kawaida tukapata kazi ya tenda Morogoro kwahiyo inabidi nisafiri kwenda Morogoro kikazi. Lakini sikumwambia Dav kama naenda Morogoro. Nimefika zangu Morogoro tulifikia hotelini na boss wangu na wafanyakazi wenzangu. Tumekaa siku mbili baada ya kumaliza shughuli zetu tunatakiwa kurudi dar. Mimi nilikataa kurudi nao nikawaambia watangulie mimi naenda nyumbani kwanza kusalimia.
Lengo si kwenda kwa baba tangu aondoke auntie nyumbani siendi mara kwa mara nia yangu ilikuwa kwenda kwa Dav kumfanyia surprise sababu ilikuwa jumapili nilikuwa na uhakika kuwa Dav atakuwepo nyumbani. Na kabla sijaenda nilimpigia kuumuliza yupo wapi akanambia yupo nyumbani na mimi sikutaka kumwambia kuwa nipo Morogoro. Basi nikachukua zangu bodaboda kutoka Morogor mjini mpaka nimefika getini nimemlipa boda. Geti limeegeshwa kidogo mimi Lisa huyo ndani.
Mlango wa kuingilia ndani ulikuwa umefungwa nikanyonga zangu kitasa nikaingia zangu ndani. Nailaani sana siku hii sikuamini nilichokiona. Nilimkuta Dav amekaa kwenye sofa kifua wazi, amevaa pensi tu miguuni kwake amejaa yule dada aliyempikiaga chakula kipindi anaishi kwenye nyumba ya kupanga na dada yule alikuwa kajaaliwa jamani amejifunga kanga moja amemlalia Dav.
Sikujua kilichotokea baadae nilikuja kujikuta hospitali mama Dav yupo pembeni yake. Nililia sana siku hiyo nahisi hata msiba sijawahi kulia hivyo. Mama alinizuia nisiongee chochote mpaka nitakapokuwa sawa. Nikaendelea vizuri nikaruhusiwa kutoka hospitali nikapelekwa kwa mama yake Dav na sikutaka kuongea chochote niligeuka bubu si kwamba siwezi kuonge ila sihitaji kuongea chochote wala kuongea na yeyote yaani kwa ufupi nikawa kama zezeta. Baba alikuja kunichukua kwa mama Dav na kunipeleka nyumbani kwake. Pale pia sina amani make mimi na mama yetu wa kufikia hatupo sawa. Nikamwomba baba ruhusa nirudi Dar nikajitahidi asione kama nipo mnyonge. Baba akaniruhusu na kunipa dogo anaisindikize. Kumbuka dogo Dav kapita lakini nitamwambiaje baba uchafu huu. Nikakubali nilivyofika Dar tu baada ya siku mbili nikamwambia dogo arudi moro nisijekumzuru na nikamwambia uking’ang’ania kukaa hapa eti unanipa huduma nitamwambia baba kuwa na wewe umetembea na Dav na Ushahidi ninao. Dogo kusikia hivyo alikubali kuondoka.
Nikaanza kunywa tena viloba nikaacha kwenda kazini yaani nipo nipo tu. Tunaweza kuwa nimekaa na watu tunaongea kawaida ghafla naanza kupiga kelele yaani kwa ufupi nilikuwa chizi fresh kuna muda nakuwa sawa kuna muda zinahama. Jack rafiki yangu alikuja akanichukua na kunipeleka kwake akawa ananipa ushauri. Akanianzishia uji wa lishe yaani na afya yangu ilidorora sana. Nilivyokaa kwa jack nikaona afya yangu inaimarika nikarudi kule nilipokuwa nimepanga nikachukua vitu vyangu na kuhamia sehemu nyingine na kazi nikaacha lengo nikutoka katika sehemu ambayo Dav anaweza kunipata. Nikabadilisha line ya simu na nikamtoa Dav kabisa kwenye Maisha yangu. Familia yangu akiwemo mama yake Dav walijitahidi sana kunisihi lakini nilikataa nikaamua kuishi ulimwengu wangu. Kama sikujiua kipindi hicho hata itokee nini siwezi kuchukua Maisha yangu.
Nikirudi nitaandika nitajitahidi kusumarize ili tumalizane na hili nishachoka. Muwe na siku njema.
😂😂Noo aiseeau wewe ndo Dav
Mama mchunga , inabidi tufanye jambo kuwaunganisha😁😁😁😁Baba mchunga katika ubora wako🤣🤣🤣🤣
inauma sana ila ndio maisha fikria mtu una hamu kumuona unafikria ukimwona utakapomwona utamkumbatia kwa furaha lakini inakuwa tofauti. ila sasa hivi nishajionea sawa. namshukuru Mungu alinipa nafasi ya kumwona mama yangu kwa sura na bado naweza kumuona tofauti na wale wanaopoteza wazazi wao wakiwa wadogo. mama zao wanaishia kuona picha au kuadithiwa alikuwa hivi alikuwa vile. lakini mimi Mungu amanipa upendeleo wa kumuona japo hana mapenzi na mimi namshukuru sana Mungu kwa hilo tu.Pole sana Dadakidoti
Kwa changamoto ulizopitia
Sijui kwann chozi limenitoka
Sijawahi kuona mama anakana watoto wake huyo si mma ni shetani
jaman omary hapana naye hakuwa mtu sahihi kwanguMbona hukumrudia Omar...?!
hilo ndo la muhimu mpenziEndelea kusaka pesa bibie