Ep 17
Mapicha picha yameanza nyumbani. Ukienda kama baba hayupo kulala njaa ni kawaida tena mama yetu wa kamboa haoni aibu kukwambia kuwa kuwa leo hatujapika mwanangu huku hakijichekesha hivyo sisi na wadogo zako tumeshakula vitumbua, au maandazi hivyo wewe nawe fanya mpango wako wa kula sisi tumeshashiba. Yaani nyumbani pamebadilika sio mimi sio Joy anayeenda pale asikumbuke uwepo wa Auntie.
Kuna siku nimeenda mororogoro tulikuwa na safari yetu mimi Dav tulikuwa tunaenda Arusha Vacation nikaamua kupitia nyumbani kuwa salimia siku moja kabla ya safari. Chumba changu kimejaa vitu vya auntie, kuanzia nguo zake na makabati yake huwezi kulala mule kwa ufupi kimegeuka stoo ya vitu vya auntie.
Joy mazoea hataki kabisa chumba chake kimefungwa na funguo anazo mwenyewe. Chumba cha wageni kuna ndugu yetu mtoto wa shangazi amefikia pale kutoka kanda ya ziwa kufanya shughuli zake na kuondoka.
Nikaamua kulala chumbani kwa wadogo zangu. Morogoro hali ya hewa ni baridi kidogo tofauti na hali ya hewa ya Dar. Nikachukua gauni langu nimelala nimelivaa. Alfajiri kama saa kumi nastuka usingizini nakuta wenzangu wamelala chini. Nashangaa nimelowa mwili mzima. Mdogo wangu akaniuliza dada umelowa? Nikamwitikia ndio akaguna kwanza pia akasema pole sana dada angu nitafanyaje sasa.
Sikumtilia maanani sana nikahisi labda mdogo wake atakuwa anakojoa kitandani japo ni bint mkubwa tu darasa la sita. nikaamka nikajiandaa na kubeba mizigo yangu na kwenda zangu kwa Dav kwa ajili ya safari. Nguo zangu zilizolowa nikaziweka kwenye mfuko. Nimefika kwa Dav tunaenda kwa mama kwanza kumsalimia safari yetu ni kesho yake. Jioni tumerudi kutoka kwa mama yake Dav ndo nakumbuka nguo nilizoziweka kwenye mfuko. Nikazifuata kwa lengo la kuzifua nikihisi ni mikojo tu lakini ajabu ngu hazinuki hata mkojo na yule bint ana miaka kama 14 mpaka 15 hivi na mkojo wa mtu mzima unavyonuka. Ndio nikagundua kuwa watakuwa walinimwagia maji.
Siku zimeenda namuona mdogo wetu ambaye ni mtoto wa baba na mdogo wake ambaye ni mtoto wa mama yake aliyemza huko kwingine Watoto wameanza dharau siwaelewi. Pale lazima niende kwa sababu ni kwa baba yetu. Joy akienda lazima atatoka kule wamegombana hatuna ukaribu sana na Joy lakini changamoto tunazokutana nazo kwa baba tunaambiana.
Joy ni mkorofi sana hivyo ukitokea umemchokoza unakuwa umewasha moto. Kuna kipindi cha likizo Joy alienda kukaa kule kwa ajili ya likizo yake. Yaani kulikuwa pa moto sana. Ilifika hatua Joy akawa anapika chakula chake na wao wanapika chukula chao. Yaani ni fujo tu. Kuna siku baba alinipigia simu kuhusu Joy anavyokuwa hana adabu na ametaka kuwakalisha kikao Joy kakataa kasema mpaka mama yake au antie mmojawapo awe kwenye hicho kikao ndio atakubali kukaa kikao. Na anajua kuwa haiwezekani ili mradi tu fujo.
Mama mdogo (mama wa kambo) ananigombanisha na baba yangu
Siku zimeenda sana nimemkumbuka baba yangu naamua kumpigia simu. Nilipiga sana simu inaita tu haipokelewei, nikawa na wasiwasi juu yake. Nilikaa muda kidogo nikaamua kupiga tena.
Simu ilipokelewa na mama yetu wa kufikia. Hakunisalimia anaongea kwa jeuri unapiga simu sana wewe na ukiona simu yako haipokelewei jua mwenye simu hayupo. Hiyo kauli ilinikera nilikuwa sijawahi kumjibu ila siku hiyo nilimjibu na mimi nilikuwa sikupigii wewe nilikuwa nampigia baba yangu. Akanambia huyo ni mume wangu
Namimi ni baba yetu tena mama yetu ulimkuta na alikuwa amefunga ndoa na baba yangu tena ya kanisani si kama yakwako ya bomani na umetukuta hivyo tuheshimu ili na sisi tukuheshimu. Pia usisahau mama yetu alichumbiwa na kutolewa mahali.
Sikutaka kusikia neno lingine kutoka kwake.
Kumbe nilipokata simu akaanza kujiliza na kuanza kusema kuwa nimemtukana nasikia baba alivyorudi alimwambia kuwa nimemtukana na kumuita baa med kuwa yeye na baba wote ni wahuni tu kwani walikutana bar na maneno mengine mengi. Hayo aliniadithia Joy sababu kipindi hicho alikuwa Morogoro akiwachachafya na fujo zake.
Nimekaa kama wiki moja tena nikampigia baba yangu simu lakini akawa hapokei namtumia ujumbe hajibu. Nikaamua kuwapigia ndugu zake na kuuliza kama kuna tatizo wakanambia kuwa baba aliwapigia na kuwaeleza kuwa nilimtukana hivyo hanitambui tena kama mtoto wake.
Nilivyoambiwa vile nikamtumia baba ujumbe na kumwambia. Asante baba unawaambia watu kuwa nimekutakana wewe na mke wako na kuwa hunitambu kama mtoto wako nashukuru ila ungejiuliza swali moja huyo mkeo angekuwa mama yetu na kweli nimekutukana angekwambia navyojua angekuwa amekutukana mwanae kama mnavyodai asingekwambia angemkalisha chini mwanae na kumkanya ila kwakuwa mimi sio wa kwake lazima atafanya anavyoona ni sawa kwake. Nakushukuru sana baba ila mimi nishazoea kuishi bila wazazi tangu nipo mdogo hivyo sioni ajabu kwangu.
Baba hakunijibu. Tulikaa karibia miezi sita pasipo kuwasiliana na baba nikaamua kuishi ulimwengu wangu kama alivyosema Joy. Nikienda Morogoro naishia kwa Dav labda na kwa mama yake Dav na kurudi zangu Dar. Baba alikuja kunitafuta kunipa taarifa kuwa yeye na mke wake wamepata mtoto mwingine wa kike. Ndio ukawa mwanzo mpya wa mimi kuwasiliana na baba. Ila sasa mimi ndio mtoto kipenzi cha baba hakifanyiki chochote bila kunishirikisha. Haijalishi nimepitia nini bado nampenda sana baba yangu.
Nawatakia weekend njema. Niko na mafua yananitesa kweli naona yananiletea homa. Nikipata nafuu nitarudi kuendelea. Asanteni!