Kuna wengine hatujui tulipokosea

🔥
 
EP 2

Mimi na familia yangu upande wa baba tunaenda msibani, japo Watoto wao walikuwa wameachana zile familia zilikuwa karibu sana na walikuwa wanashirikiana kwa vitu vingi. Kama mjuavyo vijijini ni wakalimu sana hasa hasa wazee wa zamani.

Tunafika msibani watu wanaendelea na maombolezo kama kawaida. Taratibu za kuleta mwili kijijini zinaendelea. Baada ya siku kama mbili mwili umefika kijijini.

Nakutana na mama yangu kwa mara ya kwanza

Baada ya mwili kufika watu wametulia bibi mzaa mama ananiita ndani anaanza kunitambulisha kwa mama wadogo ambao nilikuwa siwafahamu ananitambulisha kwa mama aisee ni binti mzuri sana kwa sura vidimboz mashavuni amenipatia pia ila yeye hana kidoti yaani tumefanana yaani copy and paste. (nahisi kwa wakati huo alikuwa na miaka kama 30 - 32) ila ajabu hakuna anayefurahia kumwona mwenzake si mama wala si mtoto. Kwa kuambiwa aliniacha nikiwa na miaka miwili alikuwa na mimba ya mdogo wangu ambaye pia hatuna mazoea wala hakuna upendo kati yetu. Nakumbatiana na mama zangu wadogo yeye tunaishia kutizamana tu. Yaani ile kitu ya mama na mwana hakuna kabisa.

Tumezika msiba umeisha tumeanua matanga nimerudi kwetu kuendelea na masomo yangu kama kawaida. Wakina mama mdogo wamekuja kwetu kuniona na kunipa zawadi na kuniaga kuwa wanarudi Dar kuendelea na Maisha lakini ajabu mama yangu hawakuja nae.

Nimehitimu darasa lasaba tulikuwa wanafunzi 60 kwa mwaka wetu tumechaguliwa watatu tu kujiunga na na elimu ya sekondari.

Naanza kidato cha kwanza ni mbali natembea umbali wa kilomita kama k.m 3.3 hivi kutoka nyumbani mpaka shule make ni kata nyingine kabisa na kata yetu make kwenye kata yetu kipindi hicho walikuwa hawajajenga shule ya sekondari.

Nasoma kwa shida ya sana shuleni ni mballi kukaa miezi mitatu shuleni kwetu bila mwalimu wa kipindi Fulani ni kawaida tu. Kila siku tunachelewa kufika shuleni na kufika nyumbani usiku ilikuwa kawaida tu.

Nakutana na mbwa mwitu wakati naenda shule

Ilikuwa kama saa mbili hivi jua la asubuhi limecshochomoza nimechelewa wenzangu wameniacha hivyo nipo peke yangu naenda shule. Napita katika ya miti sijui kishwahili chake siju niite vipori vidogogo vidogo sijui niite tumsitu.

Njia tunayopita hamna makazi ya watu ni miti, mito na mashamba tu. Ghafla naona mbwa mwitu kama kumi wanakimbia tu. Niliganda kama kisiki sikukimbia wala kupiga kelele ni kama kuna mtu aliniziba mdomo wale mbwa mwitu walinipita pasipo na shaka hawakuniona wakaondoka zao. Baadae kidogo ndo akili inanijia nami nakula mbio mpaka shule. Nafika shule nakutana na mwalimu mnoko huyo ananiuliza kwanini nimechelewa namwelezea yaliyonikuta lakini hajanielewa na akanitembeze viboko vya kutosha na adhabu juu.

Mungu ni mwema tumefanya mtihani wa kuingia kidato cha tatu nafaulu na kuingia kidato cha nne na hatimae namaliza kidato cha nne matokeo yanatoka bahati haikuwa upande wangu naambulia Four ya 31.

Maisha yanaendelea pale kijijini sikuwa binti wa mambo mengi nilikuwa mpole sana mwenye adabu, mpole pia sikuwa na makundi. watu wengi walikuwa wananipenda sana. Kama wakati ungekuwa unarudi nyumba ningerudisha wakati huu.

Nitarudi.
 
Asante mrembo,Leta habari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…