Wagumu Tunadumu
JF-Expert Member
- Dec 10, 2022
- 5,276
- 17,354
Nazan umeona hayo manenoasante mwalimu
Nafaulu
Namaliza
Naambulia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nazan umeona hayo manenoasante mwalimu
sijakataa mimi nimesoma shule za st. kayumba hivyo penye mapungufu tuvumiliane kikubwa kufikisha ujumbe. asante sana.Nazan umeona hayo maneno
Nafaulu
Namaliza
Naambulia
Ni monetary doctor...... Chogo unautaka eehMastori ya kutunga haya chai tupu
Andika stori kamili tupate UHONDRROOO
Cc: Lamomy Labella Extrovert MONEY doctor Poor Brain
Naona bro unajitahidi kushusha nyavu 😹😹Hii ep 2 hapo mwsho mwsho umekipiga kabisa chenyew kisukuma ingawaje unasema wew sio msukuma
Wivu wa kukutana na mbwa mwitu au wa kutembea km 3 kwenda shule?? 😹😹acha wivu
Badala ya kuandika 'maana yake' yeye anafupisha tu 'make'"Make" ndo nini?
Utamuweza Mnyamwezi huyu?Lissa km haujaolewa nakuja Pm unisimulie naona wivu sitaki kushare, nataka live peke angu.. Km umeolewa kwaheri hii hadithi yako sisomi Tena endelea na mashabiki zako.
KabisaYa kweli ya kutunga!Kama ya kweli tiririka mfululizo.
Dah! Omary anaenda kula tunda kimasihara! 🤨🤨Kuna rafiki yangu huyu kipenzi tumwite Hawa si jina halisi tunafanya wote kazi na umri wetu hatujatofautiana sana tunaambiza visiri vyetu vya kitoto.
Kuna jamaa tumwite Omary si jina lake sasa huyu jamaa tumemkuta pale kazini ni handsome anajua kuvaa akipita ananukia ana bezi kama ya Jaiva nae alikuwa kati ya wale wanaoniwinda. Kimoyomoyo nikasema potelea mbali maneno ya dada nitamkubali Omary nampenda sana.
hajala amemuoa hawa ndoa ya serikalini. nimeweka mipaka kati ya yao na mimi sitaki mazoea ila bila shaka tutakutana tu. sisi ni people tutaonana.Dah! Omary anaenda kula tunda kimasihara! Tena atauzwa na Hawa 🤨🤨
sIo kwel,mim k za mitandaoni hata siwez,wamtaan wananitoshaNaona bro unajitahidi kushusha nyavu 😹😹
Mimi ndio Omary, umenikera sana kutomalizia..Epi 3
Mwaka umepinduka bibi mzaa mama na babu na bibi wanapambana kuhakikisha naendelea na masomo wananitafutia chuo wanakuta nafasi zimeisha naambiwa kuwa tusubiri mpaka mwakani.
Si baba wala mama anayetoa ushirikiano wao wako bize na Maisha yao wanaoangaika ni babu na bibi tu pande zote mbili.
Wakati chuo ambacho walikuwa wameki- target wamesema tusubiri hivyo nikawa nipo tu kijijini.
Sina hili wala lile nipo na bibi tunapiga stori anapokea simu na kunipa simu na kunambia Lisa simu yako. Napokea simu kumbe ni dada yangu mtoto wa baba yangu mkubwa anayeishi mjini ananiambia kuna kazi kwenye kampuni yao anakofanya kazi wakati naendelea kusubiri kwenda shule ningeenda kujishisha pale ili nisikae bila kazi. Basi dada yangu akanitumia nauli kesho yake asubuhi nikaenda mjini na keso yake naanza kazi pale kama kibarua. Tunalipwa sh 4,000 kwa siku ila wanalipa kila mwisho wa wiki nakakubali make kwa kipindi hicho ilikuwa kubwa kumbuka sina majukuma nakula bure nalala bure kwa dada yangu.
Nimezoea kazi sasa na haikuwa kazi ngumu Lisa nimenenepa ghafla kama nimelkula hamira nimependeza yaani Lisa, Lisa kweli nina rangi ya choklate si mfupi si mrefu, nina jicho la kusinzia, vidimpo vya uchokozi na kidoti changu kwenye paji la uso. Lisa si haba wanaume wanaanza kujipendekeza kuanzia kazini kwetu mpaka mtaani. Naletewa zawadi kila iitwapo leo kidogo mji umenchangamsha nimekuwa muongeja japo dada yangu ni mpole.
Dada ananipa somo.
Sikia mdogo wangu Lisa usije ukajiloga ukaanzisha mahusiano na wanaume wa pale kazini. Utafukuzwa kazi na ukifukuzwa kazi hupo tayari kurudi kijijini?
Dada Hapana sitaki kurudi kijijini nakuahidi sitakuwa na mahusiano yoyote pale kazini nataka nitafute hela niwe kama wewe dada yangu.
Dada yangu ni fundi cherehani akitoka kazini huwa anashona nguo hiyo ni kazi yake ya ziada. Sasa dada oda ni nyingi kutoka kazini kwetu na wateja wengi ni wanaume. Jumamosi na jumapili watu hawakatiki nyumbani kwa dada. Wanalete nguo awashonee lakini wengi wao ni kuniwinda Lisa. Maneno ya dada yanatembea kwenye akili yangu sitaki kuwa na mahusiano na wanaume wa kazini. Hivyo nikawa nawatolea nje.
Wengine wakawa wanazusha wenyewe kuwa wana mahusiano na mimi wakati sio kweli. Kumbe hata supervisor wetu alikuwa ananitaka ila hajaniambia tukiwa kazini ananiuliza kama natoka soda nikikubali tunanunuliwa staff nzima. Nikikataa watu hawanywi soda. Baadhi ya watu wakadhani natoka nae maneno mpaka yakamfikia dada yangu ambaye tulikuwa vitengo tofauti. Na kila kitengo walikuwa na ofisi yao. Kwa hiyo mimi na dada tulikuwa tunaachana getini tu.
Dada akaniuliza nikamwambia kuwa siwezi kuvunja ahadi yangu kwakohata siku moja.
Kuna dada mmoja kumbe anatoka na supervior staff mwenzangu mtu mzima kidogo, nikimwamkia haitikiii, kumbe kadaivet simu yangu ili ajue huwa tunaongea nini mimi na supervisor.
Weekend dada hayupo ananipigia kunipa maagizo ya nyumbani simu yangu haipo hewani anapokea Ana (aliyedaivet simu yangu) dada anagundua kuwa simu yangu imedaivetiwa. Jumatatu tunaenda kazini dada yangu aliikuwa anafanya kazi upande wa utawala Ana anaitwa na kupewa onyo kali na uongozi. Tukio hilo likanifanya niendelee kuwa maarufu pale kazini.
Kuna rafiki yangu huyu kipenzi tumwite Hawa si jina halisi tunafanya wote kazi na umri wetu hatujatofautiana sana tunaambiza visiri vyetu vya kitoto.
Kuna jamaa tumwite Omary si jina lake sasa huyu jamaa tumemkuta pale kazini ni handsome anajua kuvaa akipita ananukia ana bezi kama ya Jaiva nae alikuwa kati ya wale wanaoniwinda. Kimoyomoyo nikasema potelea mbali maneno ya dada nitamkubali Omary nampenda sana.
Nikaona nimshirikishe shoga yangu Hawa. Kumbe Hawa ni mjanja keshapiga hatua moja mbele zaidi yangu kumbuka yeye amekulia mjini mimi ni wakuja tu.
Natarudi. mimi ni mvivu sana kesho nitajitahidi kumalizia jamani
niliemkwaza anisamehe
Ungebaki kazini jamani🥲Ep 5
Nakata tiketi ya kwenda Morogoro, naaga pale kazini kwa mbwembwe kuwa naenda kusoma. Utawala wananisihi sana nisiondoke kwani nipo kwenye orodha ya wafanyakazi wanaokaribia kupata ajira ya kudumu. Dada amenisihi sana lakini nimewagomea naikukumbuka sana nafasi hii.. Inabidi nirudi Kijiji kuaga na kujiandaa kwa ajili ya safari.
Nimefika kijijini babu na bibi wanalipokea vyema jambo la mimi kurudi shule lakini upande wa bibi mzaa mama inakuwa tofauti inakuja barua kwa babu ya kuzuia mimi nisiende Morogoro. Barua inaeleza Kwa sababu zifuatazo:-
Na nyingine kibao ila hizi zilikuwa zimetiliwa mkazo. Barua hii iliandikwa na mjomba kutoka upande wa mama naikukumbuka sana barua hii. Hapa ndo unapojidhiirisha msemo wa mdharau mwiba mguu huota tende.
- Kuwa baba hana kazi maalumu ya kumuingizia kipato ni misheni town tu.
- Baba hana mke hivyo mimi kama mtoto wa kike nani atakayeniangalia?
- Baba hana nyumba ya kuishi.
Napokea simu kutoka kwa mama ni miaka sita imepita tangu tulivyoonana kwenye msiba hatujawahi kuonana tena ananipigia simu na kunambia nisiende Morogoro kwa baba atatuma nauli nimpe muda tu ili niende Dar. Nae namkatalia babu nae anajaribu kunishawishi lakini wapi.
Natishia kujiua kuwa hakuna wa kunizuia kwenda kwa baba yangu labda kifo tu. (wazazi wawekeni wazi Watoto wenu.) nampigia baba simu na kumwambia kuwa wanajaribu kunizuia nisije huko wanadai kuwa huna nyumba, huna mke, huna kazi utanitunzaje? Baba ananijibu kama nimekuzaa mwanangu nitashindwaje kukutunza. Alokwambia sina nyumba nani achana nao mwanangu wewe siku ya safari ikifika panda bus njoo mimi ni baba yako.
Naongea na babu ananiruhusu ila ananiambia nikikuta Maisha ni magumu nimpigie simu anitumie nauli nirudi kanda ya ziwa. Tunakubaliana siku ya safari inafika napanda bus kuja zangu Morogoro huku nikifurahi kuja kuishi na baba yangu na kuwaona wadogo zangu ambao nawasikika kwa majina tu.
Nipo kwenye bus Kidoti mie naenda Morogoro. Tumefika Dodoma kwenye siti ya pembeni abilia mwenzangu ameshuka na anapanda kijana mdogo tu age mate wangu anatoka zake Dodoma anakuja Dar ndo makazi yake. Tunasalimiana anajitambulisha kuwa anaitwa Dev si jina lake. Kijana huyu anakula hovyo. Ananunua vitu anakula kama mwendawazimu yaani kama kero tunakaribia Gairo Dev anaumwa tumbo nampa pain killer nilikuwa nazo. Dev anakaa sawa tunaanza stori za hapa na pale tunabadilishana namba wote tunashuka Morogoro tulifika usiku. Ananisubiri mpaka wenyeji wanapokuja kunihchukua naye aendelee na safari zake. Kumbe yeye anaishi Morogoro wote tunaenda Morogoro mjini tofauti mitaa tu japo si Jirani.
Ajabu anaekuja kunipokea msamvu sio baba yangu mzazi ni baba yangu mkubwa kaka yake na baba. Ananiambia kuwa baba yangu kasafiri kikazi yupo tanga akirudi atanikuta kwake. Nakubali nitafanyaje sasa na wakati mji huo sio mwenyeji na baba yangu.
ya kulalia tukutane kesho. nawapenda
Wakishua wa kijijini unawaju??Dah, wa kishua halafu kwenda shule unakutana na mbwa mwitu 10?
Nwei tuendelee kustorika