Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Ukishusha episode Usiache kunitag mkuu.asante
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukishusha episode Usiache kunitag mkuu.asante
Umeolewa au una mchumba?karibu kwa swali nipo hapa
jamani sina, mume saina mchumba wala sina mpenzi niko single naenjoyUmeolewa au una mchumba?
tayariUkishusha episode Usiache kunitag mkuu.
Nakusubiri sana dada kidoti tuenndelee maana unagusa hisia zangu.mh.Nimesoma kisa cha patrickk na bado nafuatilia wakati tukiendelea kumsubiria naomba nami nishare na nyinyi historia ya maisha yangu kwa ufupi. nia visa humu ni kujifunza, kushauriana na kutiana moyo. Karibu.
Kwa jina naitwa Lisa (sio jina halisi) natokea katika mmoja wa mikoa ya kanda ya ziwa.
Nilipoanza kujitambua kuwa mimi ni nani nilikuwa nikiishi kijijini kwa babu na bibi wazaa baba. Wazazi wangu hawakuwa pale walikuwa mjini. Jinsi navyoeendelea kukua ndo nagundua kuwa hawapo pamoja wametalikiana. Mama yupo na Maisha yake na baba pia yupo na mke mwingine na wana Watoto.
Niliendelea kukua nikapelekwa shule ya msingi huko kijijini. Nikaendelea na masomo yangu kama kawaida darasani nilikuwa na akili sana hali iliyonipelekea kuwa kipenzi cha walimu. Mpaka nafika darasa la nne nilikuwa sijawahi kuziona sura za wazazi wangu wala wadogo zangu ambao nawasikia kwa majina tu.
Nakumbuka nilikuwa nje tupo likizo tunajiaanda kuingia darasa la tano nilikuwa nje naosha vyombo mara wakaja watu wa baiskeli ndo tuseme walikuwa ndo bodaboda wa kipindi kile. Na mizigo mabegi ya kutosha na mmababa mmoja hivi nikamwamkia akaniangalia sana akaanza kulia sasa mimi nashangaa huyu mbaba analia nini sasa wakati naendelea na kazi yangu ya kuosha vyombo mara bibi akatokea akamkumbatia huku akitaja jina lake mwanangu umekuja nae akaanza kulia. Ndo nikagundua kuwa kumbe huyu ndo baba yangu.
Bibi akanigeukia Lisa mwamkie baba yako aisee nilisikia kitu kama kinanikaba nikatengeneza chuki kubwa kati yangu na baba yangu najiuliza siku zote hizi alikuwa wapi. Nikamjibu bibi nimeshamwamkia ilikuwa mchaba kama saa sita hivi. Basi bibi na baba wakaingia ndani na mizigo ikaingizwa ndani mimi hata sikuwashobokea nikaendelea na kazi zangu bibi akaniita nami niingie ndani nikamgomea. Nilikasirika sana. Muda wa chakula ukafika bibi akaanda chakula huku anaimba nyimbo kuonyesha alivyofurahi kumwona mwanae. Wakapakua chakula nikagoma kula na baba nikamwambia bibi siwezi kukaa sehemu moja na huyu mbaba wao wanalia mimi nina hasira tu.
Babu wakati huo hakuwepo alikuwa amesafiri kikazi ameenda mjini make alikuwa na wadhifa kidogo serikalini. Jioni babu anarudi make babu alikuwa ananidekeza sana nilivyomuuona tu nikamkibilia na kumkumbatia namwambia kuwa kuna mbaba yupo ndani yupo na bibi wanajiliza wanadai ni baba yangu. Babu nakumbuka alinituliza na vijizawadi vya mjini. Ndo nikakubali kuingia ndani.
Baba alikaa kijijini kama wiki mbili hivi na alikuja na zawadi kibao kwa ajili yangu. Na kila akitaka kwenda sehemu ananibembeleza tunaenda wote. Hali hiyo ilipelekea kuanza kidogo kidogo kumzoea na kuamini kuwa ni baba yangu. Wakati wa kurudi kwenye kutafuta nakumbuka nilimsindikiza na mpaka mjini nililia sana kuona anaondoka na kuniacha alimbembeleza sana akiahidi kurudi kunichukua. Nikamkubalia akaondoka huku mapenzi ya mtoto yakazaliwa mpaka leo nampenda sana baba yangu hunambii kitu kwake.
Maisha yakaendelea kama kawaida kwa babu, tulikuwa tunaishi Maisha mazuri tu ya kawaida ila sio magumu sababu babu yangu kidogo alikuwa anajiweza yaani kwa ufupi pale kijijini tulikuwa wakishua.
Upande wa mama kwao napo sio mbali na pale kijijini kwetu nikijiji cha Jirani tu hivyo nilikuwa nikienda mara kwa mara kuwasalimia babu na bibi pia japo pia mama yangu nilikuwa simfahamu.
Nilikuwa darasa la sita sasa ukatokea msiba upande wa mama, mama mkubwa dada yake na mama alifariki alikuwa akiishi Dar es Salaam lakini nilikuwa namfahamu make akija Kijiji ilikuwa lazima aje nyumbani kwa babu mzaa mama kunisalimia na kuniletea zawadi za hapa na pale. Huyu nilikuwa namchukulia kama mama yangu. Mama alikuwa anaweza kuja kwao kutoka Dar na asije kwetu kuniona nitasikia tu mama yako alikuja na kuondoka hivyo moyoni mwangu hata hakuwepo. Ndugu upande wa mama niliwaona ni bibi, babu, mamamkubwa (aliyekufa) na mjomba make hao ndo walikuwa wakinijali na kuja kuniona mara kwa mara hivyo upendo wa mama sijawahi kuupata mpaka leo.
Endelea kuwa na mimi nitarudi.
Umesha cope na hizo Traumajamani sina, mume saina mchumba wala sina mpenzi niko single naenjoy
Musa Banzi akutafuteNisameheni kwa kuchelewa nilipata msiba hivyo uliniweka bize kidogo. karibu
Ep 9
Tupo kwa mama tumepewa chumba chetu. Namuuliza Joy mbona unanichukia mdogo wangu nimekukosea nini mbona hatujawahi kuwa karibu kusema labda nilikukosea pasipo kujua niambie nijue mdogo wangu hivi unajua huwa nakutaja mara ngapi au hujui huwa nakuwazia mara ngapi kukuona kumbuka tupo wawili tu kwa mama yetu inabidi tupandane.
Joy ananijibu Lisa usinichoshe sikupendi na kamwe sitawahi kukupenda uanalijua kosa lako wewe? Kosa lako ni kukaa mbali na mimi kipindi cha utoto wetu kuna muda unaonewa unatamani dada angekuwepo angenitetea ushawahi kunitetea nilipoonewa wewe japo mara moja tu. Hapana hukuwepo ndo maana nakuchukia Lisa najua sio kosa lako kuwa mbali na mimi ila kuhusu kupata upendo kutoka kwangu sahau wewe ni mkosi tu katika Maisha yako. Kama mama yako mwenyewe aliyekuzaa anakuchukia mimi nitakupendaje tena uache kiherehere. Kitu ambacho hukiju Lisa mimi naishi dunia ya peke yangu si wewe, si baba wala si huyu unayemuita mama yako yupo katika moyo wangu wote nyie ni wafu mmekufa!. Na sitaki usumbufu anapanda kitandani anaanza kuchezea simu yake mimi namtazama naanza kulia tu. Mama anakuja anauliza mbona mko hivyo kuna nini? Wote hakuna anaemjibu tunabaki kimya. Mama wala hajali anaondoka zake baki na shida zenu si hamaki kuongea anafunga mlango na kuondoka zake. Joy anacheka kwa jeuri ananiambia unamwona huyo unayemwita mama yako hajali kuhusu sisi bora wewe na baba kuliko huyu shetani unafikiri anfurahia uwepo wetu hapa? Amka kwenye ndoto zako Lisa ishi Maisha yako kama ninavyoishi mimi.
Maneno ya Joy yananiumiza sana sina la kuongea nabaki kuwa mpole. Mjomba anatuita anamua kutotoa out mimi na Joy ila mama anabaki nyumbani lakini anatupa onyo kali kuhusu utambulisho wetu kwake. Tunaondoka na mjomba anatupeleka mlimani city anatununulia vitu vingi sana anatupeleka sehemu kula anatuuliza utambulisho wetu kati yetu na mke wake na sisi tunamkana tunasema ni shangazi yetu anatuuliza maswali mengi ya mtego lakini tunayakwepa. Anasema nikikutazama wewe Lisa naiona taswira ya mke wangu kwako niambie ukweli mwanangu wewe ni nani. Kwa unyonge namkana tena mama “Hapana mjomba ni shangazi yang utu”. Mjomba anarudisha swali mbona ujio wenu namuona mke wangu hana furaha kabisa tofauti wanavyokujaga Watoto wengine wa ndugu zake.? Joy anajibu labda hajisikii vizuri kiafya ila sisi sio Watoto wako kamuulize vizuri yeye ana shida gani.
Tunarudi nyumbani na mjomba mama ana wasiwasi sana hata sisi tunaona kuwa amebadilika kesho yake asubuhi tunaamua kuondoka zetu mpaka mjomba anashangaa tunavyoondoka ghafla.
Tunaondoka zetu na mimi narudi kwa baba yangu mdogo akili imechoka kwa mawazo Maisha kwa bamdogo yanaanza sasa kash kash mpya.
Msichana wa kazi anaondolewa, mimi sasa ndo nachukua majukumu yake. Bora yeye alikuwa analipwa mimi ni sababu ya kula na kulala tu. Natukanwa mimi. Ila naamua kuvumilia. Watoto wao wakirudi wanapewa hela waende shopping ila mimi nitabaki tu mule mule getini siruhusiwi kwenda sehemu yoyote, labda kwenye kusali jumuiya na kanisani tu lakini Watoto wao wanaenda sinema wanaenda bich na vitu kama hivyo.
Nimeanza chuo. Asubuhi kabla sijaenda naamka napika chai nawanyoshea nguo zao za kazini. Na kama Watoto wapo rikizo nikiamka nimwagilie maua, nioshe vyombo niwapikie chai, niwatengenezee juice, niwapikie cha mchana ndo niende chuo na nguo za familia kuanzia baba mpaka Watoto nafua mimi na Watoto wao ni wakubwa tu wapo sekondari lakini hawafanyi kazi yoyote ya kusaidia nyumbani. Wao ni kucheza game, kujisomea na kuangalia tv tu. Jioni nikirudi nioshe vyombo tena, nipike cha usiku na kufanya usafi kwa ujumla. Nyumba ni kubwa kuja kufanya usafi ni kazi sana yaani usiku nalala kama mfu.siruhusiwi kuangalia tv hata kama sina kazi mimi makazi yangu ni chumbani kwangu au jikoni dining nitakaa muda wa kula tu. Yaani ni hakuna unafuu hata kidogo.
Siku moja ilikuwa siku ya kupita gari la takataka, nimejiegesha gari linapita sijasikia chocote wala tangazo la kutoa takataka nakuja kustuka baadae gari limeshaondoka kitambo nikaachana nalo naendelea na shughuli nyingine. Saa tano usiku babamdogo anarudi si akaona taka hazijamwagwa bwana weee! anaulizw kwanini hazijamwagwa namwmbia nilipitiwa na usingizi sikulisikia. Akanambia nichague moja kati au takataka ndo kimoja ndo kilale ndani. Nikamjibu baba mdogo nitalala nje make usiku huu sina pa kuzipeleka. Akajibu sawa nikachukua simu yangu natoka nje nikijua ataniita nirudi ndani kama masihala bwana ananisindikiza mpaka nje natoka nje ya geti huku nikisikiliza atanirudisha ndani aha wapi kumbe amekusudia geti lile linafungwa.
Bahati nzuri kwenye simu yangu kulikuwepo na salio nikaamua kumpigia baba yangu mkubwa mjeda huwa hawaelewani viruri na huyu baba yangu mdogo baba yao mmoja ila mama zao tofauti na mimi nikapita mulemule. Bamkubwa ananiuliza una shida gani namwelezea mwanzo mwisho akanambia toka tafuta bodaboda popote ukimpata nipigie nimpe maagizo. Nikaenda nikakutana na bodaboda nampigia bamkubwa akamwelekeza sehemu ya kunipeleka boda anamwambia gharama elfu 20 bamkubwa anasema sawa tunavyooenda tunawasiliana nae tukakutana nae amekuja na gari boda anapewa hela yake. Bamkubwa ananinulia chakula njiani kwenye gari mitusi mikubwa inamtoka anavyomtukana mdogo wake nikasema ehe kimewaka kumbe wajeda wako hivi.
Asubuhi tumeamka tunaendelea na shughuli za hapa na pale simu yangu inaita ni babamdogo sijapokea nampelekea kaka yake anapokea anavyoporomosha mitusi sasa. Ulitaka mtoto afanyeje unamlinganisha mtu ulieyemgeuza kikalagosi chako na taka? Tena mwanao babamkubwa amekasirika sana sisikii maneno ya upande wa pili.
Kinaitwa kikao anaulizwa kama amenishindwa aniachie wengine watanitunza anaomba msamaha anasingizia kuwa alikuwa amelewa naulizwa kama nimeridhika kurudi kwa bamdogo nakubali ila moyoni sina amani kabisa. Tunarudi kwa baba mdogo.
Njiani natukanwa nasimangwa kuwa mimi ni mzigo tu kwake, mama yangu yupo huko anakula starehe hana hata wazo juu yangu baba naye aliendekeza wanawake wakamfilisi. Nilinyamaza zangu kimya sababu naona kama nimeshaanza kuzoea masimango yake.
Mama mdogo anamnunulia mwanae mkubwa wa kike yupo kidato cha tatu simu kwa siri sababu baba yao hataki wawe na simu hivyo inakuwa ni siri. Siku zimeenda baba yake siku kamsikia anaongea na simu usiku wa manane chumbani kwake tunaamshwa wote anapigwa mpaka anaitoa simu anaulizwa kaipata wapi anajibu simu ni ya dada Lisa. Mama yake yupo, mdogo wake wa kiume yupo na wote tunajua simu ni yake lakini jumba bovu waniangushia mimi. Kuanzia mtumiaji wa simu na mnunuaji wote wanakiri kuwa simu ni yangu. Napigwa sana kwa makosa mawili kosa la kwanza kwanini nampa mdogo wangu simu wakati najua ni mwanafunzi? Naambiwa nina roho mbaya nataka kumwaribia mwanae Maisha. Kosa la pili simu ya gharama kama hii nimeipata wapi nimeanza michezo ya wanaume nikienda chuo nafanya na ujinga. Na kwanini simu hiyo naitumia kwa siri. Nimegeuka mbuzi wa kafara maskini mimi Lisa nilipigwa kama kibaka tena kwa kuchangiwa babamdogo na mke wake na manene ya kasfa juu..
Naomba unitume contacts zako pm tuangalie namna ya kuunganisha mioyo yetujamani sina, mume saina mchumba wala sina mpenzi niko single naenjoy
🤣🤣🤣Lissa km haujaolewa nakuja Pm unisimulie naona wivu sitaki kushare, nataka live peke angu.. Km umeolewa kwaheri hii hadithi yako sisomi Tena endelea na mashabiki zako.
🤣🤣Hapo pa kumuita mama shangazi..! umenikumbusha mama yangu alinambia nimuite mama mdogo by then alikuwa ameolewa kwngne ambako sio kwetu, huwa nikikumbuka wakati huu napatwa na PTSD...
Maisha ni Funzo kubwa sana daa pole dear.Nisameheni kwa kuchelewa nilipata msiba hivyo uliniweka bize kidogo. karibu