Dadakidoti
JF-Expert Member
- Jul 26, 2024
- 399
- 1,409
- Thread starter
- #361
au wewe ndo DavKweli aisee, nikiwa mkubwa sitaki niwe kama dev😂
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
au wewe ndo DavKweli aisee, nikiwa mkubwa sitaki niwe kama dev😂
ameshaniua bado kunizika tuTuko pamoja mpaka Dav akuue
sijui kwakweli.Nambie yupo zenji sehemu gani nikusaidie kumtafuta
Asante sana.Maskin pole sana Mungu atakupa mume mwema ataekufuta machozi yako🥺☹️😪 Dah! hivi inawezekana ikawa karma baba alivomtenda Auntie ndo na nyie binti zake hamjapata wanaume wema?? Mlilie sana Mungu na uwaombee msamaha wazazi naamini utapata mume mwema Lisa usikate tamaa, umepitia mitihani mingi
duh!Kiroho ni kuwa baada ya kutolewa mahali wewe ni mke halali kabisa wa Dav na kimila pia ukikutana na Hali kama hizo inabidi upambane kama mama mjengo na sio kukimbia.
Na kama humtaki tena inabidi urudishe mahali ili upate mwenza mwengine wa kufangamana na roho yako.
Poleee ila ukiwa na hamu ya kumtafuta nambiesijui kwakweli.
sawa asantePoleee ila ukiwa na hamu ya kumtafuta nambie
Ahsante sana kwq simulizi yako hii nzuriEp 21
Siku zilienda Dav hakuamini kama ningesema basi. Nilirudisha pete kwa mhuisika Dav hakuamini kama ningemwacha nilimwambia kuwa siku ukiona umebadilika na unaweza kuniheshimu japo kidogo na kutulia utanitafuta ila sio kwa sasa Dav nahitaji kupumzisha akili yangu sasa. Nikikaa sawa nitakwambia ila sidhani kama naweza kukusamehe. Hivi hatujaoana Dav huko hivi ukiniweka ndani ukajua tayari nipo chini ya himaya yako itakuwaje. Kinachoniuma mwanamke yuleyule toka umepanga mpaka umejenga kwako bado tunakosana kwa sababu yake. Kitanda kilekile ninachokilalaiaga mimi bora mgeenda sehemu nyingine si hapa. Au ningewakuta sehemu nyingine sio hapa kwako ningekusamehe kabisa. Au angekuwa mwanamke mwingine siku ile si ulikana ukasema ulikuwa unampa hela ili akupikie na hapa alikuja kukupikia tena sababu unampa hela? Dav alilia sana, alinipigia magoti lakini sikujali kilio chake wala magoti yake niliondoka zangu nikawaacha kwenye kikao na nikaazimia kumuondoa Dav kabisa Dav kweye Maisha yangu na nilifanikiwa kumuondoa mazima.
Mahusiano yangu na Dav yalidumu kwa miaka mitatu na miezi minne na kipindi chote hicho japo ilikuwa long distance relationship sikuwahi kumsaliti wala kuwaza kufanya hivyo mpaka tunaachana. Nikawa bize na Maisha yangu japo ilikuwa ngumu lakini mwisho wa siku niliamua kukubali matokeo.
Maisha yana pilika pilika nyingi sana. Kwenye heka heka za hapa na pale nikakutana na kijana mwingine mtanashati ni daktari katika hospitali kubwa hapa dar alinisumbua kwa kipindi cha mwaka na zaidi. Nilishamtoa Dav kwenye akili yangu nikaamua kuwa naye ila kumbe yule jamaa alikuwa ameoa na ana Watoto watatu familia yake inaishi mkoani lindi.
Nilivyogundua tu sikutaka kuangalia nyuma wala sina cha kupoteza kwake nikakimbia futi mia. Hakuna mtu namwogopa kama mume wa mtu. Maisha yalisonga nilikaa single miaka miwili yaani mtu akiniambia habari za mapenzi simwelewi kabisa hata kidogo. Nikaamua kujikita kwenye kazi zangu.
Nikaja nikakutana na huyu mpendwa namaanisha mlokele ni mtu maarufu kidogo nikaanza nae mahusiano nikiamini huyu ni mtumishi wa Mungu hawezi kunitenda. Msinilaaumu jamani Lisa nakula nashiba kuna siku tulijikuta tumevunja amri ya sita hata sielewi ilikuwaje. Mungu naye hakuwa mbali jamani mimba hiyo. Nikalea mimba yangu mpendwa yule naye kumbe ni silent killer ana matukio yake pia. nikaamua sasa kuwa bize na mimba yangu.
Namshukuru sana Mungu alinijalia handsome boy mwanangu ana miaka miwili sasa ananipa kila sababu ya kupambana. Sasa hivi nina amani na katoto kangu nikiwa single mother.
Kuhusu nyumba ya antie aliyokuwa anajenga niliimalizia na document zake ninazo mimi siku yoyote akitokea nipo tayari kumpa pasipo kudai chochote kile.
Dav alikuja kuoa mwanamke mwingine lakini walishindwana. Walikatana mpaka mapanga wakapelekana mpaka mahakamani. Dav siku hizi ni chapombe ana midevu kama osama yaani usmat ule hana tena nilikutana mwaka juzi nilivyooenda kumsalimia baba tulikutana mjini bahati mbaya nikiwa na kichanga aliumia sana. Kuna siku huwa anamfuata baba yangu na kuanza kumsumbua baba kuwa mimi nimke wake anamtaka mke wake nilimwambia baba ampeleke polisi. Ila baba hataki anampenda Dav ila mimi nilishakula viapo na viapo siwezi kurudi tena kwa Dav. Simchukii nilishamsamehe kabisa ila pia simpendi namchukulia kama mtu wa kawaida tu.
Mama naye yupo south Africa kuna kipindi aliumwa sana alipata ajali akateguka mguu akawa anahitaji msaada wetu ndugu zake wakatwambia kuwa twende kumuuguza tukagoma sio mimi sio Joy alikubali kwenda south Africa kumuuguza ilibidi aende mdogo wake. Alivyopona tu alikuja Tanzania akatuomba msamaha, tulimsamehe hivyo alirudi south kuendelea na Maisha yake ila tuko poa kabisa. Joy naye anaendelea vizuri mwezi wa 7 tunatarijia kula ubwabwa mdogo wangu antarajia kufunga ndoa. Hatuna ukaribu wa kivile ila tunawasiliana japo kidogo kidogo.
Baba naye ndoa yake inapumulia gas walitengana chumba na mama yetu wa kambo na mdogo wetu ni mdangaji maarufu Morogoro mjini. Yaani ni ameshindikana. Kwa baba mimi na Joy tuliacha kwenda kabisa nina miaka mitatu toka nilivyoenda mwaka 2021 sijawahi kukanyaga tena. Nikimmisi baba yangu huwa najitahidi kwenda na mabus ya kufika mapema moro na mtoto wangu tunafikia ofisini kwa baba jioni tunaru zetu Dar naondoka juu kwa juu.
Katika hekaheka zote hizo nimefanikiwa kujenga kakibanda kangu kadogo kazuri japo si kivile lakini kanaridhisha kapo Mbezi Msumi. Nitaarajia kuhamia kabla ya pasaka mwaka huu. Nina amani furaha na afya njema mimi na mtoto wangu tuko poa kabisa.
Sijutii kuwa single mother sababu mtoto wangu ananipa kila namna ya kupambana na ndiye mtu pekee niliye naye katika Maisha yangu japokuwa ni mdogo lakini ananipa furaha. Nina amani na sasa hivi naufanyia kazi msemo wa Joy naishi ulimwengu wangu kabisa. Mwanangu ndiye dunia yangu.
Asanteni kwa kuwa na mimi, niliyemkosea au kumkwaza kwa namna moja ama nyingine naomba anisamehe. Na samahani kwa kuwachosha ila nina Imani kuna mtu japo mmoja amejifunza kitu kutokana na historia ya Maisha yangu.
NAWAPENDA!
Mwishooooo.
asante piaK
Ahsante sana kwq simulizi yako hii nzuri
AmenUbarikiwe zaidi
haha wako wapi team Dav......Daah jamani dav kayaharibu maisha yake kwa tamaa na starehe za muda mfupi
Asante sana dada kidoti….Mungu akisaidia nitakuja kukutoa kwenye u single motherKiroho ni kuwa baada ya kutolewa mahali wewe ni mke halali kabisa wa Dav na kimila pia ukikutana na Hali kama hizo inabidi upambane kama mama mjengo na sio kukimbia.
Na kama humtaki tena inabidi urudishe mahali ili upate mwenza mwengine wa kufangamana na roho yako.
haha wako wapi team Dav......
jimbo liko wazi...😛
haha inabidi mkubali matoke hamna namnaTumepigwa kama mwenyekiti😂😂😂😂🤣🤣
asante kipenzi niko imara sana. kipindi cha nyuma kitu kidogo tu natoa machozi kama nimefiwa ila sasa nipo tofauti kabisa sitoi machozi yangu ovyo tena. nikikutana na changamoto natulia kwanza ndio naitafutia ufumbuzi sio wa kulia lia tena.Pole sana mdogo wangu,,, naaamini uliyopitia yatakufanya uwe imara zaidi!!
haha toka juzi nasubiria machungwa hata hutokei. wewe sasa si utanizika kabisaAsante sana dada kidoti….Mungu akisaidia nitakuja kukutoa kwenye u single mother